Katika Kukuza Lugha Yetu Adhimu ya Kiswahili Kimataifa, Mnaonaje Rais Samia, Atumie Kiswahili, Kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa?

Katika Kukuza Lugha Yetu Adhimu ya Kiswahili Kimataifa, Mnaonaje Rais Samia, Atumie Kiswahili, Kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa?

Wanabodi,
Leo nimetembelea kurasa fulani za website ya UN, nikakutana na neno fulani la Kiswahili kwenye moja ya program za UN , neno View attachment 2967628 hii inaonyesha Kiswahili kinazidi ku gain momentum. Neno hilo linatumika kwenye program ya usajili ya UN
Niliwahi kuandika Usiyoyajua Kuhusu Samia UN: Kumbe alitaka kuhutubia Kiswahili! Baada ya Kiswahili kuwa Lugha ya Afrika, Rais Samia kukipaisha kuwa Lugha ya Dunia sasa mnaonaje kama tukimshauri Rais Samia, kwenye hotuba yake ya kuhutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA baadae mwaka huu, Rais Samia ahutubie kwa lugha ya Kiswahili, hivyo sio tuu atakuwa amekipaisha sana Kiswahili bali ataacha alama isiyofutika milele ya kuwa mtu wa kwanza kuhutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa lugha ya Kiswahili, hivyo jina lake kuingia kwenye historia ya UN milele kwa kuacha alama isiyofutika milele kimataifa.
Angalia Rais Samia akihutubia UN
View: https://www.youtube.com/live/F17SLI9LHA8?si=2aCTb9_9Qql9f_Qi amini nakuambia, kama angehutubia kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili, angekuwa more fluency no stammering na angetoa bonge la hotuba historic!.

Kwa sasa japo Kiswahili ni lugha ya Africa lakini huwezi amini, ni mataifa mengi makubwa yanayotangaza kwa lugha ya Kiswahili kuliko mataifa ya Africa.

Mfano kwenye Redio, Tanzania ndio nchi ya kwanza duniani kutangaza kwa lugha ya Kiswahili, Sauti ya Tanganyika, ile mwaka 1951, na watangazaji wa mwanzo wa Kiswahili wote walitoka RTD.

Angalia historia ya RTD

Hivyo ni watangazaji wa Tanzania ndio walianzisha idhaa za Kiswahili za redio zote duniani kuanzia
BBC Swahili,
VOA Swahili
DW Radio
RFI- France
NHK- Japan
Radio Moscow- Urusi
All India Radio - India
Radio China - China
Transvaal Radio- South Africa
Swiss International- Uswisi

Nchi za Afrika Radio ya pili ya Kiswahili ikawa Sauti ya Kenya na Sauti ya Zanzibar.

Sisi Tanzania, tumelala sana!, sasa Kenya ndio inaongoza kusambaza Kiswahili duniani kwa kufyatua watangazaji na waalimu wa Kiswahili duniani kote!.

Sasa hivi vyuo vikuu vingi vina mtaala wa Kiswahili, lakini sijui waalimu wa kutoka Tanzania ni wangapi!.

Nikiwa Geneva Uswisi nilishanga kukuta waalimu wa Kiswahili ni Wakenya na wana kiswahili kibovu ajabu!, huku Watanzania kibao wana Kiswahili safi, wanasugua lami vijiweni!.

Tanzania tunatakiwa kuamka, tukifanyie marketing Kiswahili kimataifa tukianzia na UN.

Hili la rais Samia kuhutubia UN kwa Kiswahili, liko ndani ya uwezo wetu, hatuna sababu ya kuendelea kukumbatia lugha za colonial legacy wakati tayari Africa tunayo lugha yetu ya Africa ambayo ni Kiswahili.

Hili mnalionaje wenzangu?.
Tena siku anakwenda kuhutubia UN kwa Kiswahili, atue New York na Airbus ya ATC na contingent kubwa ya waandishi wa habari wa Tanzania.

Mimi ndie mwandishi wa habari wa kwanza wa kujitegemea wa Tanzania kuripoti UNGA, marais wa nchi za wenzetu, japo wanaweza kuzungumza zile lugha 6 official za UN, English, French, Spanish, Chinese, Greek na Arabic, ikikutikana wazungumzaji wa Kiswahili ni wengi zaidi, Kiswahili kitaingizwa kuwa lugha ya 7 ya UN.

Paskali

Kiswahili ni lugha ya hovyo sana na ndio maana watz wengi ni WA hovyo pia!
 
Kiswahili ni muongoni mwa lugha zenye hadhi kubwa hapa duniani, hivyo tutumie lugha yetu katika kuutangaza utamaduni wetu Watanzania.
 
Back
Top Bottom