Mimi tumezaliwa wawili kwetu ila tunakaa miezi mnne hatujapigiana simu, ila wote tuna wasiliana na mama, mama yangu kwao walizaliwa wanne wamebaki wawili nao pia hawawasiliani, mara ya mwisho kwenda kwa uncle na mama mkubwa ilikua 2001, huwa hatupigiani simu labda itokee kuna tukio kama msiba au harusi, cousins na nephews hakuna tunayewasiliana kama hamna tukio, baba yangu alifariki tukiwa wadogo so hatujawahi kuwa na ukaribu na upande huo, familia yetu kila mtu na marafiki zake unaweza kufa ikapita mwaka na ndugu wasijue, kwetu undugu hakuna na hatuna bifu tukikutana ni salamu na bia mbili tunaachana tutakutana baada ya miaka mingi, ikifika xmass huwa naumia natamani na sisi tungekua familia kubwa tukutane tusherekee ila ndio ishakua hivi, nakumbuka siku ya graduation yangu alikuja bimkubwa peke yake tulipotoka kwenye mahafari tukarudi nyumbani akanipa mpunga nikasherekee mtaani, nikaenda kwa mshikaji wangu nae alikua amegraduate nikakuta sherehe na ndugu wengi nilitamani sana
Sent from my SM-G610F using
JamiiForums mobile app