Katika dunia ya sasa, mheshimu sana yule anayefunga safari kuja kukutembelea "physically"

Katika dunia ya sasa, mheshimu sana yule anayefunga safari kuja kukutembelea "physically"

Pia kutembeleana kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa unayemtembelea na anayekutembelea. Mf. Mi niliweza kumpata fundi tiles kutoka kwa nyumba niliyotembelea na kupenda jinsi alivyoweka tiles za nyumba yake na kumuomba namba za simu za huyo fundi. Any way kutembeleana kunaimarisha undugu, urafiki pamoja na ushirikiano mwingine.
Well said bro.
 
Mimi tumezaliwa wawili kwetu ila tunakaa miezi mnne hatujapigiana simu, ila wote tuna wasiliana na mama, mama yangu kwao walizaliwa wanne wamebaki wawili nao pia hawawasiliani, mara ya mwisho kwenda kwa uncle na mama mkubwa ilikua 2001, huwa hatupigiani simu labda itokee kuna tukio kama msiba au harusi, cousins na nephews hakuna tunayewasiliana kama hamna tukio, baba yangu alifariki tukiwa wadogo so hatujawahi kuwa na ukaribu na upande huo, familia yetu kila mtu na marafiki zake unaweza kufa ikapita mwaka na ndugu wasijue, kwetu undugu hakuna na hatuna bifu tukikutana ni salamu na bia mbili tunaachana tutakutana baada ya miaka mingi, ikifika xmass huwa naumia natamani na sisi tungekua familia kubwa tukutane tusherekee ila ndio ishakua hivi, nakumbuka siku ya graduation yangu alikuja bimkubwa peke yake tulipotoka kwenye mahafari tukarudi nyumbani akanipa mpunga nikasherekee mtaani, nikaenda kwa mshikaji wangu nae alikua amegraduate nikakuta sherehe na ndugu wengi nilitamani sana

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
Nadhani wewe ndio wa kubadilisha upepo
 
Umesema kwel kaka, hakika kakuthamini mno, tena mazingira haya ya kwetu ya kazi mpk jmosi ukufika nyumbani hoi jpili unajikuta unataka kulala tu upumzishe mwili. Hali ya kutembeleana imekua ngumu mno.
 
Back
Top Bottom