Katiba Mpya: NEC ya CCM yatoa tamko kuwa serikali 2 ndio msimamo wa chama!

Katiba Mpya: NEC ya CCM yatoa tamko kuwa serikali 2 ndio msimamo wa chama!

Jk anaiua ccm kwa kuwafharau wanachi ndo maana walingangania hili bunge ligeuke bunge la katiba watumie wingi wao ila wakumbuke malipo ni hapa hapa mi nawalaani wao na vizazi vyao
 
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha NEC ni kama ifuatavyo:wajumbe wa kutoka Zanzibar wameridhia kuwa na mfumo wa serikali mbili kwa masharti ya kwanza Zanzibar isiwe nchi,pili rais wa Zanzibar mara zote atakuwa makamu wa rais,tatu waruhusiwe kukopa nje ya nchi na deni liwe la Zanzibar,nnekuondolewa kero zote.Hii ni hatari sana katika nchi ambayo watu wake wana kubali kuuza wenzao pindi wanapo pewa fursa ya kuwawakilisha.kama ingekuwa Enzi za mwalimu wajumbe wote kutoka Zaanzibar wange chapwa viboko.kwa sabau hiyo watanzania na wazanzibar msisubiri serikali tatu wenzenu wametuuza.
 
Jk anaiua ccm kwa kuwafharau wanachi ndo maana walingangania hili bunge ligeuke bunge la katiba watumie wingi wao ila wakumbuke malipo ni hapa hapa mi nawalaani wao na vizazi vyao

Yaani inasikitisha sana CCM inavyotuona mazuzu hivi hivi...yaani wanadiriki kujitungia na kujitangazia mustakabari wa nchi for their own political interests ...alafu wanajua ikitoka hapo bungeni ndo basi tena imepita maana inajua WTZ ndo zetu zitapigwa kura za NDIO mpaka basi , and then CCM watakuwa wameshinda...easy.

Kama Nape na wenzake wako busy kuandaa rasimu yao itakayokidhi serikali mbili pia kuangalia uwezekanao wa kuboresha Muungano , hasa Wizara ya mambo ya nje na mengine, haya mabunge ya katiba ya nini??? Tunapoteza 8. 2 Billioni wakati mahospitalini wajawazito wanalala kitanda kimoja watatu!!!!!!!!!!!!
 
Tamko hili la CCM-NEC linamuweka Rais J.K katika hali yenye kutoeleweka mbele ya jamii. Wiki iliyopita alifungua mkutano wa Tanzania Center for Democracy na kuwambia wahumbe kwamba wajumbe wanaoenda Dodoma kwenye Bunge la katiba wasiende na misimamo ya taasisi zao bali waende kwa maslahi ya Taifa. Jana kapiga U-turn na sasa CCM wanakwenda na Serikali mbili! Lakini kuna jingine pia. Kikwete alisema anataka katiba itakayodumu miaka 50 ijayo. Kwa kugangania serikali mbili katiba hii sidhani kama itadumu hata miaka 10 ijayo. Waingereza wanasema; It is dead on arrival. What a waste of money?
 
wajumbe wa NEC kutoka Tanganyika ni mazezeta,Wanzanzibar ni wajaja na makini ndio maana wao wanahakikisha wanakuwa na Rais wao,Serikali yao,Katiba yao na mawaziri wao kinyume na hicho kwao ni bora muungano ufe
 
Msimamo wa ccm ndio msimamo wa wananchi wote wa tanzania wapenda amani na maendeleo,anayepinga serikali MBILI huyo anataka kutubagua watanzania na kuleta chokochoko zisijo na tija!! Kidumu chama cha mapinduzi

Provided that na KERO ZOTE ZA MUUNGANO mtazimaliza hukohuko bungeni ili kamati za kumaliza kero zile historia kwa siku zijazo!!
 
Kikao cha siku 2 cha NEC ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kimemalizika na kutoa taarifa kupitia katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho,bwana Nape Nnauye kuwa wamekubaliana kuendelea na msimamo wa kuunga mkono serikali 2.

Pia,bwana Nape ameongeza kuwa watafanyia kazi changamoto za muungano zinazolalamikiwa ambapo wameendaa hoja za kuziwasilisha katika bunge la katiba.Hoja hizo ambaza amekataa kuzitaja ndio zitakuwa na maelezo ya namna ya kutatua kero za muungano

Katika hatua nyingine,Nape amesema hawatishiwa na hatua ya vyama vingine kwenda kwa wananchi kwani hata wao(CCM) wanaweza kwenda kwa wananchi na kuwaeleza jambo hilo.

CHANZO:ITV

MY TAKE:
Hatua hii ni sawa na kutangaza mgogoro mapema!

