Katika jambo la ovyo na la aibu amefanya mwenyekiti wa CCM ni kumteua Makonda kuwa Katibu Mwenezi wa CCM

Chama chao, Makonda wao, Mlitaka amteuwe nani? Waacheni na mawowowo yao.
 
Ahsante kwa taarifa.

Akili kubwa huongelea maendeleo.

Akili za kawaida huongelea matukio.

Akili mbovu huongelea watu.
 

Wakati Mungu anataka kuwatoa wma Isralel Misri, alikuwa alimtuma Musa kwa Farao, akimwambia nitaufanya moyo wake Mgumu hatowaruhusu kitahisi. Mungu alifany hivyo ili amchape zaidi.

Wakati mwingine anguko likikaribia watu wanakuwa wakaidi, na ukiwa mkaidi unakosa Hekima na maamuzi sahihi, hapo ujue anguko lako limefika, Mama yenu ashaangula, ccm nayo so mda itaanguka.
 
Jana ilibidi nichokonoe masikio yangu niliponsikia Makonda akimpa waziri mkuu miezi sita awe ameshughulikia kero zote za ardhi! Haya ngoja tuone.
 
Mkuu acha mvua inyeshe ili tupaone panapovuja. Mamlaka ya uteuzi naona ilipima "strengs vs weaknesses" zake na hatimaye kujiridhisha anakidhi viwango vyote vya kuwa ni "asset" ndani ya chama kupitia nafasi aliyopewa.

Hayo mengine kuhusu kuwa ni "liability" kwa chama chake muda utaamua. Chama kimemuamini katika nafasi aliyokabidhiwa, natambua hatafanana kiutendaji na watangulizi wake katika nafasi hiyo.

"Acha mvua inyeshe tuone mahali panapovuja kupitia utendaji wake".
 
Makonda kaletwa sio kwa ajili ya wapinzani wa nje bali wa ndani ... yamkini hali si shwari, huenda kuna watu wananyemelea kiti cha mama yetu...
Mama Samiah kajiua kwa risasi yake mwenyewe. Anadhani anawakomoa CHADEMA kumbe anajikomoa mwenyewe. Baada ya CHADEMA kususia ule mkutano wa vyama mama akaona awakomoe CHADEMA kwa kumteua Makonda. Yetu macho
 
Ukute wananchi ndo wanapenda mambo hayo... ccm mbele kwa mbeleee
 
Amewekwa hapo kwa makusudi maalum ya kufanikisha ushindi wa ccm kwenye uchaguzi mkuu ujao na baada ya uchaguzi huo atapandishwa cheo kuwa katibu mkuu wa chama hicho. Mark my words!
 
Yeye ndio anataka kuzungumziwa. Sasa itabidi azungumziwe tu. Mtu anaongea pumba hadharani kwani msimzumzie?
Basi anapata anachokitaka kwamba anataka azungumziwe na kweli mnamzungumzia. Hata hivyo ndio aina ya siasa zetu hizo kujadili jadili matukio matukio ya mpito.
 
Lipi alilofanya ambalo sio la ovyo na aibu kwa Taifa?
 
Kumbe mazuzu tuko wengi nji hii?
 
Hatumii kodi za Wananchi bali anatumia pesa za CCM, halafu kama kwako wewe ni mtu mdogo unamuongelea wa nini kutwa kucha? Punguza hasira subiri zamu yenu Makonda awanyooshe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…