Kikao cha siku 2 cha NEC ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kimemalizika na kutoa taarifa kupitia katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho,bwana Nape Nnauye kuwa wamekubaliana kuendelea na msimamo wa kuunga mkono serikali 2.
Pia,bwana Nape ameongeza kuwa watafanyia kazi changamoto za muungano zinazolalamikiwa.
Katika hatua nyingine,Nape amesema hawatishiwa na hatua ya vyama vingine kwenda kwa wananchi kwani hata wao(CCM) wanaweza kwenda kwa wananchi na kuwaeleza jambo hilo.
CHANZO:ITV
MY TAKE:
Hatua hii ni sawa na kutangaza mgogoro mapema!