Katika dunia ya sasa, mheshimu sana yule anayefunga safari kuja kukutembelea "physically"

Habari za wakati huu kaka na dada zangu wa humu JamiiForums.

Katika dunia ya sasa ambayo watu huweza kujuliana hali kwa njia ya simu/mitandao, muheshimu sana yule anayefunga safari kuja kukutembelea "physically"

Kuna mwalimu wangu mmoja alikuwa anaitwa Adonijah yeye alikuwa anatufundhisha somo la communications skills mwaka 2007 aliwahi kutuambia jambo la maana sana.

Mzee yule alitufundisha kwamba, muheshimu sana mtu anayeamua kukuandalia zawadi kwa mikono yake mwenyewe kuliko yule anayediriki kutoa pesa na kununua kisha akuletee.

Yaaani just imagine siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwako (Birtday) imefika na rafiki zako wanawiwa kukuandalia kitu cha kukupongeza nacho na mara nyingi huwa ni card pamoja na cake.

Kulingana na maelezo ya mwalimu wangu yule ni kwamba, siku zote mthamini sana rafiki ambaye atakuwa tayari kuchukua karatasi kisha akaandika salama za kukutakia heri ya siku yako ya kuzaliwa.

Mthamini sana mtu huyo kuliko yule anayetoa pesa yake mfukoni (let's say 5,000/=) kisha ananunua kadi na kukuletea au kumpa mtu alete. Aliyetayari kuandaa kadi kwa mikono yako anaweza kuwa anakuthamini zaidi kuliko yule aliyeinunua "ready-made" dukani.

Katika dunia hii ya sasa ya science na technology ambayo pesa/maisha yamekuwa magumu sana ni jambo la kawaida kukuta mtu na dada yake tumbo moja hawajaonana "physically" miezi 6 alafu wote wanakaa hapahapa Dar.

Unakuta mtu anafanya kazi katika taasisi binafsi (Bank) kuanzia jumatatu mpaka ijumaa, na kwa baadhi ya taasisi mfanyakazi anaenda mpaka siku ya jumamosi nusu siku, yaaani wanaingia saa mbili kisha wanatoka saa saba mchana.

Baba/ Mama anaondoka nyumbani saa 11 alfariji kuelekea kazini watoto wakiwa bado hawajaamka na kurejea usiku saa 4 watoto wakiwa tayari wamelala.

Jumapili ndio siku pekee ambayo mtu anapata muda wa kufanya shughuli ndogo ndogo za hapa na pale akiwa nyumbani kwake ikiwa ni pamoja na kwenda kanisani, kukagua madaftari ya watoto, siku hiyo hiyo afanye usafi, apumzike na mambo mengine mengi.

Ukiona mtu amefunga safari kuja kwako wewe ndugu, jamaa au rafiki ujue kuna mgonjwa, msiba au sherehe baaas, mbali na hapo fahamu kuwa huyo mtu amekuthamini na kukupenda sana. Mpe muda wako.

Give him your time, mpikie vizuri, piga naye story kwa maana huyo anakupenda. Kwanini ameamua kuja kwako? Kama suala ni kukusalimu tu si angeweza kukupigia simu kukujulia hali? Au unadhani yeye hana mambo ya kufanya mpaka akutafute physically? Ni kwa sababu anakupenda na kukuthamini.

Kwa bahati nzuri mimi ni moja kati ya watu waliobahatika kukaa na watanzania kutoka katika makabila mbalimbali. Mimi nimekaa sana na watu wanaitwa wazaramo. Hawa wazaramo mpaka sasa ndio kabila pekee ambalo bado ninaona wanao huu utamaduni wa kukutana ana kwa ana na wapendwa wao.

Kwa kusema hivi simaanishi kuwa makabila mengine hawana upendo wa namna hii, la hasha, bali ni kutokana na ukweli kwamba hawa ndugu zangu wazaramo wengi wao wapo katika ajira binafsi (wamejiajiri) kwa maana mtu wa namna hii anakuwa na namna ya kujipangia mambo yake kuliko yule aliyeajiriwa.

KUMBUKA: Mthamini sana mtu (ndugu/rafiki) anayetumia muda wake mwingi kukutana na wewe wakati angeweza kukujulia hali kwa njia ya simu tu.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Nyuzi Kama hizi...humu JF zimekuwa adimu sana siku hizi!
 
Binafsi ninauwezo sana wa kutembelea ndugu. Mwaka mmoja nilitoka bara nikaenda Unguja kwakuwa kuna ndugu zangu nikaenda kuwatembelea. Nikatumia siku 3 kuwasalimia wote. Hakika lilikuwa jambo kubwa sana. Na hii sio huko tu kila wakati nafanya sana hivyo.
Nimejikuta ni mtu ninayeufahamu ukoo wangu kwa baba na mama vizuri sana.
Kwangu ni raha sana kutembelea ndugu.
 
2025 tutawashawishi wananchi wampe Samia ushindi wa 90% Ushindi huu ni wa asante kwa kazi kubwa aliyoifanya.
Kwa utendaji wa RAIS Samia Sisi kama watanzania tulipaswa kumuacha achape kazi, watanzania ,Afrika ,Dunia inajua Rais Samia atashinda mafisadi.
 
Rais Samia amefanya mambo makubwa mazuri kwa muda mfupi wa utawala wake.
Rais Samia ni mtu mwenye huruma nami nakubaliana naye kabisa. Wanaomuogopa Rais Samia ukiwafuatilia kwa makini utagunduza kuwa ni watenda maovu na wanashikwa na uwoga kutokana na uovu wanaoutenda.
 
Kinachowafanya Wapinzani waweseke ni Kwasababu Rais Samia ame wa outsmart kwa kila kitu.
 
Bwana mkubwa Mbowe kama unapita hapa nakuomba ikiwezekana tembea kwa magoti hadi chamwino ukaombe radhi kwa Rais Samia la sivyo mtakufa tu mtakuwa mmekaidi sauti ya Mungu.
 
Utafiti umefanyika na unasema kuwa Rais Samia atawashinda mafisadi na wezi wa mali za umma.
 
Tunapenda Rais Samia asipate changamoto kubwa katika kupambana na CHADEMA pamoja na wanasiasa wengine uchwara wa upinzani.
 
Tanzania ya Samia inapendeza na kuwaka kila kona kwa maana huyu mama ni mwanadiplomasia mzuri sana.
 
Kuepuka kutongozeana wake na ku admire minyama nyama ya wake za watu. Kila mtu akae kwake. Tukutane neutral place Kama pub.
Mimi namaliza hata miaka mitatu sijaingia nyumba ya mtu. Misibani naishia kwenye hema, kwenye harusi tuonane kanisani au holini.
Sitaki umbea jumbani yangu na hata waif anajua. Akimualika rafiki yake namtizama huyo mgeni mwanzo mwisho mpaka atoke. Siku nyingine hamkaribishi.
Inaonekana una wivu na mke wako.Watakaomtongoza kamwe hawatakuja hapo nyumbani
 
Kinachowafanya Wapinzani waweseke ni Kwasababu Rais Samia ame wa outsmart kwa kila kitu.
Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania, Yampongeza Rais Samia na Kuipongeza Tanzania, Kujenga Mazingira Bora ya Biashara ya Mafuta, Uwekezaji.
 
adonijah abayo 😀 kutembeleana ilikuwa zamani saivi ni kuchorana tu ni bora kila mtu akae kwake ....cha muhimu cmu tu inatosha
.
 
Back
Top Bottom