Katika Kukuza Lugha Yetu Adhimu ya Kiswahili Kimataifa, Mnaonaje Rais Samia, Atumie Kiswahili, Kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Leo nimetembelea kurasa fulani za website ya UN, nikakutana na neno fulani la Kiswahili kwenye moja ya program za UN, neno



Hii inaonyesha Kiswahili kinazidi ku gain momentum. Neno hilo linatumika kwenye program ya usajili ya UN. Niliwahi kuandika Usiyoyajua Kuhusu Samia UN: Kumbe alitaka kuhutubia Kiswahili! Baada ya Kiswahili kuwa Lugha ya Afrika, Rais Samia kukipaisha kuwa Lugha ya Dunia sasa mnaonaje kama tukimshauri Rais Samia, kwenye hotuba yake ya kuhutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA baadae mwaka huu, Rais Samia ahutubie kwa lugha ya Kiswahili, hivyo sio tuu atakuwa amekipaisha sana Kiswahili bali ataacha alama isiyofutika milele ya kuwa mtu wa kwanza kuhutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa lugha ya Kiswahili, hivyo jina lake kuingia kwenye historia ya UN milele kwa kuacha alama isiyofutika milele kimataifa.
Angalia Rais Samia akihutubia UN
View: https://www.youtube.com/live/F17SLI9LHA8?si=2aCTb9_9Qql9f_Qi amini nakuambia, kama angehutubia kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili, angekuwa more fluency no stammering na angetoa bonge la hotuba historic!.

Kwa sasa japo Kiswahili ni lugha ya Africa lakini huwezi amini, ni mataifa mengi makubwa yanayotangaza kwa lugha ya Kiswahili kuliko mataifa ya Africa.

Mfano kwenye Redio, Tanzania ndio nchi ya kwanza duniani kutangaza kwa lugha ya Kiswahili, Sauti ya Tanganyika, ile mwaka 1951, na watangazaji wa mwanzo wa Kiswahili wote walitoka RTD.

Angalia historia ya RTD
Hivyo ni watangazaji wa Tanzania ndio walianzisha idhaa za Kiswahili za redio zote duniani kuanzia
BBC Swahili,
VOA Swahili
DW Radio
RFI- France
NHK- Japan
Radio Moscow- Urusi
All India Radio - India
Radio China - China
Transvaal Radio- South Africa
Swiss International- Uswisi

Nchi za Afrika Radio ya pili ya Kiswahili ikawa Sauti ya Kenya na Sauti ya Zanzibar.

Sisi Tanzania, tumelala sana!, sasa Kenya ndio inaongoza kusambaza Kiswahili duniani kwa kufyatua watangazaji na waalimu wa Kiswahili duniani kote!.

Sasa hivi vyuo vikuu vingi vina mtaala wa Kiswahili, lakini sijui waalimu wa kutoka Tanzania ni wangapi!.

Nikiwa Geneva Uswisi nilishanga kukuta waalimu wa Kiswahili ni Wakenya na wana kiswahili kibovu ajabu!, huku Watanzania kibao wana Kiswahili safi, wanasugua lami vijiweni!.

Tanzania tunatakiwa kuamka, tukifanyie marketing Kiswahili kimataifa tukianzia na UN.

Hili la rais Samia kuhutubia UN kwa Kiswahili, liko ndani ya uwezo wetu, hatuna sababu ya kuendelea kukumbatia lugha za colonial legacy wakati tayari Africa tunayo lugha yetu ya Africa ambayo ni Kiswahili.

Hili mnalionaje wenzangu?.
Tena siku anakwenda kuhutubia UN kwa Kiswahili, atue New York na Airbus ya ATC na contingent kubwa ya waandishi wa habari wa Tanzania.

Mimi ndie mwandishi wa habari wa kwanza wa kujitegemea wa Tanzania kuripoti UNGA, marais wa nchi za wenzetu, japo wanaweza kuzungumza zile lugha 6 official za UN, English, French, Spanish, Chinese, Greek na Arabic, ikikutikana wazungumzaji wa Kiswahili ni wengi zaidi, Kiswahili kitaingizwa kuwa lugha ya 7 ya UN.

Paskali
 
Wanabodi,
Leo nimetembelea kurasa fulani za website ya UN, nikakutana na neno fulani la Kiswahili kwenye moja ya program za UN , neno View attachment 2967628
Adress katiba mpya, Tume huru , sheria nzuri za uchaguzi, mgombea binafsi and the like. acha petty issues kama hizi za kugha...of what use with regard to promoting democracy in Tanzania

Msikilize aliyekwenda shule ya uandishi wa habari unaojitosheleza and analsis of issues thereof

View: https://youtu.be/EEcYjw7tiQQ
 
Mkuu P

Kuhutubia UN kwa kiswahili ni wazo lisilo na tija. UN wanatumia mashine kufasiri hivyo Mwarabu, Mhispania, Mchina au mkorea watapata habari ile ile bila kujali ni kiswahili kimetumika au kiingereza. Ni wazo hafifu

Julius Malema wa EFF S. Africa alisema, ''Kiswahili kiwe lugha ya Afrika si kwasababu kinaongewa na watu wengi lakini kimesambaa na tuna mahali pa kuanzia'' Melema alitoa mfano wa Ibo ya Nigeria inaweza kuwa na wazungumzaji wengi lakini Kiswahili tayari kina mataifa mengi yanayozungumza na kinasambaa.

Malema anasema ukichukua kiswahili na Lugha nyingine , kiswahili kina nafasi kwasababu kuna mataifa mengi tayari, kuna mahali pa kuanzia kuliko kuanza na lugha kama Zulu na kuitangaza ambapo nje ya S.Africa hakuna anayeijua.

