Dah ! Mgombea wa CCM Mpya John Pombe Joseph Magufuli sijawahi kumuona akifanyiwa mahojiano ya aina yoyote na chombo cha habari wala kushiriki katika mdahalo kushindanisha mipango na maono yake.
Mambo yakiharibika wanaCCMpya wanaelekeza lawama siyo kwa Mgombea wao bali kwa wataalamu na wasaidizi kama Bashiru Ally kushauri kununua wanasiasa wa upinzani, Dr. Philip Mpango sera za fedha & Uchumi, Humphrey Polepole dhana potovu kuwa upinzani utakuwa umekufa 2020, Prof. Palamagamba Kabudi kuhusu korosho n.k kwa kumshauri mgombea wao vibaya.
Ingekuwa kipindi hiki hakijarekodiwa basi tungempelekea mtangazaji Fardhia Middle kuhoji vipi ACT-Wazalendo, CHADEMA, CUF, CHAUMMA wote waliwapeleka wagombea wa urais ktk kipindi pendwa cha Dakika 45 ITV Tanzania kuelezea na kutetea toka ndani ya mioyo yao sera, mipango na maono yao lakini CCM Mpya wanamficha mgombea wao asije studio kuhojiwa ?