Kaka Paskali, natofautiana na wewe kwa kiasi kikubwa sana ukilinganisha na nilivyowahi kutofautiana na wewe huko siku za nyuma kabla ya post hii..!! Usisahau uliitwa kuhojiwa na toka pale ni kama uliufyata flani hivi..!!
1. Mfikilie mpiga kura aliyeko Lituhi huko wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na unahitaji kufanya naye mkutano wa kisiasa. Asilimia kubwa ya walioko huko (hii ni kwa vijiji vyote) hawana smartphone, bando kwao ni shida etc. Mtu wa hivi unafanyaje naye mkutano wa KIDIGITALI..??
2. Ulishawahi kutana na walimu/ watu waliopewa vishikwambi wakati wa sensor..??? Ilikuwa tabu sana kwenye kuvitumia. Na ukumbuke hao ni wali na wengine wana uelewa wa maswala ya mitandao. Lakini walipata shida haswa.
3. Mfikiri mtu aliyeko mchoteka kule Tunduru mbele ya Mbesa Mision. Hivi kufanya naye mkutano wa kidigitali mtu yule aliyeko huko, au aliyeko Lusaunga huko Biharamulo, au aliyeko Mtinko Singida ni rahisi kama mnavyofikiria wewe na mto mada pamoja na wengine wenye mtazamo huo?
4. Huko seriali tu, we tuma e-mail leo halafu usikilizie. Serkali hadi leo bado ni mwendo wa hard copies. Ukitaka wakushangae jifanye unawasiliana kwa mail.
5. TAKWIMU ZENU MNZOTUMIA KWASHAWISHI WATU KUWA MIKUTANO YA KIDIGITALI INAWEZEKANA NI ZA MJINI TU, TENA KWA BAADHI YA WATU KAMA VILE ma-MD, Directors, Managers, supervisor etc. Imajini, hapa Dar tu kuna watumiaji wangapi wa viswaswadu??
Paskali, tuwe realistic. Sisi mikutano ya kidigitali bado sana. Kwanza kuna sehemu ndani ya Tanzania bado wana 3G na wengine 2G. Hata hiyo 5G inayotangazwa sana ni mbwembwe tu. Wenye simu ya kuhandle hiyo 5G inawezekana kabisa hata wewe
Pascal Mayalla na mwenzio
comte bado hamzimiliki. SI kwa maana ya uwezo kifedha, ila kwa maana ya uwezo wa mitandao ya simu kutoa huma hiyo. Kama kuna towers zenye capacity ya 5G hapa Dar (achia mbali Tanzania) itakuwa labda karibu na airport au mahoteli makubwa ambako wanalengwa watu wanaotoka kweny nchi zenye huduma hizo