Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?

hiyo namba 5 aliyewasimamia Downs na Richmond ndiye huyohuyo aliyewashauri Tanesco kuvunja mkataba wewe kama wakili unaweza kulifafanua vizuri inakuwaje wakili anaweza kusimamia pande mbili zinazoingia mkataba bila kuathiri upande mmoja. lakini miongoni mwa wahusika wa hiyo kampuni no mjumbe wa bodi ya Tanesco
 
Watu wakihoji na kuonya mnawapiga risasi na kuwapa kesi za ugaidi, na bado.
 
Mbona wengi waliodhulumiwa na serikali ya Tanzania hawajatekeleza maeneo yao wanafanyiwa ushenzi tu na kupelekwa immigration na kusumbuliwa kila kukicha na kuanza kuwaita wauza madawa ya kulevya na vitimbwi vingi ili waondoke na maofisa wa serikali wachukue mali au wamuuzie mwingine ndio staili ya Tanzania kwa wawekezaji ambao sio wazawa na wazawa wananyanganywa bila kupepesa macho na wakileta jeuri wanafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi au bili ya TRA isiyolipika
 
Kama kuna wengi kama wewe wanafikiri hivyo ulivyosema basi Tanzania ina shida kubwa ya raslimali watu na inaelekea ni umekata tamaa ya maisha je kizazi chako utakiachia nini??
 
Hata ukivunja yote leo bado kuna sunset clause ambayo ni miaka kumi zaidi kwa hiyo Tanzania ijifunze kutokudhulumu watu kwa ubabe na ifukuze all foreigners so that no foreign person can own anything in Tanzania ndio hamtashitakiwa
 
Ajabu ni kwamba aliyejipostion katika mkao wa kula ana maoni tofauti kabisa na sisi tunavyoona dah hii nchi hii?????
 
Kaka Paskal shikamoo. Naomba tumia uwezo wako wote WA usomi, uanasheria na uandishi WA habari wako, kwenye Jambo hili la Bandari tumsikie Mzee wetu Kabudi ambaye namheshimu Sana aseme neno kuhusu nawe utuandikie thread ya kile alichosema kama alishiriki na hakushiriki na nini maoni yake. Naona nyie wote mnanivuruga Tu. Hasa Lisu kasema ukiunga mkono tu ina maana umelambishwa asali, vinginevyo huna akili. Yaani mwenye akili hatakiwi kuukubali. Dah

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Unafanya exploration kwa miaka 10 hayo madini utachimba lini.

Kampuni yenyewe uchwara, ukisoma vyombo mbali mbali share value zake imepanda mara dufu baada ya kutunikiwa hiyo tuzo.

Hata hao wachambuzi wanashangaa kampuni ambayo haikuwa na market value ata $10m dollar, imezawadiwa zaidi ya $110m how do you justify such damages.

Wanasheria wao wenyewe wamechukua kesi kwa ahadi tu wakishinda kuna malipo wakishindwa imekula kwao. Malipo yenyewe anadaiwa Tanzania.

Tanzania aikushiriki hiyo kesi, huyo jamaa kafungua shauri 2020 baada ya Magufuli, wakati eneo limetaifishwa toka 2017.

Wana siku 120 za ku-appeal hiyo decision hawatofanya.

Ukome kumsingizia Magufuli katika wenu wa kuifilisi nchi.
 
Sawa endelea kujifariji kwani hata ile ya eco bagamoyo mlisema hivyo hivyo baadae mkalipa kimya kimya ndege umerudi. Hii Watanzania walishiriki vizuri sana soma submissions zao na waliwata hawa watu mwaka 2022 kuelewana ikashindikana kwa hiyo
 
Sawa endelea kujifariji kwani hata ile ya eco bagamoyo mlisema hivyo hivyo baadae mkalipa kimya kimya ndege umerudi. Hii Watanzania walishiriki vizuri sana soma submissions zao na waliwata hawa watu mwaka 2022 kuelewana ikashindikana kwa hiyo
Hao ECO na Indiana hawana tofauti yoyote, wote mafisadi tu.

