Katibiwe ila fahamu kuwa tiba mbadala wote ni matapeli

Ni kweli mababu zetu walitibiwa kupitia miti shamba na walipona kwa sababu zamani kulikuwa hakuna ujanja ujanja km ilivyo sasa. Ukosefu mkubwa wa ajira,ugumu wa maisha,watu kukosa uaminifu vyote hivyo vimepelekea kila mtu kuwa tapeli.Si umesikia juzi tu mamlaka ya dawa imekamata watu wanaojiita waganga wakiuza vumbi la Kongo huku wamechanganya na VIAGRA? Kwanza sifa ya mganga wa kweli sharti lake ni kutojitangaza ila ubora wa dawa zake ndo humtangaza. Ukikuta mganga anajitangaza hapo jua ni upigaji.
 
Zamani ni magonjwa machache tu ambayo mababu waliweza kujitibu. Mengi yaliwau kwa wingi sana. Ikitokea mlipuko ulikuwa unatambaa na maelfu ya watu. Bahati nzuri ni kuwa magonjwa yatokanayo na mtindo wa maisha kama kisukari, pressure hayakuwepo au yalikuwa kwa uchache sana. Tusifanganyike kuwa mababu walijiweza kwa tiba. Magonjwa yaliwatesa sana na hawakujua yalikotoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…