Katibu wa TEC: Maaskofu wanahitaji kuisoma mikataba iliyosainiwa, walipoitwa hawakuambiwa kulikuwa na nini

Unavyoandika kwa kirefu unakuwa unaanika utupu wako wa kichwani. Elewa tofauti ya kupangisha na kuuza.

TICTS alikaa pale TPA miaka 22 na ameshaondoka, bandari yetu tuliiuza?.

Mnakuja na maneno ambayo mkiyatumia mnajua mtateka hisia za wajinga wenzenu, eti bandari imeuzwa!. Stupid mindset.
 
Wewe ndiye maamuma usiyejua maana ya bandari kisasa, tatizo la wajinga huwa hamjijui kwamba hamjui hivyo mnazidi kuusambaza ujinga wenu kwenye jamii.

DPW ni mmiliki wa mzigo wa madini uliopo kule DRC na huko marais wawili wameshamaliza kutia saini mikataba ya kibiashara tulikuwa tunasubiriwa sisi tu. Kagame alishasaini na Tshisekedi hali kadhalika.

Huku Tanzania ndio kuna wajinga weengi mmoja wao anaitwa Kalamu, wanapinga vitu wasivyovijua faida zake zitakuwa ni zipi kwenye ongezeko la kodi ya hazina na kwenye uchumi mzima wa taifa.

Hamza ni hazina ya taifa anaongoza TCAA mamlaka ya anga wakati huo huo anaingia mikataba yenye kuja kuingiza pesa nyingi kwenye hazina ya nchi. Huwezi kabisa kumlinganisha na mawakili wengi njaa tulionao.
 
TICTS naye alitusainisha IGA?
haya sasa tuyaache, yamekwishapitwa na wakati mkuu wangu 'steve'.
Nisome tu kama nilivyojieleza hapo juu.
 
Unavyoandika kwa kirefu unakuwa unaanika utupu wako wa kichwani. Elewa tofauti ya kupangisha na kuuza.
Nikueleze tu wazi juu ya hili la "utupu". Mimi nikiwa mtupu, wewe hata ile akili ya kukupeleka chooni utakuwa huna. Utakuwa huna tofauti yoyote na ng'ombe zizini.
Katika hili usiwe na mashaka juu ya ninachokizungumzia hapa.
Hili haliwezi kamwe kuwa na ubishi wowote kati yetu. Umenielewa!
 
Katika maswala ya "Bandari" huko hakuna 'Rocket Science' ngumu ya watu kushindwa kuielewa, isipokuwa watu waliolala akili kama wewe hapo unayeshangaa wanachofanya DP World (na kwako, ni hao tu DP World) wenye uwezo huo.
Ungeweza kuwa na akili za kutosha kuelewa unachoelezwa, ungekuwa ulishatambua muda mwingi sana; lakini kwako huu ni mlima usioweza kuupanda.
Na hali ni hiyo hiyo, inapokuja kwa watu unaoona wewe ni mahiri katika eneo fulani. Huyo Hamza, hana lolote la kujivunia katika elimu yake. Alijitokeza kutetea mikataba hii ya DP World, na kujionyesha wazi kabisa kwamba elimu hana; lakini kwako, (kama siyo Hamza huyo huyo), unamwona kama ndiye mtaalam asiye na mfano.

Kwa hiyo, kiujumla, umekwisha jionyesha wazi kwamba, elimu ya kutosha huna; na unachokitetea hukijui. Ila kilicho wazi, unayo maslahi makubwa na DP World.
 
Samia angekuwa anasikiliza mawazo ya kipuuzi kama haya ya kwako angekwama siku nyingi sana. Hekima sahihi anayoitumia ndio inafanikisha uwekezaji wa DP World pale bandarini.

Hamza sio tu kwamba ametetea mkataba huu, yeye ndiye aliyeshiriki kuuandaa huko Dubai, pia ameandaa mikataba mingi sana ya awamu ya JPM.

Manunuzi ya ndege zote 13 zilizokuja yalianza na utiaji saini ya makubaliano ya kibiashara ambayo Hamza alisaini kwa niaba ya TZ kabla hata ndege hazijaja.

Roho mbaya inakupeleka pabaya sana wewe dada.
 
Mkataba wa miaka 30 umesainiwa tayari umebaki utekelezaji wa kivitendo pale bandarini. SSH amefunga goli kali sana la kisigino.
 
Mkataba wa miaka 30 umesainiwa tayari umebaki utekelezaji wa kivitendo pale bandarini. SSH amefunga goli kali sana la kisigino.
Hii ni mipasho isiyokuwa na maana yoyote na sitapoteza muda nayo tena.
Alichofanikiwa nacho ni kuwaonyesha watu waziwazi kuwa yeye ni tapeli na fisadi. Hana heshima tena.
 
EEeeenHEEeeee!
Acha niwe na "roho mbaya" kwa mtu yeyote wa aina yako. Hiyo ni beji ya heshima kabisa ninayoivaa kwenye paji la uso, wakati matapeli wanapoona hivyo.

