Ni kweli mababu zetu walitibiwa kupitia miti shamba na walipona kwa sababu zamani kulikuwa hakuna ujanja ujanja km ilivyo sasa. Ukosefu mkubwa wa ajira,ugumu wa maisha,watu kukosa uaminifu vyote hivyo vimepelekea kila mtu kuwa tapeli.Si umesikia juzi tu mamlaka ya dawa imekamata watu wanaojiita waganga wakiuza vumbi la Kongo huku wamechanganya na VIAGRA? Kwanza sifa ya mganga wa kweli sharti lake ni kutojitangaza ila ubora wa dawa zake ndo humtangaza. Ukikuta mganga anajitangaza hapo jua ni upigaji.