Katiba Mpya: NEC ya CCM yatoa tamko kuwa serikali 2 ndio msimamo wa chama!

Katiba Mpya: NEC ya CCM yatoa tamko kuwa serikali 2 ndio msimamo wa chama!

Kwani kulikuwa na haja ya kutangaza wakati hilo linajulikana ? Huu ni ujinga kupinga maoni ya wananchi ambao keshoutaenda kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza wakati hujalifanyia maoni yao ........

Tumia akili wewe, jibu hoja, acha kulia lia hapa.
 
Kumbe bado walikuwa wanajadiliana? Mimi nilidhani wanao msimamo tangu awali. Inaelekea kuna mvutano ndani ya CCM kuhusu idadi ya serikali za muungano
 
Najiuliza maswali yafuatayo nakosa jibu:-1.Hivi tumekaa na changamoto za muungano au kasoro ndogondogo kwa muda gani na kushindwa kupata suruhu ya pmj.2.Leo hii nchi hii ikagawanyika watabaki na aina gani ya muundo ktk nchi na aina gani ya nchi.Ni busara gani itatumika ktk kupata aina ya muundo wa serikali itakaokuwa na faida kwa vizazi vijavyo (miaka 50).Pia natafakari kama ni kuepuka gharama kwa nini tusibaki na nchi moja.Watanzania tusiwe na akili ya mbayuwayu,wakati wa kula ya maoni tutoe maoni kwa mujibu wa uwezo wa akili aliotupa mungu na si akili ya kushikiwa na aina yoyote ya vyama.
 
Kikao cha siku 2 cha NEC ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kimemalizika na kutoa taarifa kupitia katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho,bwana Nape Nnauye kuwa wamekubaliana kuendelea na msimamo wa kuunga mkono serikali 2.

Pia,bwana Nape ameongeza kuwa watafanyia kazi changamoto za muungano zinazolalamikiwa ambapo wameendaa hoja za kuziwasilisha katika bunge la katiba.Hoja hizo ambaza amekataa kuzitaja ndio zitakuwa na maelezo ya namna ya kutatua kero za muungano

Katika hatua nyingine,Nape amesema hawatishiwa na hatua ya vyama vingine kwenda kwa wananchi kwani hata wao(CCM) wanaweza kwenda kwa wananchi na kuwaeleza jambo hilo.

CHANZO:ITV

MY TAKE:
Hatua hii ni sawa na kutangaza mgogoro mapema!

Safi sana, Msimamo wa CCM sio Msimamo wa Watanzania, na bahati nzuri si watanzania wote ni wana ccm. Hivyo hilo wala halitutishi, wakiamua wawe na serikali mbili hao ni CCM lakini kauli ya Wananchi kupitia Tume ya Jaji Wayoba iko wazi na dhahiri. Atakaye amua kughiribu akili zetu yeye ang'ang'anie Msimamo wa serikali mbili. Hizo ni kauli za watu waliolewa madaraka na sasa wameamua kuaga Ikulu ili wajaribu kuwa wapinzani. Mwenendo, Kauli na Tabia za Viongozi na wafuasi wa CCM zinadhihirisha kwamba wamechoka kuongoza dola sasa wameamua kupinga hata maoni ya wengi, kwa nini tunawabembeleza tuwangojee kwenye boksi la Kura ili wakae pepmbeni kidemokrasia....
 
kulikuwa na haja gani ya kuunda tume ya kupita na kukusanya maoni kwa wanachi ikiwa maoni ya ccm ndio yanayofaa kuwa katiba ya tanzania?

mbona chadema nao wanasema wanataka serikali tatu,inamaana wananchi wote wanataka serikaki tatu,kila chama kina wawakilishi wake na kila chama kinatetea mambo yake,sioni ubaya wa ccm kusema wanataka serikali 2 maana ndio msimamo wao kama chadema wanavyotaka serikaili 3
 
Kikao cha siku 2 cha NEC ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kimemalizika na kutoa taarifa kupitia katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho,bwana Nape Nnauye kuwa wamekubaliana kuendelea na msimamo wa kuunga mkono serikali 2.

Pia,bwana Nape ameongeza kuwa watafanyia kazi changamoto za muungano zinazolalamikiwa ambapo wameendaa hoja za kuziwasilisha katika bunge la katiba.Hoja hizo ambaza amekataa kuzitaja ndio zitakuwa na maelezo ya namna ya kutatua kero za muungano

Katika hatua nyingine,Nape amesema hawatishiwa na hatua ya vyama vingine kwenda kwa wananchi kwani hata wao(CCM) wanaweza kwenda kwa wananchi na kuwaeleza jambo hilo.

