Katiba ya CCM haina suala la Ukomo wa muda wa uongozi.

Kuna vikao halali vinavyoruhisiwa kubadili katika lakini siyo kinyemela tunamuachia msajili afanye kazi yake.

una umiza kichwa bureee wameshakwambia tofauti ya2004 na2006
....vikao wanakaa wao wewe na mimi hatupo..waachieni lichama lao mbona husikiii.....
wewe kenya uganda na rwanda wameshaamua wanafanya mikutano yao pekee yao ...sisi tz tunaanza maneno inasaidia nini wakati wameshajitenga wanaendelea na mambo yao
 
Ni katiba ya ajabu muundo wake uko hivi:
-Mtei (mchagga) hakuna ukomo wa M/kiti
-Makani (msukuma) M/kiti vipindi viwili
-Mbowe (mchaga) hakuna ukomo wa M/kiti

Yaani mwenyekiti akiwa mchagga hakuna ukomo ila akiwa kabila nyingine ukomo upo?

 
Ukiangalia kwa makini kwa jicho la tatu utagundua madhaifu ya wanaccm kwenye masuala kadhaa ya msingi.

1. Wako radhi wakomae na matatizo ya chadema kuliko walivyo radhi kukomaa na matatizo ya chama chao. CHADEMA ilishatoa ufafanuzi wa swala la katiba, sisi wana CHADEMA wenyewe hatuna mashaka, wao wana mashaka zaidi na sisi kuliko wanavyopaswa kuwa na mashaka na mambo yao.

2. Hawawapendi viongozi wa juu wa CHADEMA hasa mwenyekiti na katibu ambao misimamo yao na utendaji wao umesaidia sana kuikuza CHADEMA. Hawataki kujifunza ili wakinusuru chama chao juu ya kauli za mwenyekiti wao za kuacha rushwa maana kinaenda kufa, hawataki kuumiza kichwa juu ya tuhuma za katibu wao kuhusishwa na ujangili na yeye kukiri.

3. Ccm wana aina ya viongozi ambao wao ndio wana mahaba nao walioko CHADEMA na wanataka wawe kwenye uongozi wa juu wa CHADEMA kuliko viongozi wengine. Sarakasi za upotoshi wa katiba ni kuwatetea watu wao. Ccm hao hao hawana muda kudeal na matatizo ya kiuongozi ndani ya chama chao. Uongozi ndani ya ccm unapatikana kwa mafurushi ya fedha. Hawana muda na hilo ila wana muda na uongozi utakavyo patikana CHADEMA.

Mengine yanasikitisha zaidi...

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wewe na Mwigamba nani alikuwa na nafasi nzuri ya kujua? Mwigamba amesema kuna uchakachuaji.
 
Wewe na Mwigamba nani alikuwa na nafasi nzuri ya kujua? Mwigamba amesema kuna uchakachuaji.

we mwehu mimi na wewe tumsaidie mwigamba asipigwe tena awaachie lichama lao ya nini kungangania
 
Ahsante kwa ukiri Chadema ina matatizo.

 
we mwehu mimi na wewe tumsaidie mwigamba asipigwe tena awaachie lichama lao ya nini kungangania
Asipopigwa Mwigamba watapigwa wengine maana wana madai ya msingi lazima wayaseme.

 
Ni katiba ya ajabu muundo wake uko hivi:
-Mtei (mchagga) hakuna ukomo wa M/kiti
-Makani (msukuma) M/kiti vipindi viwili
-Mbowe (mchaga) hakuna ukomo wa M/kiti


Mtajaribu sana kupandikiza ukabila, haitasaidia...!!
Mtajaribu sana na mengine mwngi, haitasaidia...!!

Katiba ya CCM haina ukomo wa uongozi, huko nako kuna 'ukabila'..??
Poleni sana wana-CCM, Chadema inawasumbua sana.
 
Asante sana Mwanaukweli,angalau umerudisha kumbukumbu, operation chaos!!
Tuwe imara kwa viongozi wetu wenyewe wasije wakakata tamaa,kumbe walijua Mbowe amesurrender kumbe changa la macho.Wanataka kutulazimishia Zitto,sisi hatumtaki( hata kama kaaga kigoma)
 

Usitafute pakutokea, huna. Labda wadanganye misukule, wenye nazo timamu huwezi kuwababaisha kijinga.

Kwa hili naona hata misukule watakucheka. Hebu jisomee mtiririko wa suala la katiba ya chadema na uwache unazi usio na mpango:


Huu utafiti ni wa Chabruma.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo wewe una uchungu na Chadema? Kwa hiyo wewe unataka Chadema iimarike?

Niambie nia ya wana CCM kushupalia hili ni nini? Kwa nini tunayepambana naye ndie atuchakulie kamanda?
 

FaizaFoxy, kwanza nikupe pole sana kwa 'kukerwa' na mabadiliko ya katiba Chadema.
Usiwe na wasiwasi, hauko peke yako katika kadhia hii, wengi sana kati ya wana-CCM wamekerwa sana na mabadiliko haya.