WALIKUA WAPI SIKU ZOTE WASISHUGHULIKIE HIZO KERO HADI KWENYE KATIBA MPYA?. kWA MAANA HIYO HATUNA KATIBA MPYA MANAKE WANANCHI WATAIKATAA HIYO YA KWAO ILIYOCHAKACHULIWA. HIYO NI KATIBA YA CCM SIYO YA TANZANIA, NA KIKWETE ATAKUA AMETUPIGA CHANGA LA MACHO MNAFIKI MKUBWA.
 
Msimamamo wa CCM ndio msimamamo wa wanyonge na wazalendo!

wazalendo kama mama na baba yako,nyie wapuuzi sana hv mnadhani mnaweza mkatuamulia aina ya katiba tuitakayo wakati maon yetu yako waz tunataka serekal 3,hv hata pesa na rasilimal zilizotumika kukusanya maon ya rasimu zote mbili bado haijawafungua macho nn wananch wanataka?fanyen ujing wenu kupitia uwing wa wabunge wenu wa ccm kuchakachua maon yetu ndan ya rasimu halafu tutawamaliza huku mitaan kwenye kura za maon.
 
Tamko hili la CCM-NEC linamuweka Rais J.K katika hali yenye kutoeleweka mbele ya jamii. Wiki iliyopita alifungua mkutano wa Tanzania Center for Democracy na kuwambia wahumbe kwamba wajumbe wanaoenda Dodoma kwenye Bunge la katiba wasiende na misimamo ya taasisi zao bali waende kwa maslahi ya Taifa. Jana kapiga U-turn na sasa CCM wanakwenda na Serikali mbili! Lakini kuna jingine pia. Kikwete alisema anataka katiba itakayodumu miaka 50 ijayo. Kwa kugangania serikali mbili katiba hii sidhani kama itadumu hata miaka 10 ijayo. Waingereza wanasema; It is dead on arrival. What a waste of money?
wajumbe wa NEC kutoka zanzibar ni wajanja na makini maana wanahakikisha utaifa wao uko palepale,wana Rais wao,Serikali yao,katiba yao na mawaziri wao,mazezeta ni kina Nape kutoka Tanganyika hawana chochote,Wanzanzibar ukiwakatalia hivyo wanavyotaka wako tayari muungano ufe
 
huo ni msimamo wa watu mazezeta kama ccm lakini wazanzibar ni makini na wajanja wanahakikisha utaifa wao haufi kwa kuwa na Rais wao,serikali yao,katiba yao na mawaziri wao kinuyme na hapo bora muungano ufe
 
Mbona kila siku tupo barabarani wewe unataka barabara ipi au kwa mtei zipo zingine unamaanisha.

Warioba aliisaliti CCM. Alipewa nafasi hiyo ya M'kiti wa Tume ya Katiba akiunganishwa na Salim na Butiku ambao wote walikuwa wapendwa wa Mwalimu na siasa zake, pakiwa na uhakika kuwa hatathubutu kumsaliti Mwalim au CCM. Kikwete hakuamini kuwa kumbe binadamu aweza kuwa NYOKA. Laiti Mwalimu angekuwa hai katu Warioba asingekubali asingetoka na ajenda ya serikali tatu. Salim huyo ndo angeruka kimanga. Naamini CCM ilibakia mdomo wazi baada ya kuona na kusikia usaliti wa Warioba na wenzake. Mzee Mkapa alimuelewa vzri Warioba, ndo maana hakumpa madaraka ktk kipindi chake chote cha urais zaidi ya kumpa kuongoza ile Tume iliomjeruhi Nalaila Kiula. Hakumtaka kabisa. Ona sasa ameweka CCM ktk mtihani mkubwa wa kugeuza suala la serikali 3. Msiomfahamu Warioba ndo zake. Haaminiki kabsaaa. Ana uchu wa madaraka kweli kweli baada ya Mzee Ruksa kumuonjesha u W/Mkuu ambao nao ulimshinda. Anadhani ktk mfumo wa serikali 3 anaweza kupata mojawapo ya nafasi 3 za urais. Mh, nani akupe!!! Ng'o sahau kabisa. CCM sasa wamekufahamu vizuri rangi zako zote. Mauimivu ulowapa hawatayasahau.
 
Tamko hili la CCM-NEC linamuweka Rais J.K katika hali yenye kutoeleweka mbele ya jamii. Wiki iliyopita alifungua mkutano wa Tanzania Center for Democracy na kuwambia wahumbe kwamba wajumbe wanaoenda Dodoma kwenye Bunge la katiba wasiende na misimamo ya taasisi zao bali waende kwa maslahi ya Taifa. Jana kapiga U-turn na sasa CCM wanakwenda na Serikali mbili! Lakini kuna jingine pia. Kikwete alisema anataka katiba itakayodumu miaka 50 ijayo. Kwa kugangania serikali mbili katiba hii sidhani kama itadumu hata miaka 10 ijayo. Waingereza wanasema; It is dead on arrival. What a waste of money?
That guy is hypocrite!
 
