Katika historia ya TISS, ni mara moja tu walifanya Press Conference, ilikuwa ni mwaka 2010, nini hasa kilijiri?

Mwanadiplomasia Mahiri

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
685
Reaction score
2,355
Nyakati kama hizi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2010 ambapo Rais wa kipindi hiko, Jakaya Kikwete alikuwa anajiandaa kutetea kiti chake kwa muhula wa pili na wa mwisho.

Ghafla kuna tuhuma za wapinzani zikaelekezwa Idara ya Usalama wa Taifa.

Katika hali isiyokuwa yaa kawaida, TISS kupitia kwa Jack Zoka ikaitisha Press kujibu tuhuma zile kama sikosei. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza na pengine ya mwisho kwa Idara hiyo kufanya hivyo.

Nini hasa kilijiri mpaka TISS wakaitisha press kinyume na taratibu zao?

Karibuni wakongwe.

Pia soma: Press Conference ya TISS!. Sio Bure....Kuna Jambo!
 
Ni nn kilitokea?
KAZI ni kipimo cha utu
 
Na ndo tukio la kijinga zaidi walilofanya
 
Bongo ni Bongo tu . Kule US, CIA press conference, matangazo ya ajira , nk Huwa ni vitu vya wazi kabisa. CIA mara kadhaa huongea na jamii ya wamarekani na dunia kupitia Press na media zingine hata mitandao ya kijamii pia.
Kiukweli Mimi mwenyewe nimeshangaa sana TISS kufanywa kama kilinge Cha wachawi kiasi kwamba idara ya usalama wa Taifa iwe ajabu kufanya press conference Africa tunaujinga wa ajabu sana
 
Africa itazidi kuwa Afrika tu. Waasia tuliokuwa nao sawa kiuchumi, kijamii, kijeshi, na kisiasa Leo wako mbali pengine mara 50 ya tulipo sasa. Thailand, Singapore, Philippines, Korea nk ni mifano mizuri
 
Bongo ni Bongo tu . Kule US, CIA press conference, matangazo ya ajira , nk Huwa ni vitu vya wazi kabisa. CIA mara kadhaa huongea na jamii ya wamarekani na dunia kupitia Press na media zingine hata mitandao ya kijamii pia.
Naaam tena huenda vyuoni kabisa kutangaza nafasi
Sio kificho, wanachoficha ni training , selection creteria na mission
 
Nyakati kama hizi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2010 ambapo Rais wa kipindi hiko, Jakaya Kikwete alikuwa anajiandaa kutetea kiti chake kwa muhula wa pili na wa mwisho.

Ghafla kuna tuhuma za wapinzani zikaelekezwa Idara ya Usalama wa Taifa.

Katika hali isiyokuwa yaa kawaida, TISS kupitia kwa Jack Zoka ikaitisha Press kujibu tuhuma zile kama sikosei. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza na pengine ya mwisho kwa Idara hiyo kufanya hivyo.

Nini hasa kilijiri mpaka TISS wakaitisha press kinyume na taratibu zao?

Karibuni wakongwe.
Yaani wajongo mnavyowachukulia hao tiss ni kama aliens fulani hivi..
Jamii yetu imejengwankwenye misingi ya uwoga nankufichwa mambo mengi..
 
Back
Top Bottom