We Kafiri Hii Hapa Mnafata Nani...?
Au sio Biblia hii Mchungaji Anaitumia kubariki Ndoa ya Mashoga..
View attachment 2121224
JE UKRISTO NI USHOGA NA BIBLIA INASEMAJE KUHUSU USHOGA.
Mwanzo nitangulie kwa kusema nimesoma vitabu vingi sana ila sijawahi kuona kitabu kinachopinga ushoga kama Biblia
na kwa sababu biblia ndio kweli juu ya yote na haijaacha kitu hicho kimeshasemwa tayari na kikapingwa kwa nguvu zote .
“Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.”
— Mambo ya Walawi 20:13 (Biblia Takatifu)
“na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;”
— 1 Timotheo 1:10 (Biblia Takatifu)
“Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,”
— 1 Wakorintho 6:9 (Biblia Takatifu)
Warumi 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁶ Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
²⁷ wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.
²⁸ Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Lakini kwanini watu wanafanya hii inatokana na tamaa zao binafsi na Mungu amewaacha ili siku moja makazi yao yawe kule kwenye ziwa liwakalo moto usiku na mchana
“Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”
— Ufunuo wa Yohana 21:8 (Biblia Takatifu)
Mbarikiwe