Katika suala zima la ndoa, dini ya Kiislamu ipo vizuri

Katika suala zima la ndoa, dini ya Kiislamu ipo vizuri

Unaonaje? Na wanawake wangeruhusiwa kuolewa na wanaume wanne kama ilivyo kwa wanaume kuoa wanne naona hapa kama imeegemea upande mmoja mkuu.. maana kwa maisha ya sasa wanawake wana uwezo wa kufanya kazi na kupata pesa pia na wana uwezo wa kumudu wanaume wengi pia.. unalionaje? Hili mkuu na kama haiwezekani kwanini?
Mwanamke kumtosheleza mume mmoja tu ni shughuli. Sasa hao wanne atawamudu vipi na kila mmoja anataka shoo kila siku?!!!
 
Mtt akizaliwa baba atakuwa nani?
 
Uislamu ni dini ya haki sio tu ndoa mambo mengi katika uislamu yametolewa ufumbuzi ila wachache katika watu ndio wataelewa.
Wale wanaojitoa mhanga na kujilipua mabomu na kusababisha vifo vya halaiki ndio haki yenyewe hiyo?
 
Mwanamke kumtosheleza mume mmoja tu ni shughuli. Sasa hao wanne atawamudu vipi na kila mmoja anataka shoo kila siku?!!!

Kwani anafanya nao wote wanne kwa wakati mmoja si tofauti tofauti.. anaweza vizuri tu kumudu sikuiz wanadanga na kila baada ya masaa matatu analala na mwanaume hawezi shindwa kuwamudu MKUU
 
Mtt akizaliwa baba atakuwa nani?

Hiyo ni kazi ya kuhesabu siku zake tu mbona rahisi sana hiyo.. wewe hauijui hiyo .. mwanamke hata alale na wanaume mia kwa mwezi.. ujauzito ukiingia atajua wa nan! Hilo usiwe na hofu nalo
 
Hiyo ni kazi ya kuhesabu siku zake tu mbona rahisi sana hiyo.. wewe hauijui hiyo .. mwanamke hata alale na wanaume mia kwa mwezi.. ujauzito ukiingia atajua wa nan! Hilo usiwe na hofu nalo
Ndo mna mnaharibikiwa nyinyi kwa kutanguliza matamanio ynu mbele we umeona wapi imefanyika
Uislamu umeweka kila kitu kwenye stahiki yke sasa ww unavosema ivo yni ata akili ya mtoto wa la kwanza haiingii

Sisi tunafuata maandiko yanasemaje sio Matamanio yetu
 
Mwanaume hawezi kuwa na mke mmoja ni unafki tu unaoa mke mmoja halafu unachepuka

Huku unaoa wanne maumbo tofauti wanavutia unatokaje nje sasa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
hao waliooa wanne ndio wanaongoza kuchepuka kwa mwamvuli wa mke! Ndo maana mikoa yote yenye uislam inaongoza kwa wanawake malaya na waasherati! Eg singida.
 
hao waliooa wanne ndio wanaongoza kuchepuka kwa mwamvuli wa mke! Ndo maana mikoa yote yenye uislam inaongoza kwa wanawake malaya na waasherati! Eg singida.
Wanyaturu wamekufanyaje mkuu ,

Kwahyo wa Mbulu ni waislamu ? Maana kule babati we unavuta tu hawajaumbiwa hapana

Achana na hizo assumption zako

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ndo mna mnaharibikiwa nyinyi kwa kutanguliza matamanio ynu mbele we umeona wapi imefanyika
Uislamu umeweka kila kitu kwenye stahiki yke sasa ww unavosema ivo yni ata akili ya mtoto wa la kwanza haiingii

Sisi tunafuata maandiko yanasemaje sio Matamanio yetu

Mnasingizia maandiko ni swala la kujadili mkuu.. huo utamaduni wa watu ( waarabu) haiwezekani kwa mwanaume iwe sawa kwa mwanamke isiwe sawa sio haki mkuu
 
Nzuri zaidi ni ile "mke uji"
Hata kama hujaandika ndoa uji .Kilichokuwa kinajadiliwa ni ndoa. So hakuna hicho ulichoandika mke uji.Kuna wazinzi wana justify uzinzi wao na ku label majina yasiyokuwepo kwenye sheria na taratibu za kisheria za kiislamu.Mada ni ndoa za kiislamu kama umesahau.
 
