Maudhui makuu ya mazungumzo ya viongozi hawa Tundu Lissu vs Mh. Rais Samia Suluhu Hassan [Brussels, Ubelgiji] na Mh. Freeman Mbowe vs Mh. Rais Samia S. Hassan [Dar es Salaam, Tanzania] ni
maridhiano ya kisiasa kwa mustakabali wa
kujenga Tanzania ya HAKI kama tunda la UPENDO na AMANI.
Hawa wanaonesha kutofurahishwa na hatua hii ya viongozi hawa wa CHADEMA kuonana na Rais na kufanya mazungumzo naye ambayo kiukweli ni hatua njema kuelekea kwenye maridhiano na upatanisho mkuu.
Hawa wanaamini kuwa ni kilichowakutanisha hawa ni zaidi ya mazungumzo tu. Wanadhani viongozi hawa kwa kitendo chao cha kukutana na Rais ni
UNYONGE na
KUUZA UTU wao na possibly wameenda kutulizwa kwa fedha - mulungula eti ili wanyamaze....
Hawa bila shaka ni watu wa ajabu sana na pengine bila shaka yoyote kuwa hawajui watakacho ktk harakati zao za kisiasa na kama wanajua, basi hawajui hicho wakitakacho watakipata kwa njia gani.
Hawa viongozi, Mh. Freeman Mbowe [M/Kiti CHADEMA - taifa] na Mh. Tundu Lissu [M/M/Mwenyekiti Tanzania Bara si tu wamezungumza na kila kitu kubaki gizani, bali wametoa.
View attachment 2145007
mrejesho (feedback) ya maudhui ya mazungumzo hayo hadharani kila mtu akiona na kusikia...
Hivi ukiwasikiliza hawa viongozi wa chama hiki kikuu cha upinzani hapa chini kwenye video hii, kuna mwana - CHADEMA mwenye akili timamu atasema haelewi lolote kweli...?
Sikiliza...
Mazingira ya kuendesha siasa za upinzani hapa Afrika hutegemeana na aina gani ya uongozi uliopo madarakani wenye dhamana ya kuongoza nchi. Ninasema hivyo kwa sababu viongozi wengi hapa barani Afrika, wale waliopo madarakani ama wale hata waliowahi kushika madaraka ya kuongoza serikali za nchi zao wana sifa zinazofanana sana kiutendaji.
Wanapoingia madarakani kwa mara ya kwanza wanakuwa karibu sana na wananchi na huku wakitoa ahadi lukuki kuwa watazingatia, kutii na kusimamia matakwa ya katiba. Na kwa msingi huu hujinadi kuwa watahakikisha kuwa wanatenda haki kwa watu wote kupitia haki zao zote zilizowekwa kikatiba.
Lakini wakinogewa na kulewa na madaraka hapo ndipo linapogeuka kuwa ni tatizo kubwa. Pale udhaifu na madudu yao ya kiuongozi yanapoanza kuwekwa hadharani, basi hapo ndipo madhila ta siasa zao huanza kuonekana, huku wahanga wakubwa wakiwa ni vyama makini na vyenye nguvu vya upinzani, wanaharakati, wanahabari na vyombo vya habari.
Si jambo baya kwa mhanga wa siasa chafu za chama tawala kufanya maridhiano na kiongozi wa nchi. Hii inatokana na ukweli kwa inahitajika "entry point" ili kurudisha mazingira rafiki ya chama cha upinzani kuendesha shughuli zake za kisiasa. Kuna mambo machache ambayo haiyumkini yanapelekea kuwepo kwa dhamira hii njema, ambayo kwa uchache ni;
1. Nchi ikiwa na katazo la Rais la wanasiasa wa vyama vya kufanya siasa za wazi ili wapate kunadi sera, kuimarisha vyama vyao na kuongeza idadi ya wanachama
2. Nchi ikiwa na viongozi na wanachama wengi wa vyama vya upinzani wakiwa mahabusu huku wakikabiliwa na kesi zinazotokana na kuendesha shughuli zao halali za kisiasa.
3. Nchi ikiwa inakabiliwa na wakimbizi wengi wa kisiasa wanaoishi nje ya nchi kwa hofu ya usalama wa maisha yao, kwa sababu zitokanazo na shughuli zao za kisiasa.
4. Nchi ikiwa na watu wengi waliouawa, kujeruhiwa, kupata ulemavu kisa eti kutokana na hisia ya wao kuwa ni wapinzani wa chama tawala.
5. Nchi ikiwa na watu waliopoteza ajira, kushushwa vyeo, kuhamishwa katika maeneo yao ya kazi kutokana na misimamo yao ya itikadi za kisiasa.
6. Nchi kuwa na watu ambao akaunti zao za fedha, biashara ama vitega uchumi kuhujumiwa kutokana na misimamo yao ya itikadi za kisiasa.
Haya ndiyo mambo ya msingi ambayo yamepelea FAM na TAL kuweza kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Rais SSH. Viongozi wa chama makini ambacho kimepitia changamoto nyingi zitokanazo na rafu mbaya za kisiasa katika kipindi cha awamu ya tano ya uongozi wa kiimla wa JPM hawawezi kukwepa kufanya hivyo. Nafasi nzuri ikitokea ya kuponya majeraha basi milango huwa wazi ili kurahisisha zoezi hilo.