TANZIA Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Tixon Nzunda afariki kwa ajali ya gari

TANZIA Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Tixon Nzunda afariki kwa ajali ya gari

Taarifa za awali kutoka mkoani Kilimanjaro zinaeleza kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Tixon Nzunda pamoja na dereva wake wamefariki dunia kwa ajali iliyotokea eneo la Mjohoroni mkoani humo.

Bado mamlaka husika hazijatoa taarifa juu ya ajali hiyo.

View attachment 3020136View attachment 3020137
Picha kutoka eneo ilipotokea ajali

======

Dkt. Tixon Tuyangine Nzunda alikuwa katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro, nafasi aliyoteuliwa na Rais Samia Suluhu na kuapishwa 19 Machi, 2023.

Nzunda alizaliwa January 29, 1968 na ameacha mke na watoto wanne. Aliajiriwa na Serikali mwaka 1992 kama afisa msaidizi wa elimu daraja la tatu na tangu hapo ameshika nafasi kadhaa ikiwemo katibu mkuu msaidizi utumishi, katibu tawala mkoa wa Rukwa na naibu katibu mkuu Serikali za mitaa.

Picha kutoka Maktaba.

Tuendelee kuwa na Mungu kwa hili.Kumbuka marehemu haombewi bali tunaombea waliobaki.
 
Mbona Tangazo limewahi kutolewa 😏
 

Attachments

  • IMG-20240618-WA0040.jpg
    IMG-20240618-WA0040.jpg
    119.3 KB · Views: 7
  • IMG-20240618-WA0041.jpg
    IMG-20240618-WA0041.jpg
    110.2 KB · Views: 5
Mwendokasi wa hovyo, wangeondoka mapema na wakaenda mwendo wa kawaida wasingefika? halafu hili swala la kwenda kumpokea Makamu magari zaidi ya 50 ili iwe ni nini? gharama kubwa kwa walipa kodi
 
Mwendokasi wa hovyo, wangeondoka mapema na wakaenda mwendo wa kawaida wasingefika? halafu hili swala la kwenda kumpokea Makamu magari zaidi ya 50 ili iwe ni nini? gharama kubwa kwa walipa kodi
 
Madereva wa magari ya serikali😳
Wakati mwingine utakuta madereva hawana makosa, pengine walikuwa wamechelewa kwenye shughuli na maboss wengine wana kawaida ya kuwakoromea madereva na kuwafokea kabisa "kanyaga gari wewe si unaona tunachelewa"...... dereva afanyeje si lazima atii amri ya boss ananyoosha mguu matokeo yake si yanakuwa hayo.
 
Back
Top Bottom