Tatizo letu hatujui kuuza bidhaa zetu. Kama tulivyoshindwa katika utalii na kiswahili pia.
Kuna nchi wanahitaji Walimu wa Kiswahili. Badala ya kuifanya kama '' bidhaa'' akili zetu zimezama kununua V8 za DCc

Kiswahili tu kingeajiri watu wengi wenye kipato lakini ni bla blah kama kawaida yetu.

Hatuhitaji Rais azungumze UN tunahitaji mikakati ya kukisambaza kupitia Walimu tukitengeneza ajira
 
Wanabodi,
Leo nimetembelea kurasa fulani za website ya UN, nikakutana na neno fulani la Kiswahili kwenye moja ya program za UN , neno View attachment 2967628
Washauri wa SSH wanampotosha sana. Ana fursa kubwa sana ya kukitanza Kiswahili na akawa comfortable kwenye hotuba zake kulikoni matumizi ya English yanayomfanya aonekane hajui kuhutubia!
 
Mambo ya kiswahili tuwaachie akina Khadija Kopa, mashauzi, akina ZUCHU n.k kwani Kwa mipasho na blaablaa zingine lakini mambo serious ya kitaalam hukuti kiswahili hata huko maofisini wanakosema Kuna lugha 2 yaani English and Swahili utakuta maelekezo au barua yenye mambo mepesi ndo zinaandikwa kiswahili lakini yakianza mambo ya kitaalam hukuti kiswahili nenda kwenye mikataba ya kandarasi mbalimbali ni mwendo wa kimombo siyo kwamba hatuitaki lugha yetu la hasha ila Bado haijafikia viwango.
 
Ukisema mkongwe unaona kwa jicho la tatu haupingwi labda umegundua kitu!
Mkuu kipara kipya , ni kweli kwenye ushauri huu kuna jicho la tatu fulani hivi...

Kwa vile wengi wanaamini Rais Samia ndie anaendelea 2025, sisi wa jicho la tatu tunaona otherwise, hotuba yake ya mwaka huu kulihitubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, inaweza kuwa ndio ..., kwasababu mwaka 2025 kipindi cha UNGA watu watakuwa busy sana na kampeni, hivyo the time is now!, this year!.

Tena kuna kitu kizuri sana nimemshauri Rais Samia akifanye kabla ya 2025, Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
Lakini kwa vile mimi ni nobody, no one listen to me!, ila...

Naendelea tuu kushauri
P
 
Labda Kongo kule KIVU Mashariki

Congo Kiswahili kinaota chenyewe kama Uyogapori huko ndo muinvesti Initiative maana kina impact Kubwa sana
Mambo ya kina Chinuwa Achebe tuwaachie wao

Byzewei tarehe za KIKOKOTOO zimekaribia mvua zielekezwe huko...

Mashaka Masanelo Fungameza
 
Hilo linaweza lisikuze kiswahili, bali hotuba inaweza ikapuuzwa.
 
Mkuu Paskali endelea kuwashauri kwani ndicho kipaji Mungu alichokupa ushauri huwa wanauchukua na kuufanyia kazi kimya kimya nani atatokeza hadharani kukiri paskali alitushauri,ni sawa na mtoto hata akishauriwa na mzee wake hawezi kukiri kwa muda ule mpaka ipite muda au mzee aondoke ulimwenguni ndio anakuja kukiri mzee alinishauri ushari nikaufanyia kazi,hivyo usichoke tunakuaminia mzee karma soon majibu yatakuja!
 
Mayala P

Acha wakenya waendelee kipokonya rithi zetu mana pengine vyombo vimepuuza mlima wenyewe tulishapokonywa kimataifa ni wakikenya
 
Mkuu Retired , kwanza asante kwa ushauri, na mimi niwe kama huyo, ila sio kila kitu siasa!.

Pili sio lazima kila anachofanya fulani na wengine wote tufanye hicho hicho, watu tunatofautia uwezo, haiba na mitazamo, watu wa kupigania katiba mpya wapo na waipiganie, wa kukikuza Kiswahili, pia tupo na tukikuze!. Japo ni kweli lugha is petty issue compared to katiba mpya, ila ina umuhimu wake!.

Kwenye issues za katiba mpya, mimi nimejikita kuelimisha umma kuhusu katiba hii iliyopo.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=ds6cD7Jt4djkuvvUKaribu
P.
 
You are very collect! Ninaamini kabisa ingelikuwa kuna uhuru wa kuandika/uhuru wa habari ungelikuwa Mayalla wa zamani. Ulikuwa tegemeo la kupata habari za weledi mkubwa. sasa mejikita kwenye mambo ambayo watoto wako/wangu hayatawasaidia sana katika Tanzania isiyo na haki!

Najua ulikuwa vocal , intelectual vocal journalist, mpaka bunge likakutishia, from there on mayalla tuliyekuwa tumemzoea kwa weledi akatoweka
 
 
Rais Chisano ndio rais wa kwanza kuzungumzia kiswahili katika UNGA. Kurekebisha hiyo sententi yako kuwa Samia atakuwa wa kwanza kuzungumza kiswahili!
 
Rais Chisano ndio rais wa kwanza kuzungumzia kiswahili katika UNGA. Kurekebisha hiyo sententi yako kuwa Samia atakuwa wa kwanza kuzungumza kiswahili!
Duh...!, believe it or not, sikuwahi kulijua hili!.
Kumbe tumepigwa bao!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…