MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Clinton hakuachia urais. Rekebisha hapoHaya mambo hutakiwi kuyasema mbele ya jamii inayowaza kut.ombana kama sehemu ya mafanikio. Jamii ambayo mtu anawaza atafute hela ili awe na mademu wakali na awabadilishe kama nguo. Huo utaratibu uko nchi ambazo zishaachana na utapiamlo na uzinduzi wa vyoo vya misaada. Ukiishi sehemu watu hawana ustaarabu ukiwa kinyume nao inaonekana unajisikia au una kiherehere.
CEO wa McDonald's miaka michache nyuma hapo alifutwa kazi kwa kujihusisha na mahusiano na mfanyakazi wake. Hawakuishia hapo, walifanya uchunguzi na kugundua alijihusisha na wafanyakazi wengine watatu na alikuwa na kesi ya kujibu na hatimaye akirudisha kiasi fulani cha mamilioni aliyolipwa na kampuni. Ukitazama performance wise jamaa aliinyanyua sana brand ila hawakujali hilo.
Bill Clinton aliachiza ngazi ya urais wa Marekani kwa kesi ya kutoka kimapenzi na mmojawapo wa secretary wa White House, Monica Lewinsky.
Ukija bongo mambo ni tofauti kabisa. Degree za chupi, HR na wafanyakazi, mabosi na wafanyakazi, wachungaji na waumini. Fujo tu