Ha ha ha! Wewe wasema. Sijaongea hayo yote nimeongelea nafasi aliyopewa marehemu. Na hii ndo ilikuwa mada husika. Nadhani hujui muundo wa Utumishi serikalini. Kuna muundo wa kiutumishi serikalini. Ambao mtu kama hujui utaishia kuwa mbishi tu.
kuhusu muundo wa utumishi inahitaji muda kuelezea na kufafanua ili uweze fahamu. Kwa kifupi. Katibu Tawala Mkoa ni ngazi ya juu ya kiutumishi. Huyu ndo msaidizi na mshauri wa karibu wa RC. Na ndiye mwenye dhamana ya watumishi wote wa serikali katika mkoa. Hata wakurungezi wa idara na vitengo vyote anauwezo wa kutoa maelekezo itapobidi.
DCI, huyu ni mkurungenzi wa makosa ya jinai. Anashughulika na makosa yote ya jinai hawezi toa maelekezo ya kiutendaji kwa watumishi wengine wa umma. Yeye kitengo chake ni huko katika mashitaka na mambo yote ya jinai basi.
RAS ambae ni Katibu Tawala katika mkoa wake anapokea taarifa zote za utekelezaji katika mkoa kutoka idara zote za serikali. Ikiwepo Polisi, TRA, Halmashauri, Hospitali za Mkoa, na taasisi zinginezo. RAS kwa muundo wa sasa ndiye Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.
Yeye ndo mwandaaji wa Taarifa inayokwenda Ikulu kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Taifa.
Huyu anaweza toa maelekezo ya kiutendaji kwa wakuu wa idara au taasisi za serikali zilizopo katika mkoa, inapobidi na maelekezo yakazingatiwa. Pia RAS ndiye mpitishaji wa bajeti ya mkoa na halmashauri zote katika mkoa baada ya kupitisha bajeti zao upeleka kwa RAS ili aweke sahihi na Mkuu wa Mkoa. Pia RAS anaweza toa maoni iwapo ataona inafaa katika bajeti hizo. Na ndiye upigia bajeti zote za mkoa chapuo ili ziweze kukubalika wakati wa mjadala wa bajeti na Kamishina wa bajeti kabla wizara haijawasilisha Bungeni.
Hivi unajua watumishi toka Ikulu, wakienda katika majukumu ya wazi kiutendaji, si yakificho wana ripoti kwa nani? Hasa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inapohusishwa katika majukumu hayo. Nimekuwa nikiona watu wanadharau sana nafasi ya Katibu Tawala Mkoa. Nadhani ni kutokujua miundo ya Kiutumishi. Ni nafasi kubwa na nyeti sana kiutendaji. Na huyu kwa lugha nyingine ni Mwajiri, na msimamizi mkuu wa watumishi wote katika Mkoa.