Uongo wa kwanza!
Katika Maidhwatain sura za kujilinda dhidi ya shari, Surat nnas aya inasema kuomba hifadhi kutoka Mungu; Alladhii yuwas wisu fi suduurinnas, minal jinnati wa nnas. Kwa maana unaomba hifadhi ya kujilinda kutoka kwa Mungu kutokana na wale ambao wanaotia wasiwasi katika nyoyo za binadamu ambao miongoni mwao ni binadamu na majini.
Na katika surat jinni kuna aya inaelezea madai unayoyatoa kuwa ni ushirikina na aya nilishakuwekea hapo awali. Hivyo usitunge mambo.
Jini hawezi kukuacha salama. Kila binadamu anayezaliwa kuna jini anamzingira huyu binadamu maisha yake kila mahali, na ndiye huyu usipoomba hifadhi kwa Mungu anafahamu siri zako zote. Ndiye huyu anayewasiliana na majini wa mganga, unafika kwa mganga anajua siri zako zote. Jua ya kwamba majini wa mganga wanazungumza kupata habari kwa huyu jini anayekuzingira muda wote. Anaitwa Qaarin. Tangu utoto kuzaliwa anakuzingira huyu. Sasa usichanganye mafaili kwa ufahamu hafifu na kuzushia unayoyataka wewe.
Ukiamua unalindwa na malaika, ukiamua unalindwa na mkuu wa malaika Jibril amani ya Mungu iwe juu yake. Na ukiamua unalindwa na Mungu.
Kuna malaika wanaitwa Ruhaniyyun. Hawa ni malaika wa rehma. Ukiwa unafanya dhikri sana muda wote unakuwa nao. Dua zetu zote ni kujikabidhisha kwa Mungu. Ikiwa kama unadua inayosapoti madai yako iweke hapa tuuuone ukweli wako!
13. Na lau tungelitaka tungempa kila mtu uwongofu wake. Lakini imekwisha kuwa kauli iliyotoka kwangu : Kwa yakini nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa, majini na watu.
Hiyo ni Surat Assajidah
_________________
Hii ni Surat jinni
6. Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.
Hiyo ni Qur'an na ndivyo inavyosema! Sasa huo uislam unaouzungumzia wewe sijui wa wapi? Wewe endelea kuneng'eneka na majini, jehannamu itajazwa wewe na majini.
Jini ni jamii miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa na Mungu kama jamii ya viumbe mbalimbali vilivyoumbwa. Jamiii imekusanya jumla ya jumia mojamoja. Kwenye jamii wapo miongoni mwa waliyo wazuri na kinyume chake. Na ndivyo ilivyokwa majini pia. Wapo waliyojisalimisha kwa Mungu na wapo waliyomkanusha Mungu. Akiwa anafanya ibada kuna tatizo gani? Tunu ya kumuabudu Mungu hujapewa wewe binadamu peke yako, tunu hii Mungu kaieneza kwa viumbe vyake wengineo pia. Hii ni tafsiri ya kwetu kwenye uislam, usiifananishe iwe sawa na yako.
Hapa ndipo unapoonesha ajabu yako!
Wapi ulishaona jini anakula chapati maji au tambi? We wapi ulishaona jini anakunywa uji? Naye anakunja chapati anachovya kwenye mchuzi?! Kila kiumbe kimepatiwa aina yake ya chakula cha kula.
Kwa imani yetu Malaika kaumbwa na nuru, jini kwa moto na binadamu kwa udongo. Ni aina 3 ya viumbe tofauti. Viumbe ambavyo vinatahiniwa na Mungu ni viwili, ni binadamu na majini. Kwa imani yetu malaika hamuasi Mungu hata mara moja. Kwa imani yetu Ibilisi hakuwa malaika bali ni jini. Wapo waliyojisalimisha kwa Mungu na wapo wanaoleta ukaidi kwa Mungu kama binadamu tu. Kwa namna hiyo usilazimishe tufanane.
Laa ikraha fi ddiin.
Uzuri wa uislam kinachofuatwa ni dalili. Uislam si dini ya mtu mmoja mmoja. Dini yetu elimu yake ipo wazi haikufungwa. Wapo watu wana elimu kubwa kuliko masheikh unaowasikia. Kwetu ile ni dhamana mtu aliyepewa aishike. Ila haimaanishi ana elimu kubwa kuliko wengine, la hasha! Mifumo yetu haipo hivyo! Hata hao waliyopewa dhamana wanafahamu hayo pia.
Sharifu majini kajipa lakabu ya namna hiyo si kwa tafsiri unayotaka kuiaminisha wewe kwenye umma wa Jf. Kama unavyoona baadhi ya wachungaji wanavyotoa mapepo, kwa muktadha huo kwa sababu naye ni kazi yake akajipa lakabu ya namna hiyo ya kuwa yeye anawatoa watu majini/mapepo yanayowaingilia watu ambapo kwa upande wa kiislamu jini akimdhuru binadamu anakuwa amemuasi Mungu na anakuwa ni sheytwani, binadamu naye akimuasi Mungu kwa mwenendo wa namna hiyo naye anaitwa sheytwani. Kwa elimu hii kwetu kuna sheytwani wa kijini na wa kibinadamu. Kwa usuli huo kwa sababu ndiyo kazi aliyofungamana nayo akaamua kujiita sharifu majini. Yaani yeye ni kiboko wa kuyaondoa majini mashetani yanayowadhuru watu.
Uongo mwengine huu!
Niliyoyaelezea juu yanajitosheleza kujibu hili. Na uongo ni uongo na uongo ni dhambi. Yaani haipindishwi, hata uufanye uongo kwa mtu aaswi kwa Mungu huo uongo unaandikwa umefanya uongo. Hivyo utaandikiwa dhambi ya kuwa muongo.