Ndio maana kwenye post uliyo quote mara ya kwanza nikaandika issue ya Tanzania pengine hakuna definition ya performance wala time frame ya kupima results.

Hawa watu wanachukua maeneo, wanayakalia. Wanasubiri yachukuliwe kwa mikataba ya ovyo nchi inayoingia; halafu baada ya hapo wanakimbilia arbitration.

Sisi raia atuoni hiyo mikataba (sijui wewe mwenzangu kama upo serikalini), kwa hivyo ni ngumu kuelewa kiwango cha uwekezaji na kupima kiwango cha damages wanazo tafuta.

Either way serikali pia ingeweza kuwa ina fungua kesi zake za damages tena it’s entitled to large sums of damages kushinda mwekezaji katika mazingira ya eco na huyu Indiana.

Muda waliokalia hayo maeneo serikali imetengeneza large loss of potential income kushinda mwekezaji ambae hajafanya kitu kwenye potential loss of income zake (up to the point of performance); if both parties are to assess the injury at the time of expropriation Tanzania has incurred larger loss.

Ni hivi hizo case ni za kutengeneza ndio maana serikali aijaenda arbitration kujitetea na hata hapa bado wana miezi minne ya kukata rufaa; they won’t do it.

Sasa kwanini ushangae wakilipa kama awakuona umuhimu wa kujitetea, au kufungua counter claims; ni deal za watu humo serikalini ndio maana wanapenda raisi kama ‘Bi Tozo’ wamchezee.
 
Naamini sio jambo jema kuwakejeli watu ulionao kwenye fani kuwa ni wabovu. Hii nikutaka kuwaaminisha watu kuwa wewe ni mzuri kuliko wao.
 
Sawa endelea kujifariji kwani hata ile ya eco bagamoyo mlisema hivyo hivyo baadae mkalipa kimya kimya ndege umerudi. Hii Watanzania walishiriki vizuri sana soma submissions zao na waliwata hawa watu mwaka 2022 kuelewana ikashindikana kwa hiyo
Hata hiyo BIT ya U.K. ime expire since 2004, sunset clause inawalinda wale waliongia mikataba during the period of 1994-2004 when the BIT was active for further 20 years; not contracts entered after 2004.

Ni kesi za watu humo serikalini hiyo aikuwa ya kushindwa huko.
 
Walikuwepo kwenye kesi nenda mtandaoni kaangalie ile ya Winshear na Tanzania nayo ni kama hiyo alafu utaelewa tatizo liko wapi. Tena kuna nyingine ya Montero nayo itakuja karibuni na nyingine zitaendelea kwa sababu ya utendaji na mfumo mbaya wa nchi
 
Hayo madini ndio yamepata thamani sasa kabla ya hapo yalikuwa bado kwa hiyo huwezi kuja kimfukuza yule alikuwepo zamani kwa sababu sasa hiyo madini yanahitajika ni kama vile umnyanganye mtu ardhi kwa sababu hajajenga gorofa pale chole road baada ya kumuacha auze anufaike na mali yake. Kwani nani kawekeza sasa kwenye hiyo migodi huyo alipe??
 
Walikuwepo kwenye kesi nenda mtandaoni kaangalie ile ya Winshear na Tanzania nayo ni kama hiyo alafu utaelewa tatizo liko wapi. Tena kuna nyingine ya Montero nayo itakuja karibuni na nyingine zitaendelea kwa sababu ya utendaji na mfumo mbaya wa nchi
Labda uweke hiyo link inayoonyesha serikali walitokea kwenye arbitration.

Decision niliyoona mimi Tanzania aija respond kwenye hayo madai ya Indiana.

Ila wana siku 120 za kutoa pingamizi toka tarehe ya maamuzi bila ya kufanya hivyo zikipita hizo siku hayo maamuzi ni enforceable.

Ni hivi kama na wewe ni sehemu ya wanufaikaji ni muda wa kuambizana inatosha na kumwambia huyo mama airudishe nchi alipoikuta 2021 na kufungasha virago 2025.

Kabla ya kufungusha atuwekee mtu sahihi anaeweza kasi ya 2015-2021 ameifanya nchi imerudi kuwa ya ovyo sana ndani ya muda mfupi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…