TANZIA Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Tixon Nzunda afariki kwa ajali ya gari

Taarifa za awali kutoka mkoani Kilimanjaro zinaeleza kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Tixon Nzunda pamoja na dereva wake wamefariki dunia kwa ajali iliyotokea eneo la Mijohororoni mkoani humo.

Bado mamlaka husika hazijatoa taarifa juu ya ajali hiyo.

View attachment 3020136View attachment 3020137
Picha kutoka eneo ilipotokea ajali

======

Dkt. Tixon Tuyangine Nzunda alikuwa katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, nafasi aliyoteuliwa na Rais Samia Suluhu na kuapishwa 19 Machi, 2023.

Nzunda alizaliwa January 29, 1968 na ameacha mke na watoto wanne. Aliajiriwa na Serikali mwaka 1992 kama afisa msaidizi wa elimu daraja la tatu na tangu hapo ameshika nafasi kadhaa ikiwemo katibu mkuu msaidizi utumishi, katibu tawala mkoa wa Rukwa na naibu katibu mkuu Serikali za mitaa.

Picha kutoka Maktaba.

So sad really Mungu awarehemu.
 
Huko serikalini ajali nyingi sana.

Ni kulogana au uzembe wa madereva??

Pole kwa wafiwa.
Hakuna cha kurogana wala nini, nyingi ni uzembe wa madereva na kupenda mwendo wa ngiri kisingizio Kuna kazi maalumu wanawahi, lakini pia serikali Haina speed limit Kwa gari maana mashirika ya kimataifa na taasisi mbalimbali za mabeberu aka wafadhiri huwa Wana speed limit lakini kikubwa ikifika saa 12 jioni dereva park tafuta hotel lala mpaka asubuhi na gari ikitembea zaidi ya huo muda basi staff aliepo kwenye hiyo gari lazima apaki pembeni aandike email ya kwanini asafiri zaidi ya muda huo (akipewa go ahead anaendelea na safari)

Shida serikalini "boss" ndo msemaji wa safari na anapanga muda kuondoka na kufika na hata kama dereva amechoka atajiju though sio wote siku hizi Kuna baadhi wanajitajidi kuishi kirafiki na madereva na kumfanya dereva kuwa free kumshauri boss wake kuhusu mwenendo wa safari Yao na kupanga muda vizuri

Hoja ya msingi, wapumzike Kwa amani ndugu zetu Watanzania
 
Taarifa inasema RAS na dereva wake wote wamefariki kwnye ajali lkn taarifa zote za ziada zinatoa maelezo kumhusu RAS peke yake hata RIP za wasomaji zinamlenga RAS pekee, najiuliza tu huyu dereva na familia yake hawaihitaji hizo RIP na faraja kwa kuondokewa na mpendwa wao au sio kipaumbele!?
Anyway RIP kwa wote waliopoteza maisha na Mungu awe mfariji kwa wafiwa wote.
 
Wanaangalia mteule tu wa Rais
 
Taarifa za awali kutoka mkoani Kilimanjaro zinaeleza kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Tixon Nzunda pamoja na dereva wake wamefariki dunia kwa ajali iliyotokea eneo la Mijohororoni mkoani humo.

Bado mamlaka husika hazijatoa taarifa juu ya ajali hiyo.

View attachment 3020136View attachment 3020137
Picha kutoka eneo ilipotokea ajali

======

Dkt. Tixon Tuyangine Nzunda alikuwa katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, nafasi aliyoteuliwa na Rais Samia Suluhu na kuapishwa 19 Machi, 2023.

Nzunda alizaliwa January 29, 1968 na ameacha mke na watoto wanne. Aliajiriwa na Serikali mwaka 1992 kama afisa msaidizi wa elimu daraja la tatu na tangu hapo ameshika nafasi kadhaa ikiwemo katibu mkuu msaidizi utumishi, katibu tawala mkoa wa Rukwa na naibu katibu mkuu Serikali za mitaa.

Picha kutoka Maktaba.

Rip RAS....

Poleni Sana Wafiwa....Mungu awatie nguvu
 
Back
Top Bottom