Mimi nadhani hakuna sababu ya CCM kuogopa ujio wa serikali tatu maana inaonyesha ndio mfumo wananchi wengi wanoutaka na ni hisia zangu hautakuwa na madhara yoyote. Wananchi wa Tanganyika wanatka kuwa na serikali yao kutokana na kelele za wazanzibari kusema wanaonewa hali watanganyika nafasi zao nyingi zimechukuliwa nao. Nadhani wakati umefika kila mtu apewe uhuru wa kuamua mambo yake ya ndani na kushirikiana yaly yatakayokuwa ya muungano.
 
Serikali hata iwe moja,Tanganyika iwepo.Wabunge wanawakilisha watu na si chama.Tume imewafikia asilimia kubwa ya watu (raia) wa Tanzania,na 64% walisema serikali tatu,sasa hii ya CCM inatoka wapi?kulikuwa na sababu gani ya tume kama CCM wana agenda yao!
 
Warioba aliisaliti CCM. Alipewa nafasi hiyo ya M'kiti wa Tume ya Katiba akiunganishwa na Salim na Butiku ambao wote walikuwa wapendwa wa Mwalimu na siasa zake, pakiwa na uhakika kuwa hatathubutu kumsaliti Mwalim au CCM. Kikwete hakuamini kuwa kumbe binadamu aweza kuwa NYOKA. Laiti Mwalimu angekuwa hai katu Warioba asingekubali asingetoka na ajenda ya serikali tatu. Salim huyo ndo angeruka kimanga. Naamini CCM ilibakia mdomo wazi baada ya kuona na kusikia usaliti wa Warioba na wenzake. Mzee Mkapa alimuelewa vzri Warioba, ndo maana hakumpa madaraka ktk kipindi chake chote cha urais zaidi ya kumpa kuongoza ile Tume iliomjeruhi Nalaila Kiula. Hakumtaka kabisa. Ona sasa ameweka CCM ktk mtihani mkubwa wa kugeuza suala la serikali 3. Msiomfahamu Warioba ndo zake. Haaminiki kabsaaa. Ana uchu wa madaraka kweli kweli baada ya Mzee Ruksa kumuonjesha u W/Mkuu ambao nao ulimshinda. Anadhani ktk mfumo wa serikali 3 anaweza kupata mojawapo ya nafasi 3 za urais. Mh, nani akupe!!! Ng'o sahau kabisa. CCM sasa wamekufahamu vizuri rangi zako zote. Mauimivu ulowapa hawatayasahau.

Kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa alipewa Uenyekiti ili atunge maoni kutoka kichwani mwake!? Mi naamini aliteuliwa kwa kuwa ni Jaji, hivyo atakuwa FAIR kuleta mrejesho HALALI wa kile Wananchi walichotolea maoni, na wala si kwa matakwa ya Chama fulani( Chama chake kikiwemo). Kama aliteuliwa ili kulinda maslahi ya KIKUNDI, nadhani nafsi yake ilimsuta kuleta majibu ya UONGO, hivyo kwa kuwa yeye ni Jaji akaona kupotosha HAIWEZEKANI akaleta majibu ya Watanzania walichopendekeza. Huyu hakuwa peke yake, walikuwepo na wadau wengine wengi tu ambao naamini walisimamia haki, kwa mfano Prof Kabudi, Prof Baregu, Dr Mvungi( R.I.P) na wajumbe wenzao wengine wengi makini na wenye ueledi, ambao wasingeweza kuleta UONGO, kwani hawakutumwa kuleta UONGO. Hivyo nimpe sifa Jaji Mzee Warioba na timu yake kwa kuleta majibu ya Watanzania. Wale wote waliokuwa wanasema Tanganyika inawanyonya Zanzibar kwa unafiki sasa wako kimya. Ila wale waliosimamia na kuamini kuwa Tanganyika inawanyonya ZNZ, wanafurahi, kwani walipendelea Tanganyika Huru irudi, Zanzibar Huru iendelee halafu tuwe na Serikali ya Muungano.
 
Wana jf nimekuwa nikijiuliza ni kwa sababu gani CCM hawataki kabisa serikali 3, ni jana tu nimemuona Mizengo Pinda anadai eti hata akiamshwa usingizini atataja serikali 2.Ni kwa sababu zipi haswa?
 
Nimekuwa nikijiuliza kwa nini wadau wengi na wapenda muungano wamekuwa wakitetea serikali mbil na sio moja au kuelekeza nguvu kuishauri znz kufuta serikali yao?
 
Back
Top Bottom