CHANZO:ITV

MY TAKE:
Hatua hii ni sawa na kutangaza mgogoro mapema!

Wajikumbushe tu kilichotokea Draft ya BOMAS nchini Kenya....
 
chadema walivyosema wanataka serikali 3 wametangaza nini?
kila chama cha siasa kilichosajiliwa kimepewa nafasi ya uwakilishi katika bunge la katiba we unafikiri hizi nafasi watazitumiaje? kila chama kipo huru kutangaza misimemo yake,uwingi wa wajumbe wa ccm bungeni usikupeshida,maana hata huku mitaani ccm inawanachama wengi ushahidi angalia matokeo ya chaguzi ndogo na kubwa,waacha ccm watangaze msimamo wao,ni sawa na chadema walivyotangaza,tuache ushabiki wa kipumbavu
 
akiri fupi sana. Yana anaandaa hoja kujibu sababu za serikali na jinsi ya kutatua migogoro ya muungano? kwa nini hawakuziandaa mapema na kuzitatua kabla ya katiba mpya..?
 
Mimi huenda nikaungana na msimamo wa ccm, sababu kuu kuna wachochezi wa kiislamu wana ajenda zao za siri kwenye serikali3.
 
Mimi huenda nikaungana na msimamo wa ccm, sababu kuu kuna wachochezi wa kiislamu wana ajenda zao za siri kwenye serikali3.

Inaonesha hata ukienda haja chooni pia unawaza udini.
 
Kwa hiyo na sisi tunataka kama hizo za Ujerumani kwa maana tuwe na serikli ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika?, kama ni hivyo sawa, sasa hapo hauwi Muungano tena. Logic za serikali3 ni kuwaridhisha tu wale wanaotaka kujitawala, vinginevyo serikali ifaayo ni moja jamani, tuache kujitoa ufaham wakati ukweli tunaujua. Ila serikali mbili kwa muktadha wa huu mfumo wa SJMT na SMZ si sahihi hata kidogo.

1392658234202.jpg
Tunataka serikali moja tu hakuna ya Zanzibar wala ya Mungano
 
Njama za CCM ni kukwamisha katiba mpya isipatikane ili uchaguzi ujao ufanyike chini ya katiba hii mbovu.
Lakini mi nawatahadharisha, wafanye wafanyavyo... hata chini ya katiba hii mbovu uchaguzi mkuu ujao wanapigwa vibaya...
 
Mchakato mzima wa kuandaa katiba mpya umeshanajisiwa na kikundi cha watu wachache wanaojivisha mwamvuli wa CCM. Ni aibu na fedheha iliyoje kama maoni na matakwa ya wananchi wa Tanzania wasiopungua asilimia 61 ya wananchi wote wa Tanzania yatabinywa na kuburuzwa na kikundi cha watu wasiozidi 200. Ni vyema sana Kikwete na marafiki zake akatambua wazi kuwa anakotaka kuipeleka nchi yetu sio kuzuri. Akina Nape na wengineo hawana tofauti na wanaopuliza vuvuzela ambao kwao wanaamini kila mtu anafurahia kelele wanazopiga

Katika hili ni vyema wananchi na kila anayelitakia mema taifa letu akaona wazi kuwa wamepuuzwa, kudharauliwa na mbaya zaidi wamebaguliwa kwa maoni na matakwa yao kupuuzwa na wasimame katika maneno na msimamo wa Marehemu Mzee Nelson Mandela kama inavyonukuliwa:

On discrimination; “I consider myself neither morally nor
legally obliged to obey laws made by a parliament in which I am not
represented.
”

Hakika huu udhalimu na dhambi inayofanywa na akina Nape kwa kutumia nguvu ya Kikwete italeta maafa makubwa na hakuna jinsi wataweza kukwepa lawama na kila kitakachotokea kutokana na hila na ghiliba zao.
 
mbona chadema nao wanasema wanataka serikali tatu,inamaana wananchi wote wanataka serikaki tatu,kila chama kina wawakilishi wake na kila chama kinatetea mambo yake,sioni ubaya wa ccm kusema wanataka serikali 2 maana ndio msimamo wao kama chadema wanavyotaka serikaili 3

usisahau kuwa asilimia 67 wali_pendekeza serikali tatu!
 
Back
Top Bottom