Katiba Mpya: NEC ya CCM yatoa tamko kuwa serikali 2 ndio msimamo wa chama!

Katiba Mpya: NEC ya CCM yatoa tamko kuwa serikali 2 ndio msimamo wa chama!

Bw,simiyuYetu jaribu kutumia kichwa kufikiri,usjitoe akili kwa sababu ya kibaba cha siku moja,watu wa aina yako ni hatari sana katika jamii,sisi hapa Unguja wallah hatutakubali katu kuendelea kufunikwa na Serikali ya Muungano,tumeshindwa kwa miaka mingi kupata maendeleo ya Nchi yetu sababu ya upuuzi huu.

Waeleze hao na sisi huku Tanganyika pia tumechoka tunaitaka Tanganyika yetu.
 
Wewe ni mmoja kati ya MAADUI wa Zanzibar.

Kwa kweli waweza kuniita majina mengine utakavyo...kwenye hili siwezi kujifunza unafiki...nafsi yangu haiko tayari kukubali kuwa na serikali ya Zanzibar yenye mamlaka kamili huku Tanzania bara hikisemekana ndiyo imebebwa na serikali muuungano.

Kama Zanzibar wanataka uhuru kamili...basi Tanzania bara ipewe uhuru kamili....kama tunataka muungano Zanzibar ifutwe..na Tanzania Bara (ingawa wengine upenda kuiita Tanganyika) isirudi, bali tuwe na serikali moja ya Jamhuri ya Muungano wa watu wa Tanzania huku tukiwa na rais mmoja tu. Hicho ndicho nafsi yangu inanituma inanisukuma kusema hapa jukwaani. Na nafsi yangu haijaanza leo kunisukuma kunituma niliseme hili.
 
Serikali tatu ndiyo mdudu gani unatuletea hatutaki serikali za majaribio ulishawahi kuona wapi duniani muungano wa serikali tatu kama siyo mambo ya kihuni.

Wewe ulishawahi kuona wapi serikali2 duniani kama siyo usanii tu.
 
Wewe ulishawahi kuona wapi serikali2 duniani kama siyo usanii tu.

Serikali mbili ziliwahi kuwepo...ambazo ni serikali ya ujerumani magharibi na ujerumani mashariki....lakini zilipoungana zilifanya serikali moja ya ujerumani...ndiyo maana kuna rais mmoja na kuna 'kansela' mmoja Angela M, wala hawana marais watatu nakadalika nakadhalika....ndiyo maana nasema kama nchi hizi (Tanzania Bara na Tanzania Visiwani) zina taka mamlaka kamili basi tuwe kama zilivyokuwa Ujerumani magharibi na Ujerumani Mashariki au kwa sasa Korea Kusini na Korea ya Kaskazi (Zamani ilikuwa Korea Moja). Ila kama tunataka kuungana basi tuungane kama ilivyo Ujerumani ya sasa.... kama hatutaki basi tuwe kama Korea kaskazini na Korea ya Kusini za sasa. Habari za serikali Tatu au serikali mbili eti ya muungano na moja serikali kamili kwa kweli kwa lojiki ni kuchezeana akili.
 
Serikali mbili ni sawa, lakini ziwe ni ya Zanzibar na ile ya Tanganyika! Otherwise hamna haja ya katiba mpya.
 
Naona dalili za kupata katiba mpya sasa zimeeanza kuonekana mapema serikali mbili ndiyo mpango mzima ndiyo zimetufikisha hapa tulipo.

Zimetufikisha hapa ambapo leo hii mtu kama wewe unaweza kutoa maoni yako bila kuzuiliwa kama unavyofanya hivi sasa.
 
Serikali mbili ziliwahi kuwepo...ambazo ni serikali ya ujerumani magharibi na ujerumani mashariki....lakini zilipoungana zilifanya serikali moja ya ujerumani...ndiyo maana kuna rais mmoja na kuna 'kansela' mmoja Angela M, wala hawana marais watatu nakadalika nakadhalika....ndiyo maana nasema kama nchi hizi (Tanzania Bara na Tanzania Visiwani) zina taka mamlaka kamili basi tuwe kama zilivyokuwa Ujerumani magharibi na Ujerumani Mashariki au kwa sasa Korea Kusini na Korea ya Kaskazi (Zamani ilikuwa Korea Moja). Ila kama tunataka kuungana basi tuungane kama ilivyo Ujerumani ya sasa.... kama hatutaki basi tuwe kama Korea kaskazini na Korea ya Kusini za sasa. Habari za serikali Tatu au serikali mbili eti ya muungano na moja serikali kamili kwa kweli kwa lojiki ni kuchezeana akili.

Kwa hiyo na sisi tunataka kama hizo za Ujerumani kwa maana tuwe na serikli ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika?, kama ni hivyo sawa, sasa hapo hauwi Muungano tena. Logic za serikali3 ni kuwaridhisha tu wale wanaotaka kujitawala, vinginevyo serikali ifaayo ni moja jamani, tuache kujitoa ufaham wakati ukweli tunaujua. Ila serikali mbili kwa muktadha wa huu mfumo wa SJMT na SMZ si sahihi hata kidogo.
 
Kikao cha siku 2 cha NEC ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kimemalizika na kutoa taarifa kupitia katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho,bwana Nape Nnauye kuwa wamekubaliana kuendelea na msimamo wa kuunga mkono serikali 2.

Pia,bwana Nape ameongeza kuwa watafanyia kazi changamoto za muungano zinazolalamikiwa.

Katika hatua nyingine,Nape amesema hawatishiwa na hatua ya vyama vingine kwenda kwa wananchi kwani hata wao(CCM) wanaweza kwenda kwa wananchi na kuwaeleza jambo hilo.

CHANZO:ITV

MY TAKE:
Hatua hii ni sawa na kutangaza mgogoro mapema!

CCM wametoa msimamo wao. Ni vizuri vyama au vikundi vingine navyo vitoe msimamo wao halafu twendeni kwa wananchi tukawaelemishe juu ya mfumo wa Serikali Mbili na Serikali Tatu. Tuwape nafasi ya kuamua mfumo upi wanaupenda na kuona utawafaa kwa maisha yao. Nina imani kubwa kuwa, atayeshinda ktk vita hii ndio atakayeshinda uchaguzi mkuu ujao wa 2015.
 
Kwanini kikwete hataki mambo yooooote ya Nyerere isipokuwa serikali mbili pekee?
 
Naona dalili za kupata katiba mpya sasa zimeeanza kuonekana mapema serikali mbili ndiyo mpango mzima ndiyo zimetufikisha hapa tulipo.
Ni kweli simiyu yetu, serikali mbili zimetufikisha hapa ktk migogoro ya muungano, ubadhirifu wa rasilimali na kutowajibika. Inashangaza kuona nec inaanza kukusanya maoni ya vigogo wake baada ya kuwa time ya warioba imesha kamilisha kazi yake. Kweli ccm ni janga na haiitakii mema nchi yetu
 
Kwanini kikwete hataki mambo yooooote ya Nyerere isipokuwa serikali mbili pekee?

Azimio la Arusha wameua, ujamaa hawautaki,miiko ya uongozi pia ila serekali mbili ndio wanaoijua .
 
Huu ni uwendawazimu , kupinga walichoamua Watanzania ni uhaini kwa umma.ccm inalaana mbaya sana.
 
Back
Top Bottom