Mtu kutaka haki yake si ujuha.
Nyerere alienda New York City mwaka 1959, akawa anahojiwa katika jopo la kipindi cha TV cha former first lady wa US, Mrs. Eleanor Roosevelt, mke wa Rais Frank Delano Roosevelt.
Katika mahojiano yale, Nyerere aliulizwa, watu wako hawako tayari, hawana elimunya kuendesha nchi, huoni kwamba Watanganyika kupata uhuru sasa ni mapema sana?
Nyerere akatoa mfano mmoja wa kifalsafa sana. Akasema, ukimkuta mtu ana koti lake, koti halimtoshi vizuri, utamwambia wewe nipe hili koti lako halikutoshi? Akasema muache mtu na koti lake, ni lake, kama linamtosha au halimtoshi ni suala jingine, yeye mwenyewe ataamua kwa uhuru wake alifanye nini koti lake.
Akasema tulikuwa nanuhuru kabla ya wakoloni, hata kama hatukuwa vizuri sana, lakini tulikuwa tunajiendesha wenyewe, tunataka kurudi kujiendesha wenyewe tuamue mambo yetu. Ni haki yetu.
Ukweli kwamba koti halimtoshi hauondoi ukweli kwamba koti ni lake, haukupi wewe haki ya kuamua afanye nini nankoti hilo.
Haki ya mikutano ya hadhara ni ya kikatiba, waachieni watu wawe nayo. Kama mitandao ina ufanisi zaidi, ukiwaingezea na hiyo haki ya mikutano on the ground utaharibu nini? Ni haki yao.
Msikilize Nyerere akidai uhuru wa Tanganyika anavyopangua hoja hii ya kusema "uhuru huu haukufai"