Madame B
JF-Expert Member
- Apr 9, 2012
- 31,155
- 35,683
Hofu ya kufa mkuu usidhani masikhara.Hata huko anapoenda ataishi kwa KUTAPATAPA vile vile.
Alitakiwa atuliee tu, alikuwa anaogopa asichokijua.
Fear of the unknown is the greater threat than the actual threat itself.
Nakumbuka mwaka 2012 niliumwa, niliumwa mwezi mmoja tu, ila huwezi amini ilikuwa inafikia hatua pumzi inakata yenyewe, naona maruweruwe ya kifo, natapatapa kuitafuta pumzi.
Nashukuru Mungu, madaktari wa Muhimbili na kwa Mvungi Kinondoni ndio waliniponesha.
Mpaka leo hii nikienda hapo kwa Mvungi wanajua tabu ile niliyokuwa naipata. Niliishi nusu duniani, nusu akhera.
Kiufupi nilionja kifo.
Mtu ambaye anaweza kutoa ushuhuda wa hali niliyokuwa nayo kipindi kile ni Mtambuzi na somebody Man P. Japo wengi walikuja kuniona wodini, kama wapo wanaweza shuhudia hali niliyopitia.
Nilipopona nilianza upya kuanzia kuongea, kutambua watu, mpaka kutembea.