Unajitahidi kujibu ila bado unajichanganya.
1. Nikisema Waislamu na Majini wanaukaribu hata wa kuitana ndugu kwakuwa ndugu ya Mwislamu ni Mwislamu mwenzake.
Sasa hapo unakanusha nini wakati wote ni Waislamu?
Yaani Mtu na Jinni Waislamu si wana namna moja ya kuabudu ? Yaani ni Dini moja.
2. Mashehe au Viongozi wa Kiislamu wanaposomea uislamu ni lazima wanafika mahali wawasome Waislamu wenzao wa Kijini.
Yaani somo la
" Mahusiano ya Waislamu watu na Waislamu Majini"
Somo hili linawapelekea hadi kwenda Ujinini ili kujua Lugha, tamaduni, na elimu za Kijini. (Baadhi ya Mashehe wanalizungumza hili)
Kwa mfano Jini Mwislamu anakuja kusali Msikitini lazima kuna taratibu inabidi zifuate ili kumwekea mazingira yake.
Ndio maana Wanawake wakiwa kwenye siku zao wanakatazwa kuingia Msikitini kuswali kwakuwa Majini yanaweza kumyonya zile damu ikapelekea hata kifo chake.
Pili Mnaposwali Msikitini Mnasalimia kushoto na Kulia, ukweli hapo mnawasalimia Majini.
Kwa hiyo hizo ratibu lazima viongozi wa Kiislamu wazitambue kwa kusoma Elimu ya Majini.
3. Umesema Mungu aliwaumba Majini ili wamwabudu.
Je Kabra ya Muhammadi Majini yalikuwa yanamwabudu nani ?
Yalikuwa Dini gani ?
Maana Manabii wote hawakufanya Shirika na Majini katika Ibada zao wala hawakuwahi kuwahubiria Majini habari za Dini.
Na Hakuna Mahali ambapo Mungu aliagiza Manabii wake wawashirikishe majini katika ibada zao.
Muhammadi ndiye nabii wa kwanza kwenda Ujinini kuwahubiria Majini Uislamu na Majini yakaukubali na Kusilimu.
Nani alimpa ruksa hiyo na wapi ?
Je kabla ya Kusilimu ni kwanini Majini hayakuwa yakimwabudu Mungu hali ya kuwa waliumbwa ili yamwabudu ?
Unataka kusema Majini yaliumbwa na ikawabidi wamsubiri Muhammadi aletewe Uislamu ndio yasilimu na kunwabudu Allah ?
4. Unaposema Kuna Majini wema na wabaya mimi nashindwa kukuelewa.
Hapo unamaanisha hawafanyi dhambi kabisa au ?
Maana Waislamu watu wanatenda dhambi na wanatubu Msikitini.
Na Majini pia najua yanakosea na yanakuja kutubu Msikitini.
Wewe unasemaje kwamba kuna Majini mema ?
[emoji117]Mwema ni Mungu peke yake yeye pekee ndiye hatendi dhambi[emoji118]
Kusema kuna Majini mema ni juhudi za Waislamu kuwatetea ndugu zao wa Kijini.
Kama kuna Majini mema yanakuja kufanya nini Msikitini ?
Unamaanisha hayatendi dhambi au unamaanishaje ?
Yaani Jinni Mwema na ahitaji kusilimu ili iwe nini?
Ninachojua majini yote ni maovu ndio maana yanatapatapa kutaka kutubu.
Halafu Kusema Mtu au Jinni ni Mwema hii kauli haitakiwi isemwe na Jinni wala Mtu.
Mungu ndiye anayejua kiumbe gani ni Chema baada ya kutubu na kuishi kitakatifu.
Ni kwamba Majini yameukubali uislamu kwakuwa yanataka kutubu dhambi zao uli kumpendeza Mola wao.
Na Majini Maovu ndiyo yanayotaka kutubu kupitia taratibu za Kiislamu.
5. Hivi ni kwanini Ibada za Kiislamu zishirikishe Majini?
Hivi Allah alishindwaje kuchagua Mtume wa Kijini ili awahuburie Majini wenzake ?
Inayumnikanaje Mtume wa Watu aende kuyahubiria Majini wakati Majini hayaonekani kwa Macho ya Kibinadamu.?
Alikukutana nayo vipi na wapi mbona qurani haielezi. Muhammadi alijifunza wapi Lugha za Kijini.
Muhammadi tunaona Allah anamtuma kwa Watu awe Mtume.
Mbona hatuoni Allah anamtuma Muhammadi kwenda kuwa Mtume kwa Majini ?
Hivi Allah kama alitaka Majini yamwabudu kupitia Uislamu kwanini hakumteua Mtume miongoni mwa Majini awahubirie Majini wenzake ?
Kama Binadamu Muhammadi ndiye aliyeyasilimisha Majini.
Basi ni wazi hata leo Majini yanasikiliza Ibada kwa Binadamu Mashehe na Maimamu.
Ndio maana yule Shehe aliniambia Majini yote yanaswali Kwenye Misikiti ya Watu.
Kama Majini yalikosa Nabii wao wa Kijini, basi ni hakika hayana Mashehe wala Maimamu wa Kijini.
Wa kuwaswalisha huko huko Ujinini.
Hivyo ni lazima Majini yashiriki katika Ibada zote za Kiislamu zinazo ongozwa na Waislamu watu Misikitini.
Hii ni hatari sana kwa baadhi ya Waislamu Watu hasa wengi wao ambao ni Maamuma kwenye Kweli ya Kiislamu