Hilo nakubaliana na wewe. Ni kwamba kura ya azimio la Umoja wa mataifa ilipigwa kuishutumu Israel kuvamia Palestine, na nchi nyingi ziliunga mkono. Lakini USA Israel nk walipinga. Na pia kama nilivyosema kura ya UN ilipigwa kupinga USA kuvamia Libya, kura ilipigwa kupinga Morocco kuitawala Sahara, nk.
Sasa suala hapa sio kwamba mataifa yakipinga kwa wingi basi wavamizi wataacha. USA, Israel, Urusi wote wamekuwa na kiburi dhidi ya maazimio ya Umoja wa Mataifa yaliyopita kwa kura nyingi. Suala ni kwamba jambo tunajua Tanzania tukipinga uvamizi wa Urusi au USA haitafanya waache, lazima tuonyeshe kwamba hatukubaliani nao.
Ndio maana nimesema hapa sio suala la kuchagua upande, ni suala la kuonyesha kwamba sisi hatuko tayari kukubaliana na nchi yeyote duniani kukiuka haki za binadamu na kuheshimu mipaka ya nchi huru, awe Urusi, Russia, Israel hata Kenya
Sasa kuna watu wasiojitambua humu wanaona tukipinga Urusi wanachofanya tunaunga mkono USA. Tukipinga USA wanachofanya tunaunga mkono Urusi. Ndio maana nawaita wajinga wajinga wanaobisha bila kuelewa siasa za kimataifa.