Katibiwe ila fahamu kuwa tiba mbadala wote ni matapeli

Katibiwe ila fahamu kuwa tiba mbadala wote ni matapeli

Inaitwa placebo effect hata huku mahospitalini tunatumia kutibu watu kwa vidonge vya sukari! The trick is to convince your brain to treat itself kwa kuamini kupitia matibabu fulani ambayo kiuhalisia ni majani au mizizi tu au vidonge vyenye sukari japo zipo herbs zinazofanya kazi kweli.

Atleast wanakua wamekusaidia kuamni kwamba kupitia kitu fulani au Mungu fulani umepona japo kuwa placebos haziponyi zinatoa unafuu tu.
“The Pharmaceutical industry does not create cures. They create customers”
“Sekta ya Dawa haileti tiba. Wanatengeneza wateja”
THE PHARMACEUTICAL INDUSTRY.jpg

Nadharia kubwa za njama za Pharma

Nadharia za njama kubwa za Pharma ni nadharia za njama ambazo zinadai kwamba jumuiya ya matibabu kwa ujumla na makampuni ya dawa hasa, hasa makampuni makubwa, hufanya kazi kwa madhumuni mabaya na dhidi ya manufaa ya umma, kwamba huficha matibabu ya ufanisi, au hata kusababisha na kuzidisha aina mbalimbali za matibabu. magonjwa kwa madhumuni ya faida, au kwa sababu zingine mbaya.[1][2] Baadhi ya nadharia ni pamoja na madai kuwa tiba asilia za matatizo ya kiafya zinakandamizwa, madai kuwa dawa za kutibu VVU/UKIMWI hazifanyi kazi na zina madhara, madai kuwa tiba ya saratani zote imegunduliwa lakini imefichwa kwa umma. inadai kuwa chanjo za COVID-19 hazifanyi kazi, na kwamba tiba mbadala zinapatikana kwa COVID-19. Katika kila kisa wananadharia hao wa kula njama wamelaumu kampuni za kutengeneza dawa kutafuta faida. Waandishi kadhaa wameonyesha madai haya kuwa ya uwongo, ingawa baadhi ya waandishi hawa hata hivyo wanashikilia kuwa ukosoaji mwingine wa tasnia ya dawa ni halali.
 
Mnaangamia kwa kukosa maarifa, elimu ya chuo kikuu haitoshi, kama ingetosha kutibu jino hata usingehitaji tabibu
Lifestyle ndo somo mlokosa mnakaririsha kusukutua na dawa zenye mint ndo mnaona fresh breath pua yu
Elimu ya Darasani inakubali kuwa kuna magonjwa haiwezi kutibu. Ile ya matapeli hao matapeli inadai inatibu kila ugonjwa.
 
Unakuta mtu anamuita Mnyakyusa nabii tangu lini Mnyakyusa akawa nabii? Alafu utaskia aposto huku kuna muujiza,,, nini kimetokea ,, eti katapika ng'ombe mzima..

Mafala wataliwa sana
Mnyaki baada ya kuona maisha magumu na ana ABC za kunena kwa lugha, anaamua kuwa Nabii. Na watu kwa kutotaka kuwajibikia shida zao, wanamtwisha nabii na kumlipa.
 
Inaitwa placebo effect hata huku mahospitalini tunatumia kutibu watu kwa vidonge vya sukari! The trick is to convince your brain to treat itself kwa kuamini kupitia matibabu fulani ambayo kiuhalisia ni majani au mizizi tu au vidonge vyenye sukari japo zipo herbs zinazofanya kazi kweli.

Atleast wanakua wamekusaidia kuamni kwamba kupitia kitu fulani au Mungu fulani umepona japo kuwa placebos haziponyi zinatoa unafuu tu.
Yap, inasaidia saikolojia tu.
 
anawatukana Watibabu wa Tiba mbadala lakini kwa siri anawafuata ili wapate kumtibia mwongo huyu na mnafiki.
Nitakuwa najikosea heshima na nakosea heshima akili yangu nikienda kufuata tiba kwa matapeli. Mara wanapima na kutibu kwa kutumia kompyuta?
 
