Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aandika barua ya kujiuzulu

Mimi ni Wamrengo wa kushoto kiasili. Huyu chongolo ni mtu mwema Sana ni mtu haswa na naamini hapendi makandokando
Hakika mkuu, Chongolo ni mtu poa sana. Sema tu amekosa ile kariba ya ubabe babe na ukorofi ndiyo maana watu wanaona kama amepwaya. By the way typing error 2024 na 2025
 
Chongolo hakufaa kuwa Katibu Mkuu; kazi inayotaka mtu analytical; yeye angepewea nafasi kama vile Oganaizesheni, Nadhani Katibu mkuu mzuri kwa CCM alikuwa ni Dr Bashiru Ally, na kipindi fulani cha nyuma kulikuwa na Wilson Mkama, Philip Mangula, pamoja na Horace Kolimba. Makatibu wakuu wazuri wa CCM walikuwa hawadumu sana kwenye nafasi hizo ispokuwa Philip Mangula.

Katibu mtendaji mkuu wa Kwanza Pius Msekwea yeye alikuwa ni intellectual sana, alama zote za CCM zilizopo leo: katiba, nembo, bendera na hata wimbo wa CCM ni matunda ya uongozi wake.
 
Duh! Yaani katika makada wooteee, imegeuka kuwa Albert Chalamila. Ngoja tuzidi kunywa mtori huenda nyama tutazikuta chini!
 
Baada tu ya DAB kuteuliwa ile video ikarushwa mitandaoni, binafsi nilipoiona nilihisi hili lingetokea. Na siyo kwa huyu Chogolo tu, ni wengi ndani ya CCM hawakupendezwa na uamuzi wa Mwenyekiti wao kumteua DAB kuwa Mwenezi wa chama, na wengi waliongea chini chini kupinga uteuzi huo.

Lakini nadhani na Mwenyekiti ana lipa fadhila kwa DAB kiaina. Kuna video ili pita pia ikionyesha DAB alivyo mpigia chepuo kuwa Mgombea mwenza wa hayati Magufuli, toka kwenye U-spika wa bunge la katiba hadi kuwa mgombea mwenza na hatimaye leo Mwenyekiti wa CCM taifa.

Baada ya huyu hatujui nani atafuata, ila ccm wengi hawakumfurahia DAB kurudishwa hata kidogo.
 
Nimeamini jf ni chanzo Cha habari nyingi Sana,tetesi ya makonda kulamba uenezi nilisikia hapa hapa ,nikachukulia POA Kama vile umbea umbeya,mwisho ikawa,pia Raisi magufuli kupitishwa kuwa mgombea uraisi nikianza kusikia mapema kupitia hapa hapa,,makamba kuondokewa nishati nikianza mapema kusikia Kama tetesi vile ,hatimaye ikawa,na hili la chongolo laweza kuwa
 
CCM yenye amsha amsha ni ile ya Kina bashiru Ally na polepole kuliko hii,ya chongolo imepoa mno Hadi inaboa
 
Ya PM tu ndio haijawahi timia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…