Zanzibar 2020 Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru ashangaa watu 12 kujitokeza kutaka urais Zanzibar, adai wengine wanatumika na mabeberu kutaka kuvuruga nchi yetu

Zanzibar 2020 Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru ashangaa watu 12 kujitokeza kutaka urais Zanzibar, adai wengine wanatumika na mabeberu kutaka kuvuruga nchi yetu

Katibu mkuu wa CCM ashangaa watu ama wanachama 12 kujitokeza ndani ya CCM kuutaka urais.

Anashangaa nafasi ni 1 ya urais watu 12 wanatafta nini? Awatuhumu wengine kua wanatumwa na mabeberu kuvuruga chama na kuleta mvurugano nchini.

Anasema hao wanachama wa CCM 12 wanaoutaka urais wanataka kuvunja umoja wa Chama cha Mapinduzi.

Msikilize hapa.

CCM huwa wanatuaminisha kwa Ni Chama chenye Democracy pana ,.
Sasa kwa mtazamo wake Karibu Mkuu CCM hawataki demokrasia ?
 
Niliwaambia humu mkafikiri utani, baada ya Jpm kuchukua fomu Bashiru alifunga ofisi na kwenda Dar ili wagombea wengine wakose fomu vp mmeamini.
 
Alijuaje idadi kuwa wako 12 ?
Kwa nafasi yake ya ukatibu mkuu, yeye ni mtendaji mkuu wa chama, kwa hiyo alikuwa anajua kila kilichokua kinaendelea ndani ya chama hasa kwa hao waliokuwa wanajipitisha pitisha kabla ya wakati kwa mujibu wa CCM kuutaka urais wa Zanzibar. Lakini, for your information, mpaka leo hii jumatatu, waliokwishachukua form za kuomba uteuzi wa kugombea urais wa Zanzibar kupitia CCM wameshafika 14, imezidi hiyo idadi aliyokuwa ameisema Dr. Bashiru.
 
Katibu mkuu wa CCM ashangaa watu ama wanachama 12 kujitokeza ndani ya CCM kuutaka urais.

Anashangaa nafasi ni 1 ya urais watu 12 wanatafta nini? Awatuhumu wengine kua wanatumwa na mabeberu kuvuruga chama na kuleta mvurugano nchini.

Anasema hao wanachama wa CCM 12 wanaoutaka urais wanataka kuvunja umoja wa Chama cha Mapinduzi.

Msikilize hapa.

Ingekuwa ni hivyo hata huyo aliepo basi asingekuwepo maana alipatikana kwenye wengi
 
Wanasahau kuwa malipo ni hapa hapa duniani
Huyu dokta anatetemeka nini, kwani haijui demokrasia?

Kumbe pamoja na ujuaji wao wanaogopa makundi, lazima yawapasue tu, na kwenye ubunge ndio itakuwa balaa zaidi, si walifurahia kununua wanadamu wenzao kama mbuzi huku wakichekelea, sasa wajiandae kwa malipo.
 
Bashiru anawadhalilisha wahaya wenzake maana wenzetu wanasifiwa kwa kuwa watu wenye akili sana
Hivi huku bara 2015 watia nia ndani ya CCM kugombea urais walivyofika zaidi ya 40 walikua wanatumiwa na wakina nani? Mabeberu au Majike?
 
Kwani mtu wao wa zenji sinasikia ni yule mzee wa maji?
Wanampigania mtu wao hapo kwa kuwaita wengine wanatumiwa na mabeberu. Bara wanapandikizi lao na Zanzibar wana wana mtu wao wanayemtaka hao wengine ni chambo.

Huyo mtu wao wa Zanzibar ndiyo anaitwa anatumika na Mabeberu,hahahahaha
 
Wacha kudanganya watu wewe na jina lako la ajabu ajabu
Hiyo clip ya Dr. Bashiru ni ya zamani, aliitoa wakati amefanya ziara Zanzibar na ilikuwa kabla hata CCM hawajafungua dirisha la kuchukua forms kwa wanachama wake wanaotaka kuteuliwa kugombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho. Alikuwa anawakemea kuanza kujipitisha pitisha kabla ya wakati, kwani kwa kufanya hivyo walikuwa wanakivuruga.
 
Wacha kudanganya watu wewe na jina lako la ajabu ajabu
Jina ni langu, kama umelipenda kamrithishe mwanao. Nilichodanganya ni kipi? Huo ukweli unaoujua wewe ni upi?
Angalia hiyo video hapo chini ya Dr. Bashiru akiwa ziarani Zanzibar mwaka jana, na angalia ilikuwa uploaded lini kwenye youtube.

Katibu mkuu wa CCM ashangaa watu ama wanachama 12 kujitokeza ndani ya CCM kuutaka urais.

Anashangaa nafasi ni 1 ya urais watu 12 wanatafta nini? Awatuhumu wengine kua wanatumwa na mabeberu kuvuruga chama na kuleta mvurugano nchini.

Anasema hao wanachama wa CCM 12 wanaoutaka urais wanataka kuvunja umoja wa Chama cha Mapinduzi.

Msikilize hapa.

Yeye alitakaie!?

Ni ngumu kuamini kama ni PhD holder.
 
Back
Top Bottom