Mnasingizia maandiko ni swala la kujadili mkuu.. huo utamaduni wa watu ( waarabu) haiwezekani kwa mwanaume iwe sawa kwa mwanamke isiwe sawa sio haki mkuu
Nikuulize swali.Assume kwamba mtu ana wake wanne.Wakipata mimba baba atakuwa anajulikana.Mwanamke akiwa na wanaume wanne akipata mimba baba anakuwa nani katika hao wanne?
Usawa wa kijinsia sio kwenye kila jambo.
Utamaduni wa kiarabu?Wamasai,wakurya ,na makabila karibu yote ya kibantu wana asili ya kuoa wanawake zaidi ya mmoja.
 
Hata hao wanaoruhusiwa kuoa wake wengi wanajikuta wameishia kuoa mmoja ni wachache Sanaa yaani wachache Sanaa walioweza kuoa wake wanne.
 
Nawasalimu kwa jina la jamuhuri

Binafsi nimekuwa mfuatiliaji mkubwa sana hasa wa maswala haya yahusuyo ndoa lakini kwa upande wangu nimeona ndoa kwa mujibu wa dini ya kiislamu wapo vizuri sana hasa katika swala zima la:-

1)Ndoa kwa ujumla
2)Talaka

NDOA KWA UJUMLA
-Hapa napenda kuzungumzia swala zima la kuoa mke zaidi ya mmoja ama kwa hakika hii kitu ni nzuri sana.

Maana licha ya kwamba tamaa ipo kwa mtu mwenyewe lakini pia kuoa mke zaidi ya mmoja inasaidia kupunguza swala zima la michepuko.

Pia ukipata wake wazuri kwa kushirikiana nao kwa pamoja unaweza kufika mbali hasa katika swala zima la maendeleo

Lakini changamoto kubwa iliyopo hapa pindi mume anapofariki watoto kuanza kugombania mali hivyo naamini nyie ni mashuhuda kwa baadhi ya familia.

TALAKA
Sasa hapa kwenye talaka ndio wamepatia kabisa yani haiwezekani mke wangu nimfumanie ugoni halafu niambiwe kitatutenganisha kifo huo ni uongo.

Haiwezekani mke awe na tabia zisizofaa ikiwemo kudharau ndugu zangu halafu niendelee kumkumbatia kisa kifo ndio kitatutenganisha.

Kama mke kakosea umemuadhibu mara mbili ya tatu bado anafanya kosa lile lile talaka ndio halali yake.

Hii sheria ya kwamba kifo kitutenganishe imewaponza watu wengi sana hadi kupelekea wengine kuona ndoa zao ni chungu na kukimbilia kutafuta tulizo nje kisiri (mchepuko) maana wanaona maovu ya wenza wao lakini wanashindwa kuwapa talaka kwa kisingizio cha hadi kifo kitutenganishe.

Kama wewe si muislamu basi funga ndoa hata ya kiserikali lakini uweke kipengele cha kuongeza mke mwingine hapo hatokuwa na jeuri ya kuringa maana kwenye ndoa ya kiserikali hata talaka zipo.

Kwa kumalizia kwenye swala la kuoa mke zaidi ya mmoja waislamu mmeupiga mwingi sana

Kumbuka kuoa sio lazima pia ndoa ndoano

Naomba kuwasilisha
Vp naww ukifumaniwa?

Kuhusiana na wake wengi ni TAMAA TU......
 
Back
Top Bottom