Katika dunia ya sasa, mheshimu sana yule anayefunga safari kuja kukutembelea "physically"

Mkuu ulichoongea ni kweli kabisa, mimi nina ndugu zangu hapa dar,nina miaka mitano sijaonana nao na mbaya zaidi hata namba zao sina.
Ndugu zangu hawa ukiwatembelea ni kama umeenda kuwapa ghasia kwa kuwa uwezo wangu wa kifedha sio mkubwa
 
Hakika utandawazi umepunguza sana ukaribu wa wanandugu tuliouzoea
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wa humu JamiiForums.

Katika dunia ya sasa ambayo watu huweza kujuliana hali kwa njia ya simu/mitandao, muheshimu sana yule anayefunga safari kuja kukutembelea "physically"

Kuna mwalimu wangu mmoja alikuwa anaitwa Adonijah yeye alikuwa anatufundhisha somo la communications skills mwaka 2007 aliwahi kutuambia jambo la maana sana.

Mzee yule alitufundisha kwamba, muheshimu sana mtu anayeamua kukuandalia zawadi kwa mikono yake mwenyewe kuliko yule anayediriki kutoa pesa na kununua kisha akuletee.

Yaaani just imagine siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwako (Birtday) imefika na rafiki zako wanawiwa kukuandalia kitu cha kukupongeza nacho na mara nyingi huwa ni card pamoja na cake.

Kulingana na maelezo ya mwalimu wangu yule ni kwamba, siku zote mthamini sana rafiki ambaye atakuwa tayari kuchukua karatasi kisha akaandika salama za kukutakia heri ya siku yako ya kuzaliwa.

Mthamini sana mtu huyo kuliko yule anayetoa pesa yake mfukoni (let's say 5,000/=) kisha ananunua kadi na kukuletea au kumpa mtu alete. Aliyetayari kuandaa kadi kwa mikono yako anaweza kuwa anakuthamini zaidi kuliko yule aliyeinunua "ready-made" dukani.

Katika dunia hii ya sasa ya science na technology ambayo pesa/maisha yamekuwa magumu sana ni jambo la kawaida kukuta mtu na dada yake tumbo moja hawajaonana "physically" miezi 6 alafu wote wanakaa hapahapa Dar.

Unakuta mtu anafanya kazi katika taasisi binafsi (Bank) kuanzia jumatatu mpaka ijumaa, na kwa baadhi ya taasisi mfanyakazi anaenda mpaka siku ya jumamosi nusu siku, yaaani wanaingia saa mbili kisha wanatoka saa saba mchana.

Baba/ Mama anaondoka nyumbani saa 11 alfariji kuelekea kazini watoto wakiwa bado hawajaamka na kurejea usiku saa 4 watoto wakiwa tayari wamelala.

Jumapili ndio siku pekee ambayo mtu anapata muda wa kufanya shughuli ndogo ndogo za hapa na pale akiwa nyumbani kwake ikiwa ni pamoja na kwenda kanisani, kukagua madaftari ya watoto, siku hiyo hiyo afanye usafi, apumzike na mambo mengine mengi.

Ukiona mtu amefunga safari kuja kwako wewe ndugu, jamaa au rafiki ujue kuna mgonjwa, msiba au sherehe baaas, mbali na hapo fahamu kuwa huyo mtu amekuthamini na kukupenda sana. Mpe muda wako.

Give him your time, mpikie vizuri, piga naye story kwa maana huyo anakupenda. Kwanini ameamua kuja kwako? Kama suala ni kukusalimu tu si angeweza kukupigia simu kukujulia hali? Au unadhani yeye hana mambo ya kufanya mpaka akutafute physically? Ni kwa sababu anakupenda na kukuthamini.

Kwa bahati nzuri mimi ni moja kati ya watu waliobahatika kukaa na watanzania kutoka katika makabila mbalimbali. Mimi nimekaa sana na watu wanaitwa wazaramo. Hawa wazaramo mpaka sasa ndio kabila pekee ambalo bado ninaona wanao huu utamaduni wa kukutana ana kwa ana na wapendwa wao.

Kwa kusema hivi simaanishi kuwa makabila mengine hawana upendo wa namna hii, la hasha, bali ni kutokana na ukweli kwamba hawa ndugu zangu wazaramo wengi wao wapo katika ajira binafsi (wamejiajiri) kwa maana mtu wa namna hii anakuwa na namna ya kujipangia mambo yake kuliko yule aliyeajiriwa.

KUMBUKA: Mthamini sana mtu (ndugu/rafiki) anayetumia muda wake mwingi kukutana na wewe wakati angeweza kukujulia hali kwa njia ya simu tu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kuna Mazuri 'nimeyaokota' hapa Mkuu.
 
Huu ni upuuzi, kwa dunia ya sasa si rahisi kuheshimu mtu kama huyo. Unaweza kuwa na msichana ama mwana Mama tu basi juwa imekula kwako, atakuja kukutembelea na akiona tu una maisha mazuri basi juwa huyo harudi kwao na atafanya kila kitu asirudi mapema huku akikaa na kukupa stress kibao, mara ataomba hiki, mara milioni 1 akamtibie baba yake, sijuwi umnunulie kiwanja. Hapo ni demu tu na wala hauna mpango naye....yaani kina Kajala siku hizi wamejazana kila sehemu na mkoa.
 
Hii mada nimezungumzia zaidi kuhusu ndugu, jamaa na marafiki. Sasa wewe kama unawaza romamce muda wote hiyo ni wewe na akili zako tu mkuu.
 
Utamaduni huu ushapitwa na wakati, utakuja lazimisha mwishowe ukaja kutembelewa nawatu kama kina Kajala na mwanawe wanataka kulala nawe pamoja huku mkicheza uchi kitandani.
 
Kuna mtu anaweza kutaka kulala kitanda kimoja na kaka/dada yake?
 
Back
Top Bottom