Unalazimisha chuki mahala haipo, na mnazungumza pembeni bila kuzungumza na muhusika, hayo ni mawazo yako binafsi tena ya kutengeneza bila msingi, au kushawishiwa uandike, pole sana.
Hatuwezi kuongea hapa kwa wakati huu sisi tuliopata kuongea nae kwa undani bila ruksa yake Dr. Bashiru mwenyewe, lakini unacholazimisha kieleweke kwa Jamhuri ya JF hana kabisa kichwani kwake. Labda ungesema Ana nia ya kugombea ujumbe wa halmashauri kuu ya CCM tunge kuelewa.
Mama Samia usilazimishiwe chuki na watu kwa kitu ambacho hakipo. Kwanza kwa silka yake Dr. Bashiru ni mtiifu, mwaminifu, na anategemewa ( you can trust and depend on him).
Amejifunza mengi na yuko tayari kuendelea kujifunza. Na anasema kwenye siasa unabaki mwanafunzi mpaka siku unaondoka kwenye uwanja wa siasa.
Tuache kutoa maoni ya kichwani mwako, mjitahidi kuongea na wahusika kabla ya kuandika, mnawaumiza watu sana, nadhani katika hali kama hizi ndio kuzaliwa roho za visasi.
Tusitumiwe haitusaidi.