Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani aandika barua ya Kujiuzulu. Lugola na Andengenye wakalia kuti kavu, Rais Magufuli asema hawafai

Mzee alikupatia kazi ulipaswa uimalize haraka, ajabu mpaka Mwaka wa 2019 unamalizika KAZI IMEBAKI KIPORO mpaka Leo.

Na mbaya zaidi mmejigeuza kuwa miungu watu na marafiki wakubwa wa Mkuu wa KAYA,Hata Bila aibu mnasaini kupokea MIFEDHA mingi Bila kufuata Utaratibu.
ULICHOKIPANDA NDICHO UTAKACHO KIVUNA.
KARIBU SANA MTAANI.
 
Kwa kweli sasa utendaji wa uadilifu ndiyo nguzo pekee tunajivunia awamu hii. Shida ni pale tunapokutana na vichwa vigumu visivyotaka kuelewa kuwa tupo kwenye awamu ya kujenga taifa lenye nidhamu na maadili wao bado wanaendeleza vijidili vya chini kwa chini.
 
Hahaha Lugora kasepa na ilani zake za chama mfukoni,na hazikumsaidia asiliwe kichwa.
 
Yaani tunahangaishwa na nida hili jamaa liko busy na mikataba feki, lakini sitangu mwanzo tulisema Hilo jamaa la hovyo?
 
Binafsi nmepokea kwa huzuni Sana taarifa ya kujihudhuru uwaziri wa mambo ya ndani.
Alitatua mengi Sana kwa upande wa mwanachi wa kawaida.mfano
~Suala la kupewa dhamana polisi bila kutoa pesa
~masuala ya kufukuzana barabarani kati ya bodaboda na mapolisi iliisha
~Nidhamu ya polisi iliimarika sana
 
Sherehe watafanya japo hakuwanyanyasa. Huyu bwana aliwanyoosha. Dhamana zikawa 24x7 na matochi barabarani yakawa japo na hekima kidogo.

Kuondoka Lugora ni pigo kwa jitihada dhidi ya dhuluma za polisi.
Ila hizi Ashok za polisi Ni aibu,
 
Tunaomba kupata undani wa huo mradi ambao mkataba wake ama MoU vilisainiwa kwa Staili ya 'Karamagi'!
 
Jana kuna taarifa ambayo haipendezi kuisikiliza lakini yaweza kuwa kweli ya kwamba Tanzania inaweza kuwa moja ya nchi ambazo raia wake watazuiwa kuingia Marekani.
Naamini hili linaweza kuwa jambo kubwa kama litatimia.Kinachonisikitisha kwa sasa watu wamehamia kwenye issue ya Kangi na kuacha jambo la wengi.

Ni vyema tuendelee kutafakali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…