Katika suala zima la ndoa, dini ya Kiislamu ipo vizuri

Hata mm kuliko nioe kanisani bora niende bomani yan
Ndoa zote zinaidhinishwa na Serikali.
Maana yake anayefungisha ndoa ni Serikali.
Ndio maana ukitaka kuvunja ndoa ni lazima uende katika vyombo vya serikali kama Mahakama.

Na Serikali ikijiridhisha kuwa ndoa flani ilifungwa kwa kukiuka kanuni za ndoa, inaivunja hiyo ndoa bila kujali ilifungwa Kanisani au Hekaluni.

Huko Kanisani na Misikitini viongozi wake wanaiwakilisha tu kazi ya serikali.

Hata kiongozi wa Mila anaruhusiwa kwenda Serikarini na kuchukua vyeti vya ndoa na kuwafungisha watu wake, ili mradi tu aaminike na jamii yake na Serikali.

Kuhusu kuoa wake wengi au mmoja
hii inategemea na uwezo wa Mwanaume.

Taraka haipaswi kutolewa kwa urahisi kwakuwa Wanaume wasio na busara wanatumia fimbo ya Taraka kuwaumiza wanawake.

Wengi wetu uwezo wetu ni wakuoa mke mmoja tu.
Kama ilivyoandikwa kwenye Biblia Takatifu.
 
Nilitaka niseme neno la hovyo sana kwa waumini wa kiislam kuhusiana na ndoa na talaka, ila acha nibakize akiba ya maneno.
Sema unachotaka kusema itakuwa hujui usemalo.
 
sijaandika ndoa uji dada/kaka soma tena
 
Na je mume akipata matatizo mke aende wapi?? Dini ya kiislamu imewaweka wanawake chini sana
Ustahamilivu wa mke kwenye masuala ya kujamiiana Sio sawa na mwanamme hata siku moja.

Hata nguvu Za mwanamme Sio sawa na za mwanamke.

Ndio maana hata wanyama (mf. Ng'ombe, dume moja hupandishiwa majike wengi ili kuzalisha)
 
Sema unachotaka kusema itakuwa hujui usemalo.
Sipendi nikukere, ila kiufupi tu ni kwamba sipendi kuona mwanamke ananyanyaswa, kudharauliwa, kudhalilishwa, wala kuonekana kwamba yeye si wa maana na kutumiwa kama chombo cha starehe kwa kurundikwa ndani na mwanamme ikali hana uwezo wa kuwahudumia.
 
Wallah mie sijawahi kuona
 
Reactions: Tui
Naunga mkono hoja 100% upo sahihi mkuu...
Hakuna kufa na kuzikana hapa [emoji1]
 
Unaonaje? Na wanawake wangeruhusiwa kuolewa na wanaume wanne kama ilivyo kwa wanaume kuoa wanne naona hapa kama imeegemea upande mmoja mkuu.. maana kwa maisha ya sasa wanawake wana uwezo wa kufanya kazi na kupata pesa pia na wana uwezo wa kumudu wanaume wengi pia.. unalionaje? Hili mkuu na kama haiwezekani kwanini?
 
...haiwezekani mke wangu nimfumanie ugoni halafu niambiwe kitatutenganisha kifo huo ni uongo.
Huwezi kuacha kwa sababu ndogo ndogo kama dharau, ugomvi, nk..
Ila kwa habari ya uzinifu (pekee), kuachana kunaruhusiwa:

Mathayo 5:32
Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.

Mathayo 19:9
..Basi nawaambieni, yeyote atakayemwacha mke wake isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, akaoa mke mwingine, anazini.”

Maana ya hiyo mistari ni kuwa kama mke akithibitika kuwa mzinzi, kumuacha ni ruksa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…