Zanzibar 2020 Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru ashangaa watu 12 kujitokeza kutaka urais Zanzibar, adai wengine wanatumika na mabeberu kutaka kuvuruga nchi yetu

CCM huwa wanatuaminisha kwa Ni Chama chenye Democracy pana ,.
Sasa kwa mtazamo wake Karibu Mkuu CCM hawataki demokrasia ?
 
Niliwaambia humu mkafikiri utani, baada ya Jpm kuchukua fomu Bashiru alifunga ofisi na kwenda Dar ili wagombea wengine wakose fomu vp mmeamini.
 
Alijuaje idadi kuwa wako 12 ?
Kwa nafasi yake ya ukatibu mkuu, yeye ni mtendaji mkuu wa chama, kwa hiyo alikuwa anajua kila kilichokua kinaendelea ndani ya chama hasa kwa hao waliokuwa wanajipitisha pitisha kabla ya wakati kwa mujibu wa CCM kuutaka urais wa Zanzibar. Lakini, for your information, mpaka leo hii jumatatu, waliokwishachukua form za kuomba uteuzi wa kugombea urais wa Zanzibar kupitia CCM wameshafika 14, imezidi hiyo idadi aliyokuwa ameisema Dr. Bashiru.
 
Ingekuwa ni hivyo hata huyo aliepo basi asingekuwepo maana alipatikana kwenye wengi
 
Wanasahau kuwa malipo ni hapa hapa duniani
 
Bashiru anawadhalilisha wahaya wenzake maana wenzetu wanasifiwa kwa kuwa watu wenye akili sana
Hivi huku bara 2015 watia nia ndani ya CCM kugombea urais walivyofika zaidi ya 40 walikua wanatumiwa na wakina nani? Mabeberu au Majike?
 
Kwani mtu wao wa zenji sinasikia ni yule mzee wa maji?
Wanampigania mtu wao hapo kwa kuwaita wengine wanatumiwa na mabeberu. Bara wanapandikizi lao na Zanzibar wana wana mtu wao wanayemtaka hao wengine ni chambo.

Huyo mtu wao wa Zanzibar ndiyo anaitwa anatumika na Mabeberu,hahahahaha
 
Wacha kudanganya watu wewe na jina lako la ajabu ajabu
 
Wacha kudanganya watu wewe na jina lako la ajabu ajabu
Jina ni langu, kama umelipenda kamrithishe mwanao. Nilichodanganya ni kipi? Huo ukweli unaoujua wewe ni upi?
Angalia hiyo video hapo chini ya Dr. Bashiru akiwa ziarani Zanzibar mwaka jana, na angalia ilikuwa uploaded lini kwenye youtube.

 

Yeye alitakaie!?

Ni ngumu kuamini kama ni PhD holder.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…