Katika dunia ya sasa, mheshimu sana yule anayefunga safari kuja kukutembelea "physically"

Katika kutembeleana naomba sana tupeane taarifa before.Mimi nathamin sana kutembelewa ila ukiingilia ratiba zangu kwakwel unakua hujanitendea haki.

Kwamfano kuna day ilikua j2 nimetoka kanisan saa 8 halaf saa 9 tuna tamasha ghafla napokea cm sista na madog pamoja na maza mkubwa wamefika kunitembelea home.
Aisee siku iliharibika vibaya sana maana mimi ndio mwenyekit wa kwaya halaf ndio mpiga vyombo/muziki so sitakiwi kosekana...halaf huku home wageni.SIKU ILIISHA VIBAYA SITAKI HATA KUKUMBUKA.kwa kifupi NILIHARIBU KOTE KOTE.

tupeane taarifa watembezi.
 
Saaaawa mpendwa
 
Hawa wavamizi sasa na sio wageni
 
Kwa wenye mawazo haya, hawana undugu.
 
Usingekuwepo nyumbani, ungeeleweka. Nafikiri hukutumia busara siku hiyo ndio maana ukaharibu kote.
 
Mmh huyo mke amekua vending machine, ukiingiza pesa tu unapata bidhaa!
 
Usingekuwepo nyumbani, ungeeleweka. Nafikiri hukutumia busara siku hiyo ndio maana ukaharibu kote.
Ni kwel mkuu.Nilikua home na ndio nikabugi kuamua wapi niwepo na wapi nipige chini.lakin kote nililazimika kuwepo.
 
Mmh huyo mke amekua vending machine, ukiingiza pesa tu unapata bidhaa!
Mwanamke/mtu mzima huwa halindwi bali anapaswa kujilinda mwenyewe. Sasa kama anamlinda mkewe dhidi ya wageni wanaokuja nyumbani, vp kuhusu huko ofisini au akienda dukani?
 
Aamuwe kumuweka mkewe lockdown nyumbani πŸ˜‚
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ tena unaweza kukuta mwanaume wa namna hiyo mwenye wivu sana na mkewe ndiye anapenda sana kuchombeza wake za watu wengine. Hii dunia hii kweli kanyaga polepole
 
Kazi ya kutembelea watu makwao halafu kwangu hawaji siwezi mimi.
Kweli mdau, waafrika hasa watanganyika tuna hii kasumba kuna watu wamejijengea wao ni wa kutembelewa tu, hii inatokea hasa mtu akiwa na uwezo wa kubadilisha mboga anajiona ni VIP yeye ni wa kutembelewa tu. Hii kwangu sioni kama ni ujamaa yaani ni utwana zaidi ya ujamaa tunaohubiri!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…