Na elimu ya kutosha kuhusu hili. Ipo hivi na ieleweke ya kwamba. Waafrika wako masikini sababu maisha yao yapo connected na mizimu, na mizimu haitaki maendeleo thus ukijenga nyumba kijijini unalogwa ukiaga unalogwa, ukisoma haufaulu,ukilima ufanikiwi,nk. Ni hadi uwe maarifa ya kucut off ile connection ndipo utoboe.Talielezea ili jinsi nguvu ya mizimu inavyozuia mtu kufanikiwa.
Alietuletea hizi dini ndio kaleta huu mkanganiyiko
Unadhani mizimu ipo Africa tu Peke yake mkuu? Unajua lakini maana ya mizimu?
Unajua kama kuna mataifa mengine ambayo yenyewe ibada zao zimeelekezwa kwenye mizimu tu na sio Mungu wala vitu vingine kama sie?
Ukisema waafrica wengi wako connected na mizimu ndomana wengi Maskini unaweza nitajia taifa ambalo lenyewe halipo connected na mizimu ndomana wao ni matajiri?
Unajua kama China au karibia nchi zote za Asia ibada zao ni mizimu,ukarimu,upendo na hawataki kuskia habari za Mungu mingine tofauti na mizimu Yao na maisha yanaenda
Unajua kama hawa waliotuletea hizi dini waga kuna muda wanafanya matambiko kwa ajili ya kutimiza mahitaji ya mizimu yao? Wao wanaanimi kama mizimu ikikasirika basi ndo unapata majanga na Mambo yako hayataenda Sawa sawa
ila kama utafanya jambo mizimu yako ikafurahi basi utafanikiwa kwenye Mambo yako the same thing walichokuwa wanafanya wazee wetu miaka kibao nyuma kabla ya kuletewa hizi dini za kigeni
Na wapo watu kibao ambao ni Christian ila hawajaacha utamaduni wa kwenda kuwaenzi wazee wao ambao ni mizimu Kwa sasa Kwa kufanya matambiko kama Mila zao zinavosma ili tu katika familia zao mambo yaende vizuri mfano wachaga na wakinga
Sasa nyie mmekazana kusema mara cut off mizimu mara kukata sijui nini ilhali ni ujinga mtupu, kufanikiwa kwa mtu kunakuja na Mambo mengi ila baadhi ya hayo ni pamoja na kujitambua,kujua unataka nini,kuamini katika unachokifanya,kujituma,nidhamu ya kazi, upendo na mwisho kabisa connection
Haijarishi huyo mtu atakuwa ni Christian/Muslim/pagan/Buddha/Hindu/ akifata hiyo misingi basi ni Jambo la Muda tu kufanikiwa kulingana na sehemu alipo na juhudi zake
Dini ya kweli hapa Duniani ni UPENDO tu, haya mengine ni utashi wetu binadamu tu na yanaleta kujigawa na kujiona wengine ni Bora kuliko wengine ila hayana faida yoyote katika jamii zetu na hasa sie ambao ujinga ni sehemu ya maisha yetu
kutwa kumsingizia Mungu mambo ambayo ata yeye anashangaa ohooo Dini ya kweli sasa ingekuwa Dini ya kweli si tungezaliwa kila binadamu teyari anaijua na kuifata sasa iweje kuwe na Dini ya kweli alafu duniani kuwe na Dini zingine zaidi ya 3000 Zingine
Yani dini mpya kuliko zote duniani ndio ije kuwa Dini ya Kweli na Dini zilizoanza maelfu ya miaka huko nyuma zenyewe ziwe za uongo, Mambo mengine bana ukifikilia unaishia kucheka tu
Ohhh kwa yesu ndio kuna mafanikio na uzima wa milele unataka kuishi milele ili ugundue nini? Ohhho Kuna mafanikio, mafanikio gani hayo ya kujazana ujinga na kutajirisha wanaojiita manabii na nyie kubakia Maskini wa kutupwa
Mchungaji/Nabii akitaka Gari mnamchangia pesa akanunue ila muumini akitaka Gari anaombewa na mchungaji, yani Akili zenu mnazijua wenyewe, sasa kama maombi yanaleta Gari/ mafanikio iweje mchungaji achangiwe pesa na sio kuombewa apate Gari?