Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani aandika barua ya Kujiuzulu. Lugola na Andengenye wakalia kuti kavu, Rais Magufuli asema hawafai

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani aandika barua ya Kujiuzulu. Lugola na Andengenye wakalia kuti kavu, Rais Magufuli asema hawafai

IMG_20200123_121805.jpg
IMG_20200123_121735.jpg
IMG_20200123_121714.jpg

Sio mbaya , kijiwe chake ametuachia huku Mwanza kinatubarki Sana .., mweshimiwa hajatoka kapa
 
Ile ilani hajanyang'anywa bali baada ya kutumbuliwa kaisahau pale alipo kuwa amekaa, na kwenda kupanda lile shangingi kakuta mp amesimama mlangoni na kumwambia hausiki na lile gari.

Muda huu tupo naye hapa anatafuta tax kuelekea kwao
Mkuu VAPS umekurupushwa kabla hujamaliza kuandika?
Kwamba amenyang'anywa ile ilani ya chama anayotembea nayo mkononi na kwenye majukwaa au?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ile lugha ya raisi wa wa Tanzania aliyokuwa anaitumia wa waziri wa mambo ya ndani na kamishina wa jeshi la magereza Mr. Andengenye bila wasiwasi wowote wale jamaa weishakanyaga nyaya za tanesco.
Kamishna wa Magereza sio Bwana Andengenye, ,Huyu yupo Fire bregade(zimamoto)
 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani Aandika barua ya Kujiuzulu.

Rais Magufuli akiwa anahutubia wakati wa ufunguzi wa nyumba za Askari Magereza, amesema kwamba..

Nampongeza sana Kamishna Jenerali, Kingu ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kuwajibika kwamba ametambua. Na nimamuheshimu na nitaendela kumuheshimu

Lugola nampenda sana ni mwanafunzi wangu nilimfundisha Sekondari, hapa umenisifia kwelikweli nakushukuru lakini kwenye hili hapana. Nilijua nisingemkuta hapa, Kamishna Andengenye ni mchapakazi nilitegemea hapa asiwepo hatuwezi tukaendesha nchi kwa misingi ya ajabu.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani nampenda sana lakini kwenye hili la kwenda nje ya nchi unasaini fedha ambazo hazijapitishwa hata na Bunge hapana.
Akafanye sasa kazi anayoiweza vizuri, KUKATA UNO!
 
Pamoja na kumsifia Rais,leo Lugola katumbuliwa.
Rais akiwa anafungua makazi ya wanajeshi wa magereza.Katibu mkuu ajiuzulu ila Lugola kaambiwa SASA BASI.
Lugola alikuwa mpole na mdogo kama piriton.
Jamaa (Lugola) alipambana na makamanda wa polisi kweli kweli huku akiwatumbua au kuwahamisha vituo hatimaye leo msumeno umemgeukia.
 
Bashe akikubali hapo sawa.. Ila sijui kama atakubali aiseee.. Angekubali, yaani mambo yangenyooka sana, ila muache Bashe anyooshe wizara ya kilimo kwanza, asiondolewe jamani, wizara ya kilimo ndio roho ya maisha ya wananchi..

Au Mh. Rais afunge macho anipe mm, naapa itanyooka kama ruler wizara nzima.💪🤔
 
Lugola asiache kuvaa mashati yake yenye bendera ya taifa bila kusahau kubeba katiba ya chama chake kila aendapo huenda mtukufu akamteua kwenye chansi nyingine!!
 
Kweli aliekuweka ndo anaeweza kukutoa nawaza kama Mimi ndo ningekuwa Kangi mbele ya kutoa sifa zote na unatumbuliwa sijui unarudi na pozi gani mtaani.
Hapo ndo utapoona mwanasiasa anakua mwanafalsafa
 
Rais John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye hawafai kuwa katika nyadhifa hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom