π Hapana, mtoto alikua anachezea cm, naona akaandika ivo, nimeelewa hakuna uchawi ππΎπ€£Niambie wapi nije supervision na vyombo vya habari unielezee vizuri ujibu na maswali yanguπ€£
Mbona mnanichanganya ninyi?Nahama nchi nahamia Burundi.ni mwehu pekee na mvivu wa kufikiri anaeamini mungu yupo ila uchawi haupo
Naomba uwe na mimi Ms R , kama kweli upo serious.Mkuu leo usiku nipo nawewe,, naamini kesho utakuja na uzi mpyaaaaaππ€πΎπ€ΌββοΈπ wabishi kama nyie ndo tunawataka.
Hakuna shida kabisaNaomba uwe na mimi Ms R , kama kweli upo serious.
Kinahitaji nini na nini Ms rHakuna shida kabisa
Relax mm ndo najuaKinahitaji nini na nini Ms r
Nachoona Madam ni unachanganya kati ya "Kiamini uchawi upo" na "Kuamini katika uchawi".....Katika hoja zako unaamini mtu kuamini uchawi upo basi eti anaamini katika uchawi kwamba hawezi fanikiwa bila uchawi nk sihivyo.Kwa kweli nawashukuru wazazi wangu na Walezi wangu na babu wa babu zangu na bibi wa bibi zangu kwa kuwa hii ajenda haikuwa kabisa sehemu ya ukoo wetu si kwa baba si kwa mama.
Niliwahi kumuuliza babu yangu mmoja kuhusu je amewahi waona wachawi? Akiwa na miaka takribani 78 hivi na mimi nimeshamaliza Chuo kikuu udaktari alinijibu "hayo mambo mimi nayasikia tu stori kila mtu anasema naye kasikia, mimi sijayawahi hata yaona" RIP Babu yangu na Bibi yangu na wazazi wangu kwa ujumla, mlinifanya imara nitabaki kuwa imara daima.
Nawasihi wote tuepuke hizi fikra za Imani ya uchawi kwani ni adui wa maendeleo. Inawezekana kuendelea na kufanikiwa nje ya fikra hizi na nje ya kufanyiwa ushirikina shirikina.
Nimekusoma ila nami hoja yangu ni kuwa, imebaki kuwa dhana ambayo yule aiaminiye ana hasara. Hakuna kuendelea kupitia masharti ya dhana hiyo, halipo hilo. Wasome wapeane digrii ila mwisho wa siku wote hao wanafanya kazi halali na wasipofanya wanakufa masikini tu. Huku sasa kwetu, mtu hata elimu hiyo hana ila anasumbua watu wote na hela wanampelekea na anawatuma vitu vya ajabu. Akikamatwa kilio.Mheshimiwa,
Kuishi Tanzania na kuijua Tanzania hakumanishi Zambia haipo, maana yangu ni kwamba kutokupitia hali hiyo hakufanyi uchawi usiwepo.
Binafsi sishabikii uchawi wala ushirikina wa aina yeyote na wala haunipi hofu katika kufanya mambo yangu ila haimanishi haupo, maana hata kifo kipo lakini haimanishi niache kupambana kuishi vizuri.
Kuna elimu ya uchawi ngazi ya degree kabisa sio mambo ya kufikirika.
Elimu bora sio kuficha uchawi kwamba haupo ni kuhakikisha watu wanafanya mambo yao bila hofu ya uchawi na kutojiingiza huko kuharibu maendeleo na mambo chanya katika jamii.
Nimewasilisha.
Mkuu uchawi ni nini ?Iwe club au elimu ila ni ya wachawi. LENGO langu sio kushabikia uchawi. Hayo mengine uko sahihi. Mambo hasi kwenye jamii ni mengi ni lazima tuyashinde ikiwemo na uchawi ili kuwe na jamii yenye maendeleo chanya.
Hapo nakuunga mkono asilimia zoteNimekusoma ila nami hoja yangu ni kuwa, imebaki kuwa dhana ambayo yule aiaminiye ana hasara. Hakuna kuendelea kupitia masharti ya dhana hiyo, halipo hilo. Wasome wapeane digrii ila mwisho wa siku wote hao wanafanya kazi halali na wasipofanya wanakufa masikini tu. Huku sasa kwetu, mtu hata elimu hiyo hana ila anasumbua watu wote na hela wanampelekea na anawatuma vitu vya ajabu. Akikamatwa kilio.
Niseme kuwa, nguvu iliyo ndani ya positive thinkers ni kubwa kuliko watu wanaodai kuwa na mambo hayo... The power of positive thinking iwafikie wote iwakomboe
Swali zuri. Imani bila matendo ni bure. Sasa unaamini vipi mambo hujayaona? πNachoona Madam ni unachanganya kati ya "Kiamini uchawi upo" na "Kuamini katika uchawi".....Katika hoja zako unaamini mtu kuamini uchawi upo basi eti anaamini katika uchawi kwamba hawezi fanikiwa bila uchawi nk sihivyo.
Mimi nadhani mapambano hayo unayolenga yalenge kwenye kupambana na fikra za kuamini katika uchawi ndio inaleta madhara katika jamii kama mauji ya albino nk na sio kupambana na watu kufuta imani kuwa uchawi upo hio imani inamzizi mzito wa imani ya kidini pia.
Mimi sijawai kuona tulip lolote la kichawi wala sina ushahidi wowote kushuhudia uchawi tangu nizaliwe ila naamini uchawi upo maana kitabu changu cha Dini ya kiislam kimesema upo, sasa kukataa kuwa haupo hii inakuwa ni sawa na kuoingana na maandiko ya kidini.
Pia nashangaa mtu anayesema anaamini MUNGU then anasema uchawi haupo hii inaonesha kuamini kwako Mungu kuna mashaka sana huna imani na wala huzingatii maandiko yake maana both Islamic and Christian writtings zime eleza uchawi upo.
Kwangu mtu anayeamini uchawi upo na haamini kwenye uchawi so perfect kuliko huyu ambae haamini kua uchawi upo.
Swali kwako Mdam:
Unaamini vipi dini yako na uamini uchawi.
Afadhali jamani. π₯°. Hii debate nzuri sana natamani siku moja tufanye live tualike na faculty husika kutoka huko UDHapo nakuunga mkono asilimia zote
πππππ Hicho kibubu kimetoboka panya wamebeba, njoo tukuazime chetuMkuu
Ushawahi weka pesa kwenye kibubu zaidi ya mwaka, na kupasua unakuta 5000 uliyoweka siku ya nyuma!?
Makaburi haya haya ambayo wote tukienda kuzika tunakaa tena juu yake au? π€£Siku utakuja kuamka makaburini sijui utasema sleep walking
Andaa mh. Kongamano hilo tuje kubadilishana utambuzi na maarifaAhsanteni sana jamani kwa kubadilishana mawazo. Haya ngoja wengine tuendelee na ratiba zingine, siku moja nitawaalika kwenye kongamano la mgongano wa fikra dhidi ya vikwazo vya maendeleo na ustawi wa jamii kwa jicho la ukatili utokanao na Imani potofu za kishirikina
π€£ππΎ Serikali haiamini uchawiπππππ Hicho kibubu kimetoboka panya wamebeba, njoo tukuazime chetu
Mkuu,Mkuu uchawi ni nini ?
Kwangu mimi kula rushwa, kuiba mali za watu, uongo uzandiki, kuchonganisha jamii kwamba bibi yako au shangazi yako ndio amekuroga, kutembea uchi kwenye nyumba za watu na kuchafua mazingira yao kufanya vitu visivyoeleweka (kwangu mimi huo ndio uchawi) na kuna sheria za kuweza kuwakabili hao watu sababu ni public nuisance na antisocial behavior
Sasa ukisema tuanze kuhukuma watu kwa definition yako ya uchawi sijui huyu ameingia kwangu ndio maana sipati mali au mtoto wangu kamuua au yule bibi mwenye macho mekundu ndio analeta mkosi mtaani tutaanza kuonea watu na ni hatari sana kwa wale watakaoonewa (persecution)