TANZIA Katibu Tawala Arusha, Bw. Richard Kwitega afariki Dunia

TANZIA Katibu Tawala Arusha, Bw. Richard Kwitega afariki Dunia

Apumzike kwa Amani. Ila madereva wa serikali na hizo overtake zenu hapana. Sasa ukichanganya na overtake za mabasi inakuwa si hali. Hata kama mnaendesha magari ya serikali (au hata mabasi) jueni ajali haichagui uimara wa gari au status ya gari-nashangaa hata hamuofii maisha yenu wenyewe mnovyo overtake! Chonde chonde fuateni sheria kama sisi raia na muache mchezo wa kuwasha mataa yenu na kupita kwenye 50 kph na hizo 120+kph. Ajali inaweza kumpata mtu yeyote ila kuna anayejiweka katika nafasi hatarishi zaidi kupata ajali kwa kuvunja sheria za barabarani kwa ubabe tu. Sasa baba wa watu kapoteza maisha hivi hivi, inauma. Poleni familia ndugu jamaa na marafiki.
 
Salaam Wakuu,

Habari Mbaya ni kwamba Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw.Richard Kwitega amefariki Dunia kutokana na ajali.
View attachment 1693548
Richati kwitega kafariki alasiri ya leo kwa ajali ya gari katika kituo cha afya cha Magugu. Richard alikuwa anaenda Dodoma Kikazi, alipofika maeneo ya Mdori Manyara gari lake iligongana na Basi la Makala uso kwa uso, Basi lilikuwa linalotoka babati.

Baada ya ajali akakimbizwa kituo cha afya cha Magugu ili baadaye apelekwe Babati kwa matibabu zaidi.

Ilipofika saa tisa na dakika 50 akafariki Dunia. Sasa mipango inafanyika ya kuurudisha mwili Arusha.

Apumzike kwa amani

View attachment 1693569
View attachment 1693583View attachment 1693584View attachment 1693585
Alikuwa Kiongozi Mwerevu, Pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki. Roho wa MUNGU awapunguzie machungu na kuwapa ubaridi wa nafsi. Marehemu apate pumziko la Amani.
 
Poleni sana Familia. Kifo chake kimenigusa sana kwa sababu nimefanya naye kazi Mkoa wa Kagera akiwa Afisa Utumishi wa Mkoa wa Kagera na yeye ndiye aliye Mratibu wa Mkoa kwa masuala yote ya Mwenge wa Uhuru.
 
apumzike anapostahili Ila hawa watu wenye magari ya serikali wanayaendesha vibaya Sana maybe kwa sababu hayasimamishwi na traffic Leo jioni nimekutana na lingine linapita service road maeneo ya Boko kidogo limgonge mwanafunzi na Wala dereva hakujali kusimama aone Kuna madhara amesababisha au laa sio sawa kabisa.
 
Madereva wengi wa Serikali hawafuati sheria. Mmoja lazima alikuwa ana overtake hapo recklessly...
 
Salaam Wakuu,

Habari Mbaya ni kwamba Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bw.Richard Kwitega amefariki Dunia kutokana na ajali.
View attachment 1693548
Richati kwitega kafariki alasiri ya leo kwa ajali ya gari katika kituo cha afya cha Magugu. Richard alikuwa anaenda Dodoma Kikazi, alipofika maeneo ya Mdori Manyara gari lake iligongana na Basi la Makala uso kwa uso, Basi lilikuwa linalotoka babati.

Baada ya ajali akakimbizwa kituo cha afya cha Magugu ili baadaye apelekwe Babati kwa matibabu zaidi.

Ilipofika saa tisa na dakika 50 akafariki Dunia. Sasa mipango inafanyika ya kuurudisha mwili Arusha.

Apumzike kwa amani

View attachment 1693569
View attachment 1693583View attachment 1693584View attachment 1693585
Mwendo wa madereva wa serikali ni tatizo. Hawafuati sheria za barabarani kabisa. Tuna waona huku barabarani mwendo wao.
Kama wataendelea hivi tutegemee ajaili za viongozi mara kwa mara
 
Back
Top Bottom