Katiba Mpya: Kakobe aungana na Wapinzani Jangwani

Katiba Mpya: Kakobe aungana na Wapinzani Jangwani

Kama Kakobe ni mtu wa Mungu, mbona anachanganya ya Kaisari na ya Mungu?

Kakobe ni mwana mazingaombwe, hana lolote ni anajua mazingaombwe. Kwani wanamazingaombwe wengi si wamejiingiza kuwa maaskofu.
 
Kuna misukule humu jf hasa kwenye hii thread,ni wajinga wawili Chabruma na kati kati au ni ufinyu wa akili au ni nini

kati kati
Mtu anapimwaje kwamba amefeli? Unatumia vigezo gani? Wewe je umejipima kwamba unamaisha kama yake?

Chabruma
Hivi katiba ni ya watu wa aina gani? Mbona mnataka kuonyesha watu upumbavu wenu? Hamna wala mbwa huku wewe tumieni akili japo kidogo
 
Last edited by a moderator:
Kama Kakobe ni mtu wa Mungu, mbona anachanganya ya Kaisari na ya Mungu?

Kuwa mtumishi wa Mungu kunamuondolea Kakobe haki ya kutoa maoni yake kama mwananchi!!?...Ikiwa watu Km Kakobe watakaa kimya na hatimaye nchi ikaingia kwenye machafuko je atakuwa kiongozi wa nani??..Biblia inasema imani pasipo matendo imekufa..sasa ikiwa tunaiombea amani nchi hii makanisani..kwa nini watu km Kakobe wasitoe michango yao ili kuzidi kuidumisha amani!!?..
 
Kakobe ni opportunist

Uko sahihi sana...jamaa ana uchu na pesa...na anatafuta mavumba kwa nguvu zote!!! maana hata dini ni mwamvuli wake tu wa kujificha...na ndio maana waumini walikuwa hawaavai madhahabu kanisani kwake wanaogopa watachangia kanisa bila kupenda!
sasa hivi karudi kwenye siasa kwanini? anatafuta pesa maana siasa ni pesa!!!
 
Kwani Kakobe kakosa nini kumshauri rais juu ya katiba? sini raia wa Tanzania kama wengine? mbona wengi tu wanashauri?

Amekosea kumashauri kupitia majukwaa ya kisiasa, kama anajiona ananafasi ktk jamii angemshauri yeye kama yeye kwa kuomba kuonana nae au kupitia madhabahu ya kanisa lake
 
Kakobe ni mwana mazingaombwe, hana lolote ni anajua mazingaombwe. Kwani wanamazingaombwe wengi si wamejiingiza kuwa maaskofu.

Sasa kama Kakobe ni mwanamazingaombwe anawezaja kuwa na wafuasi wengi na matawi mengi kiasi hiki na kukubalika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania..kiasi hata watu wa mataifa mbalimbali duniani kumwamini wakati wewe na hao maaskofu wenye nguvu za Mungu wanashindwa kufanya hivyo..ina maana mazingaombwe ya Kakobe yana nguvu kuliko nguvu za huyo Mungu wa hao!!?
 
Uko sahihi sana...jamaa ana uchu na pesa...na anatafuta mavumba kwa nguvu zote!!! maana hata dini ni mwamvuli wake tu wa kujificha...na ndio maana waumini walikuwa hawaavai madhahabu kanisani kwake wanaogopa watachangia kanisa bila kupenda!
sasa hivi karudi kwenye siasa kwanini? anatafuta pesa maana siasa ni pesa!!!

Kwani huko kwenye siasa aliwahi kugombea cheo gani ili tujuwe km alikuwa anatafuta pesa..sasa km hao waumini wanaogopa kuvaa dhahabu kwa kisingizio eti watachangia kanisa bila kupenda...sasa mbona hata mitaani hawavai hizo dhahabu na huko wanaogopa nini!!?...
 
Uombe Mungu Kikwete asikie vilio vya Watanzania walio wengi na hivyo kutosaini muswada huo wa katiba ya CCM hivyo kutoa muda zaidi wa Watanzania mbali mbali kuendelea kutoa maoni yao. Vinginevyo nina wasiwasi utabadili sana makanisa maana siku za usoni kama Kikwete atausaini mkataba huo basi viongozi wa madhehebu mbali mbali ya dini nchini wataungana na umoja huu wa vyama vitatu ili kuongeza nguvu katika kumshinikiza Kikwete ili asiingize nchi katika mgogoro mkubwa wa kikatiba. Hata kwa sekunde moja Kakobe hakuzungumzia katiba ya CHADEMA, CUF au NCCR katika mkutano ule bali alizungumza kuhusu katiba ambayo itakubalika na kila Mtanzania.

Pamoja na kuhitilafiana kwenye hili mimi heshima yangu kwako itabaki pale pale.

Alutta continua! continua!!!

😛eace:😛eace:😛eace:
Have a great day Mamndenyi 🙂🙂



BAK huwa nakupa respect siku zote,
lakini hili la kusema viongozi wa dini waanze kusimama
kwenye majukwa ya siasa siwezi kukubaliana na wewe hata kwa ncha ya upanga;

Kama wanatumia maneno ya Mungu wawahubirie watu wao kutenganisha mchele na pumba
lakini kwenda kwenye majukwaa ya siasa kwangu ni hapana, na once ningekuwa muumini wake
ningehama kanisa lake mara moja kwa kuwa haelewi hata anachokifanya. Kuweka Bibilia kando
na kuanza kufundisha katiba ya chama?????????
 
Kwenye hili nitamuunga mkono Kakobe kwa asilimia 100!!

Haiwezekani viongozi wa dini wasubiri wanasiasa wawaamulie mambo muhimu ya kwenye Katiba hadi uhuru wa kuabudu na mambo mengine yanayogusa waumini wao.

Swala la katiba ni moyo wa nchi na ndio sheria mama.Hata Kenya viongozi wote wa dini walikuwa wakali sana kwenye maamuzi kama haya ambayo ni dhahiri CCM wanataka kuyahodhi ili wafanye wanayotaka wao!

Kakobe tutakuunga mkono kwa hili tena tutaomba na Maaskofu wetu wa Kanisa Katoliki waje front haswa wasituchakachue!
 
Amekosea kumashauri kupitia majukwaa ya kisiasa, kama anajiona ananafasi ktk jamii angemshauri yeye kama yeye kwa kuomba kuonana nae au kupitia madhabahu ya kanisa lake
kama hujui mambo bora ukae kimya...ni sawasawa na kutaka mikate na chapati vipatikane counter ya Bar...ameongea siasa akatumia jukwaa la siasa..kanisani anahubiri biblia...kukutana naye kwani Raisi atakutana na wangapi!!?..km kuna mahara pa kuwasilisha maoni kwa pamoja kwa nn hasifanye hivyo!!?..
 
Kwenye Parokia yangu tulitangaziwa kwenye hili tusimame na Wakristo wa madhehebu yote ili mambo ya msingi yasiamuliwe ovyo na mwisho kuingilia hadi uhuru wa kuabudu!

Tuliambiwa tuhamasishe kila Mkristo (bila kujali dhehebu) ashiriki ili kulinda maslahi ya nchi na Ukristo! Najua si dhambi kila dini kuwa makini na uhuru wao wa kuabudu usiingiliwe kama jinsi kila kikundi kitavyosimama kulinda maslahi yao bila kuvunja Katiba iliyopo.

Katika swala la katiba huwezi kuzuia makundi yote kujadili maslahi yao kwa mapana bila kuvunja sheria zilizowekwa.

Kudos Kakobe!
 
kakobe ni raia wa tanzania so ana haki ya kuchangia maoni kama mtanzania swala la kufeli utafeli wewe na magamba wenzako
 
Tangu nianze kujua harakati za Kakobe kwenye maenea mbalimbali sijawahi kumuona au kushuhudia Zakaria Kakobe amefanikiwa kwenye mipango yake yoyote.

Hata huku kwenye siasa alikoamua kuingia tena kwa mara ya pili atafeli tena, alifanya hivyo mwaka 95 akimsapoti Mrema wakafeli wote sasa ameingia tena hatujui ataondoka na nani.

Doomsayers wapo wengi duniani, kama unafikiri dunia au maisha ni static; kaa hapo ulipo! The rest of us are looking at the optimistic and brighter Side of life, every resource and opportunity counts.
 
