Katiba Mpya: NEC ya CCM yatoa tamko kuwa serikali 2 ndio msimamo wa chama!

Katiba Mpya: NEC ya CCM yatoa tamko kuwa serikali 2 ndio msimamo wa chama!

Mm hili linanitaiza kidogo pale CCM wanaposema msimamo wao ni Serikali 2 wakati ukirejea nyuma wakati wa uundwaji wa Mabaraza ya Kata na Wiliya wote mtakumbuka walikuwa na uwakilishi mkubwa sn zaidi ya 60% kiasi cha kulalamikiwa na vyama vya Upinzani.
Sasa km hoja ilikuwa hiyo walishindwaje kwenda kuwafunda hao wawakilishi wao na hoja hiyo ya Serikali 2 ingemalizikia huku huko kwenye Rasimu ya kwanza kabla ya hii Rasimu ya 2.
Sasa km hata wawakilishi hao wa CCM kwny mabaraza ya katiba walikubali Serikali 3 hawa NEC ya Ccm wanawakilisha misimamo ya wanachama wapi au ni Msimamo wa viongozi wa ngazi za juu wa CCM.?
 
CCM acheni ujinga, kutoa msimamo wa chama kwenye masuala ya kitaifa ni uzezeta wa akili. Hii sio katiba ya chama cha mapinduzi. Watz zaidi ya 60% wanataka serikali tatu kwa mujibu wa ripoti ya Jaji Warioba. Nyinyi hayo mawazo mnayatoa wapi?Msimamo wao watumie kujenga katiba ya chama chao na si kwenye katiba ya watanzania.
 
Wajikumbushe tu kilichotokea Draft ya BOMAS nchini Kenya....
Infact nimekua nashangazwa jinsi kifo cha CCM kimekua na mapito yale yale walimo pita KANU! Kwa namna hii ya matumizi mabaya ya fedha zetu kugharimia mchakato ambao mwisho unavurugwa kuzilinda familia chache huko Zanzibar zinazo nufaika na Muungano feki sina shaka kusema Kikwete amejihumu mwenyewe kukumbukwa kama mtu aliye leta Katiba ya kwanza iliyoandikwa kwa kushirikisha wananchi!
 
Ni vema kuliweka wazi hilo ili watanzania wasipotoshwe na wenye uchu wa madaraka

Kwa hiyo jaji Warioba ana uchu wa madaraka kweli mmeamua kujiondoa akili kabisaaa!
 
Kwanini kikwete hataki mambo yooooote ya Nyerere isipokuwa serikali mbili pekee?

Mentor wake aliye mtoa Newala akampa ubunge,unaibu waziri,uwaziri na mwisho akazunguka Tanzania nzima akimtafutia urais kwa kivuli cha mlezi wa baraza la misikiti ndiye amemgomea, ili waendelee kunufaika na pesa za Watanganyika!
 
Ndio maana nimeamua kubadili signature yangu ya JF!
"Wise men talk because they have something to say, fools talk because they have to say something"
 
Mbona kila siku tupo barabarani wewe unataka barabara ipi au kwa mtei zipo zingine unamaanisha.

Akili finyu ka funza bhana,kila anayekupinga ni upande wa cdm au mtei! Think great mkuu unajidhalilisha sana
 
Msimamo wa ccm ndio msimamo wa wananchi wote wa tanzania wapenda amani na maendeleo,anayepinga serikali MBILI huyo anataka kutubagua watanzania na kuleta chokochoko zisijo na tija!! Kidumu chama cha mapinduzi

Ama kweli unamihemko....yaani we had hapo asilmia64 ya watanzania huwaoni chochote wala lolote ila nec....ya ccm .....tafakur
 
Mm sijui hichi chama na wasemaji wake wwana matatizo gan maana mwenyekiti anasema watu waache itikadi za vyama karibu mwenez anasema msimamo wa chama juu ya katiba sasa swal jk alikuwa anamwambia nan
 
Mi najuliza ccm wanapata wapi hofu kwa kurudi Tanganyika na kuipenda Tanzania bara nchi ya kusadikika.karibu tena Tanganyika
 
Ni vema kuliweka wazi hilo ili watanzania wasipotoshwe na wenye uchu wa madaraka

Nadhani una uelewa mdogo kuhusu maana ya uchu wa madaraka!
Hata kung'ang'ania serikali mbili ni uchu wa madaraka pia!
 
Serikali mbili ni sawa, lakini ziwe ni ya Zanzibar na ile ya Tanganyika!
hata mimi naungana na CCM kuwa na serikali mbili zinazojitegemea yaaani Zanzibar na Tanganyika......maana yake hakuna Muungano.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kikao cha siku 2 cha NEC ya Chama cha Mapinduzi(CCM) kimemalizika na kutoa taarifa kupitia katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho,bwana Nape Nnauye kuwa wamekubaliana kuendelea na msimamo wa kuunga mkono serikali 2.

Pia,bwana Nape ameongeza kuwa watafanyia kazi changamoto za muungano zinazolalamikiwa ambapo wameendaa hoja za kuziwasilisha katika bunge la katiba.Hoja hizo ambaza amekataa kuzitaja ndio zitakuwa na maelezo ya namna ya kutatua kero za muungano

Katika hatua nyingine,Nape amesema hawatishiwa na hatua ya vyama vingine kwenda kwa wananchi kwani hata wao(CCM) wanaweza kwenda kwa wananchi na kuwaeleza jambo hilo.


CHANZO:ITV

MY TAKE:
Hatua hii ni sawa na kutangaza mgogoro mapema!
viongozi wa ccm hawana hoja kwenye hili, hivi inawezekanaje serikali ya Tanganyika iungane na Serikali ya Zanzibar alafu upate serikali mbili,ili liliwezekana wakati ule wa watanganyika walikuwa hawajasoma lakini kwa sasa haliwezekani kama kweli ccm wanataka muungano angalau wangesimamia serikali moja, hapo ndipo utapoona jinsi ccm wanajitoa akili kwa kusimamia kitu kisichowezekana, ivi ccm wanashindwaje kuelewa kwamba wanzanzibar kungangania kuwa na serikali yao maana yake ni kukataa muungano? kama kweli wazanzibar wanataka muungano wangeomba serikali moja,lakini kinachoshangaza ni kuona wazanzibar hawataki serikali ya Tanganyika lakini wanataka ya kwao iwepo,huu muungano wa kijinga watanganyika hatutoukubali cha msingi hapo ni Serikali moja au Tatu vinginevyo ni kila nchi iwe vyake tuwe majirani wema kama tulivyo na Kenya
 
Kutokana na tume ya uchaguzi hii ndiyo itakayosimamia uchaguzi wa kura ya maoni, na vile vile kura hizo huwa hazina mawakala wowote wa kulinda kura hizo, hapo ndipo bao la kisigino litakapoingizwa na kupitisha kile kitakachoamuliwa katika bunge hili la katiba lenye wabunge wengi wa ccm.
 
Back
Top Bottom