Samia hawezi kusikiliza mawazo yangu, kwa sababu Samia ni fisadi na tapeli; kwa hiyo unachoeleza hapa ni upuuzi.
Hamza hana hadhi ya kujadiliwa kama msomi kati ya watu wanaojua maana ya usomi ni kitu gani. Kwa mtu kama wewe, ambaye unakula toka mikononi mwake, au ndiye Hamza mwenyewe, sioni tatizo lako kutomuona hivyo.
 
Ndani ya mwezi mmoja pale TPA kutakuwa na uendeshaji tofauti kabisa na ule tuliouzoea. Tujiandae kisaikolojia.

Taarifa za ndani zinasema Profesa Tibaijuka aliyekuwa mpingaji mkuu wa DP World hivi sasa kakubaliana na kila kitu kinachotaka kuanza kutekelezwa. Bado mrembo Kalamu.
 
Hii ni mipasho isiyokuwa na maana yoyote na sitapoteza muda nayo tena.
Alichofanikiwa nacho ni kuwaonyesha watu waziwazi kuwa yeye ni tapeli na fisadi. Hana heshima tena.
Heshima anaipata kutoka kwa wafanyabiashara wanaoagiza na kuuza bidhaa nje ya nchi. Heshima anaipata kutoka kwa wale wateja wa TPA waliokuwa wamekwisha ikimbia bandari na sasa watarudi tena kwa kasi kufuata huduma bora.
 
Umegeuka sasa na kuwa mtu wa mipasho?

Tibaijuka hawezi kuunga mkono ule upuuzi wa IGA, hilo ndilo kila mara ninalokukumbusha lakini mtu kilaza, tapeli, fisadi kama wewe akili yako haiwezi kamwe kulielewa hilo.
Hutaki kuelewa tofauti iliyopo kati ya mikataba chini ya IGA na mikataba hii inayofanyika sasa. Hapo ndipo ujuha wako unapolalia.
 
Heshima anaipata kutoka kwa wafanyabiashara wanaoagiza na kuuza bidhaa nje ya nchi. Heshima anaipata kutoka kwa wale wateja wa TPA waliokuwa wamekwisha ikimbia bandari na sasa watarudi tena kwa kasi kufuata huduma bora.
Ukiulizwa ni wafanya biashara gani walikimbia bandari huwezi kuwataja. Ukilaza unaanzia hapo.
"Huduma bora" hailetwi na DP World pekee, ambaye ndiye katika akili yako pekee mwenye huduma bora. Ujinga wako unaanzia hapo.
Usitake kuwapakazia wafanya biashara wote waonekane kuwa hawajali maslahi ya nchi yao kama mlivyo nyinyi, genge la mafisadi ambao lengo lenu ni kuikabidhi nchi kwa hao waarabu.
 
Mimi nipo karibu sana na watendaji waliofanikisha huu mkataba wa DP World, ninachokuambia na ukiamini.

Prof Tibaijuka hutamsikia tena akiongelea masuala ya article number 4 ya IGA, keshaupata ufafanuzi muafaka aliokuwa anauongelea mpaka akafikia hatua ya kuhojiwa na chombo cha habari cha kimataifa.
 
Wafanya biashara wa DRC wengi wanapitia Mombasa Kenya, waulize kwanini. Majirani zetu wa kusini Msumbiji waliacha kutumia bandari yetu waulize kwanini.

Ucheleweshaji katika ushushaji wa makasha, urasimu unaotengenezwa na watendaji wetu ili wapate chochote baada ya kufikiria kwamba nchi wanaipotezea wateja.

DP World watamchukia sana wajinga wachache wanaoendekeza njaa bila ya kujali efficiency nzima ya TPA.
 
Wafanya biashara wa DRC wengi wanapitia Mombasa Kenya, waulize kwanini. Majirani zetu wa kusini Msumbiji waliacha kutumia bandari yetu waulize kwanini.
Huu ndio upuuzi. "...wafanya biashara wa DRC wengi wanapitia Mombasa....", takwimu hizo unazo wewe?
Nikikwambia elimu yako ni ndogo sana kutambua mambo, usione kuwa ninakuonea. Nasema ukweli unaojidhihirisha wazi katika maandishi yako.
Msumbiji atumie bandari ya Dar es Salaam, hivi unaelewa hata jiografia ya eneo hili ilivyo?

Haya. Kama DRC walikimbilia Mombsa na kuiacha Dar es Salaam, Mombasa nako kuna DP World unayoililia kila mahala wewe kama kichaa?
 
Mimi nipo karibu sana na watendaji waliofanikisha huu mkataba wa DP World, ninachokuambia na ukiamini.
Nje ya ufisadi na utapeli unaoihusu IGA ya DP World, wewe huna jingine lolote la ziada katika maswala haya ya bandari.

Mabandiko yako yoooote humu JF tokea uingie ni swala la DP World pekee na IGA yake.

Huna uhusiano wowote na ufanisi unaofanywa na bandari zetu, ingawa sasa unatumia kinga hiyo kujificha kwenye kichaka cha haya unayoyapigania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…