Alovera ni dawa nzuri sana ya kuua vimelea. Inasaidia sana kwenye magonjwa ya ngozi, michubuko au vidonda vya nje. Matapeli wameikuza ikawa kama dawa ya maajabu, ikitibu kila kitu.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Unakuta mtu anamuita Mnyakyusa nabii tangu lini Mnyakyusa akawa nabii? Alafu utaskia aposto huku kuna muujiza,,, nini kimetokea ,, eti katapika ng'ombe mzima..

Mafala wataliwa sana
 
Ndio maana wanywa nyagi hawana shidae sababu wanatumia vichungu kila siku

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
Pombe kali zinafanya hasa kazi tumboni. Zinatibu minyoo, amiba na wadudu karibu wote wa kuleta mambo ya kuharisha na kuhara. Lakini kwa kiasi kikubwa zinaleta shida kwenye afya.
 
Inasaidia sana kwenye saikolojia lakini fahamu watu wote wa tiba mbadala ni matapeli! Babu wa Loliondo, Sheikh Yahaya, Dr. Mwaka, Dr Ndodi, Sanitarium kliniki zote, wamasai, matabibu wote wanaojitangaza redioni, watu wa maombezi n.k n.k.

Tiba mbadala wote ni matapeli, dawa zao hazifanyi kazi. Katibiwe au peleka mgonjwa wako ukiwa na hilo akilini.
Shehe yahya alikuwa anafanya Tiba mbadala? Una matatizo wewe Dr ndodi amewahi kukutapeli Nini? Mwaka je?
 
Baadhi ya tiba mbadala zinatibu isipokuwa hawa matapeli kama wanaaojiita dr mwaka ndiyo matapeli.huwa wanawapa kila aina ya midawa zao kwa kubahatisha.wanaweza kuwa wanakubadilishia tu dawa hata zaidi ya miaka miwili lengo ni kubahatisha kutibu ugonjwa.kibaya zaidi wanawake wamemwamini sana mara sjui uzazi lakini ukweli ni kuwa yule jamaa ni tapeli
 
Inasaidia sana kwenye saikolojia lakini fahamu watu wote wa tiba mbadala ni matapeli! Babu wa Loliondo, Sheikh Yahaya, Dr. Mwaka, Dr Ndodi, Sanitarium kliniki zote, wamasai, matabibu wote wanaojitangaza redioni, watu wa maombezi n.k n.k.

Tiba mbadala wote ni matapeli, dawa zao hazifanyi kazi. Katibiwe au peleka mgonjwa wako ukiwa na hilo akilini.
Watu wanaoombea nao wanafanya Tiba mbadala? Umekutana na matapeli unahitimisha kuwa wote NI matapeli
 
Baadhi ya tiba mbadala zinatibu isipokuwa hawa matapeli kama wanaaojiita dr mwaka ndiyo matapeli.huwa wanawapa kila aina ya midawa zao kwa kubahatisha.wanaweza kuwa wanakubadilishia tu dawa hata zaidi ya miaka miwili lengo ni kubahatisha kutibu ugonjwa.kibaya zaidi wanawake wamemwamini sana mara sjui uzazi lakini ukweli ni kuwa yule jamaa ni tapeli
Zipo za magonjwa simple kama ya tumbo, mapunye na vidonda. Na hayo hayana pesa. Wanakomalia figo, kisukari, ini, uzazi nk. Ndiko kuna pesa na Utapeli. Kama tu Kabudi na Magufuli walivyotapeliwa na Rais wa Madagascar. Au matapeli walivyocheza na fursa ya Covid.
 
Ndiyo wanavyotapeli kwa kauli hizo hizo.
Mi sio daktari wa mitishamba nimejiongeza tu maarifa kwa hiyo huwa najitibu mwenyewe in case, but all in all naadjust lifestyle yangu kwa kuepuka vyakula ambavyo kwa sasa waeza ona vitamu au fahari ila vinasababishia magonjwa mbeleni ndo maana sijawahi kukutana na tapeli ila hospitali mwiko
 
Back
Top Bottom