Kuyaelewa maandiko vibaya nao ni mtihani mwingine mkubwa kwa mbumbu wengi, tuangalie mifano kadhaa ya hao unaowaita watumishi wa Mungu na harakati zao za kisiasa wakati huo huo walikua wakimtumikia Mungu.
  1. Desmond Tutu, huyu alikua askofu wa Anglican Church kwa muda mrefu kule Africa kusini enzi za ubaguzi wa rangi, nimemfahamu miaka ya 80 enzi za Peter Botha kama rais wa nchi hiyo, moja kati ya hotuba zake naikumbuka hadi leo, ilikua mwaka 1985, alisema, kwa jinsi makaburu walivyo makatiri kama Yesu angekua hadi hadi sasa nadhani wangemnyonga.
  2. Siasa za Marekani husisha sana viongozi hao wa kiroho, uchaguzi wa awamu ya pili wa George Bush, mshindani wake alikua bwn John Kelly, huyu John ni Roman Cathoric, kwenye kampeni zake alionesha kuunga mkono ndoa za mashoga na utoaji wa mimba, Vatcan pamoja na kanisa la Roman Marekan wakatangaza kutokumuunga mkono kwa misimamo yake hiyo.
  3. Kwenye Biblia, Nabii Yeremia alikua akipinga na watawala (wanasiasa) hata wakamtupa kwenye dimbwi la matope, Mwafrica 1 (Mkushi) akamuokoa.
  4. Hivi unajua Yohana Mbatizaji kwanini alifungwa? Ni mtawala ndiye aliyeamua awekwe ndani na Happybirthday ya mtawala huyo huyo ikagharimu maisha yake kwa kukatwa kichwa.


Nashauri muwe mnasoma maandiko kwanza kabla hamjayatumia, kumbuka siasa ndio inayoyawala kila kitu, hata huo uhuru wa kuabudu ni maamuzi ya wanasiasa, Funguka!
usichanganye dini na siasa. Ya Mungu mpe Mungu na ya Kaisari mpe Kaisari
 
Sasa muraa wewe unakuja mujini na jembe utalima lami? mujini tunakuja na cv muraa mwache kakobe ale alivyotafuta kama vip na wewe fungua kanisa lazima uatawapata tu muraa huko ndo kujiajiri muraa kama kakobe
 
kama mnataka msiingiliwe anzisheni mchakato wa kuandika katiba mpya ya ccm,hamtawaonamaaskofu, masheh,wala watu wajukwaa la katiba ila kwa huu mchakato wa katiba ya jamhuri (Tanzania)ni wa watu wote mtatokwa sana na mapovu mwaka huu.moto moto moto moto...
 
Kakobe alionekana mkutano wa jangwani ulioitishwa na vyama vya siasa akihutubia.Swali alienda na gari ya kanisa au binafsi? Maana ana kesi aliyoshitakiwa ya kutumia mali za kanisa kisiasa kuzunguka nazo wakati wa kumpigia kampeni za uraisi Augustino Lyatonga Mrema miaka ile.

Ni muhimu kujua jibu la swali hili kujua kama mali za kanisa hazijatumika ndivyo sivyo.

Wengi tungekusifia sana kama ungehoji matumizi mabaya ya mali za umma yanayofanywa ya serikali ya CCM na sio mali za kanisa ambazo kimsingi waumini walizitoa kwa hiari yao na matumizi yake hayaathiri kwa kiasi kikubwa mustakabali wa nchi. Think
 
Kakobe alionekana mkutano wa jangwani ulioitishwa na vyama vya siasa akihutubia.Swali alienda na gari ya kanisa au binafsi? Maana ana kesi aliyoshitakiwa ya kutumia mali za kanisa kisiasa kuzunguka nazo wakati wa kumpigia kampeni za uraisi Augustino Lyatonga Mrema miaka ile.

Ni muhimu kujua jibu la swali hili kujua kama mali za kanisa hazijatumika ndivyo sivyo.

Tuambie gari la kanisa likoje na binafsi likoje ili tuweze kukupa jibu sahihi halafu hivi mtu akiwa na kesi haruhusiwi kusafiri? Ndugu tafuta kazi yenye staha sio kuja hapa janvini kupigania buku 7000/= unatia aibu ndugu.
 
Back
Top Bottom