Hivyo cheer-up, you are not alone in the depth of sorrow..!! Si unajua tena 'kifo' cha wengi harusi...!!
Otherwise, mabadiliko ndio hayo, mkitaka yaondolewe, basi njooni Chadema muwe wanachama ili mpate haki ya kubadili katiba, vinginevyo, tuonane mwaka 2015 kwenye 'mtanange' wa uchaguzi mkuu..!!
Msalimie sana Ritz ingawa naona leo yuko 'mitini'...!!!
 
Tatizo katiba ya chadema imechakachuliwa kuwa hakuna ukomo wa muda wa mwenyekiti bila ya vikao halali. Umeona tofauti yake hapo?


kwa hiyo mmeo akiwa hakuridhishi unatoka nje na kuanza kupiga yowe au mnamalizana wenyewe!kwanini jirani ndiyo aje kumfundisha jinsi ya kukuridhisha,nahisi umeelewa,mimi ni mfuasi wa Chadema sjaona tatizo liko wapi!na kama lipo nitanyoosha mkono kwenye vikao vya chama na kuhoji,kushauri au kupendekeza,sio mCcm ndiyo ahoji,kama wanaona ni kizuri kipengele hicho wakiweke kwao kwanza,au tuamini kuwa ni uoga wao kwa vichwa vilivyopo(Mbowe,Dr.SLaa),kama umemuelewa mleta mada amekuwekea hadi andishi la W.Malecela hapa kwamba waongeze mashambulizi ili wahakikishe Mbowe na Slaa hawagombei tena,kumbe tatizo kwa maCcm siyo kuchakachua katiba,ni Mbowe na Dr.Slaa kama kawaida yao.
 
You are missing the point dude!

Tatizo sio kuwepo au kutokuwepo kwa kipengele.

Tatizo ni utaratibu unaotumika kuingiza na kutoa vipengele pamoja na kauli za UONGO zinazotolewa na viongozi waandamizi wa chama kulaghai watu juu ya utaratibu huo.

wewe CDM inakuhusu nini?
Wana-CDM wenyewe hawalalamiki mnapiga kelele nyinyi!
Au mbebadili sera za chama chenu na kuingiza hii ya kuilalamikia CDM ili muonekane mnafanya kazi mbele ya WaTZ?
Kazi yenu nynyi ni kutimiza sera zenu kwa WaTZ sio vinginevyo!
Tunataka elimu bora, muondoe ufisadi, kamateni wauza sembe, mrudishe ela zilizofichwa Uswis, ela za EPA, afay bora, maisha bora kwa kila Mtz.
Kuhujumu CDM haiwasaidii kitu, mnapoteza mda wenu bure ambao mgewatumikia WaTZ!
Au mnafikiri mkifanya hivyo ndio mtapigiwa kura au mtakubalika tena? No way!
Ondoeni udhaifu wote mlioshikilia ambao unalalamikiwa na WaTZ.
Kitendo cha kuhangaika na CDM na in my point of view kinawaondolea sifa zote za kuwa watawala!
Kinaonyesha jinsi mlivyo wavivu na humuwezi ushindani wa dunia ya leo!
Chama chenu ndio kinakusanya kodi yangu inayoendesha serikali hii! badala ya kuniletea maendeleo na kuniondolea matatizo nyinyi mko busy kuhangaika na CDM! Hiyo indio kazi mliyotumwa na WaTZ au mliowahaidi WaTZ?
Jitazameni njia mnayokwenda sio nzuri na haiwasaidii kabisa!
 
Yaani mwenyekiti akiwa mchagga hakuna ukomo ila akiwa kabila nyingine ukomo upo?

Husichanganye madafu tunaongelea CCM, na swali ni kwanini katiba ya CCM haina ukomo wa uongozi??
 

Msitujazie server.. tunaongelea CCM sio Chadema.. Na swali ni kuwa tangu CCm ilipozaliwa (1977 kama sikosei mpaka ) 2013) kwa nini hiki chama chetu kipendwa hakina ukomo wa madaraka? Nilitegemea chama kikomavu kama CCM kiwe ni mfano wa vyama vichanga. swali ni hilo tu.
 
Asipopigwa Mwigamba watapigwa wengine maana wana madai ya msingi lazima wayaseme.


Umelewe swali lakini? ni kuhusu CCM kutokuwa na ukomo wa madaraka na swali ni kwanini? hayo ya Mwigamba waache wafu wazikane sisi tuongelee juu ya chama chetu kipendwa!
 
Pasco usi -justify. Kama nia yako ni uchaguzi CDM huo haupo!! tutafanya 2015 tukimaliza uchaguzi mkuu - pole kama ulikuwa unautaka uwenyekiti.

Ndege ina-takeoff sasa - hatuwezi kubadilisha wana-anga!!!
 
Umepiga ngumi kwenye 'pressure point'. Misukule imeona imeingia mitini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…