Kutoka Ikulu Katibu wa Rais hadi Katibu tawala msaidizi Utawala na rasilimali watu nadhani hiyo ni kupigwa teke kubwa haswaa.Huyu alikuwa akisimama kando wakati mawaziri,makatibu wakuu,wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wanapoapishwa.
Hakika ndugu yetu alikuwa mzoefu wa corridor za Ikulu leo unapelekwa mkoa wa Mara hii inaweza kuwa sababu kuu ya kifo chake.
RIP Katibu Tawala Msaidizi.
Ndugu yangu, Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu, ni Cheo kikubwa. Huyu ndiyo namba mbili baada ya Katibu Tawala wa Mkoa. Anakamata mafungu yote ya Mkoa. Yeye ndo msimamizi wa Watumishi wote katika mkoa. Na pia mambo yote ya Protokali. Ikulu alikuwa hana fungu, anasubiri kugawiwa. Ila Mkoani fedha yote inafikia kwake, yeye anagawa kwa idara mbalimbali.
Ni mshauri mkuu wa RAS na pia Mkuu wa Mkoa. Akitoka hapo ni kupandishwa kuwa RAS au Katibu Mkuu. Kwake yeye alipandishwa. Na isitoshe Ziara ya Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu zinapofanyika mikoani, yeye akiwa kama katibu Tawala Msaidizi ndiye anaeratibu mambo yote na kuhakikisha Protokali zimeenda uzuri na kama Ikulu watu wamepata huduma stahiki. Pia kuhakikisha Ikulu ya Mkoani ipo katika hali nzuri na salama kwa kushirikiana na Ofisi ya RSO.
Pia miaka ya Rais Kikwete alishawahi mteua aliekuwa Msaidizi au Katibu wa Waziri Mkuu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa Wa Mara. hata huyu alishinda viunga vya Ikulu, si kwamba alishushwa hapana. Katika ngazi ya kazi alipandishwa. Si kila mtu afanye Ikulu anacheo cha juu la hasha.
Unanikumbusha wakati fulani nipo kazini mahala fulani. Wakaja wanachi kadhaa na majivuno na sauti kubwa kwamba wameagizwa na mtu fulani kutoka ikulu wahudumiwe. Walikuwa na tambo nyingi. Nikawauliza mmekuja ili niwahudumie au mnajivunia kuwa mmeambiwa niwahudumie. Wakanijibu Tumeambiwa na Mkubwa toka Ikulu kuwa Utuhudumie. Mie nikawajibu wasio kuwa na wakubwa huko ikulu je siwezi wahudumia? Basi wakaanza mikwara kama hutaki tunamwambia.
Nikawajibu, vizuri mwambieni siwezi wahudumia, kwakua mmetanguliza jina lake na cheo chake. Mwambieni mimi nahudumia wananchi bila kufuata upendeleo. Kweli niligoma. Nikaendelea hudumia wananchi wengine. Kesho yake wakarudi wakiwa na adabu wanyenyekevu, wakiomba niongee na huyo mkubwa wa ikulu. Nikaongea nae akaniomba radhi kwa niaba yao. Akasema unajua hawa ndugu zetu wakisha jua tuko mahala fulani wanaanza majivuno hawajui taratibu za kazi. Basi nikamwambia nilitaka wajifunze. Baadae nilitatua tatizo lao. So kuwa Ikulu si cheo bali ni dhamana ya kulitumikia Taifa.
Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema Ampe pumziko lililo jema. Asante kwa kulitumikia Taifa lako.