Serikali unajua maana yake ni nini?Hiyo ni imani yako potofu, ninao ufahamu kwamba kurahisisha kazi za bandari ni kuifungua nchi, ni kuwezesha biashara ifanyike kwa haraka zaidi na pia ni kusafisha jina la bandari yenyewe kwani siku za nyuma wizi na ufisadi mwingi wa hapo mahali uliondoa kabisa sifa ya kupitishia mzigo wako Tanzania.
Usidhani kuwa kila mtu anafurahia maamuzi ya serikali kuingia mkataba, wapo wengi tu wenye vitumbua vyao vilivyoingia mchanga.
Hao unaowasema kuwa na "vitumbua" wanafugwa na nani?
Pamoja na upungufu mkubwa ninaouona toka kwako kuhusu ufinyu wa upeo; jambo ambalo unalisukuma sana mbele na ambalo ndilo mlilomshikisha Samia ni kudhani kwamba sisi kama nchi hatuwezi kufanya kitu chochote kutatua matatizo , hata yale madogo yaliyo katika uwezo bwetu bila ya kukimbilia hao mnaowatafuta waje hapa kuyatatua. Mbaya zaidi, hamuonyeshi uwezo wowote wa kusimamia hayo mnayotaka yatatuliwe na hao wageni. Mmeshindwa hata kusimamia hawa raia wenu, mtaanzia wapi kuhakikisha hao wageni watafanya kazi zao kwa maslahi ya nchi yetu.
Pamoja na hayo yote, niseme wazi hapa, hakuna hata sehemu moja uliyotetea mgeni mwingine yeyote mbali ya DP World. Wewe unamjua tu huyo basi? Sasa huoni maajabu hayo?