Katika utawala wake, hayati Magufuli hakwenda New York kuhutubia UNGA, je tulirudi nyuma kiuchumi na kisiasa?

Katika utawala wake, hayati Magufuli hakwenda New York kuhutubia UNGA, je tulirudi nyuma kiuchumi na kisiasa?

Kama unammisi sana dikteta twende tukakufukie kwenye kaburi lake msituchoshe.

Zama za kishamba zimekwisha lazima mlikubali hili na hii nchi hatuwezi kurudia kosa kuwakabidhi washamba.

wewe jamaa huwa ni tafsiri ya mtu mrefu mjinga.

sina uhakika kama ni mrefu lakini.
 
Compare and contrast.

Oooh!

Comparison
1. Both are/(has been) head of State.
2. Both are CCM cadres.

Contrast.
1. One was believer of austerity measures as mode of economy while other is not believer of such.
2. One favoured his home while the other is not.
3. One is Male while the other is Female.
4. One lacked diction of words (can speak anything didn't care) while the other choose what to say.
5. One didn't prefer regional and the rest of world integration while the other believe in diplomatic ways.
6. One liked to be praised the other prefer to work and let people judge.
7. One was jack of all trades the other prefers to listen and be adviced on different matters.

etc.....
#Mama 2025
 
Not nécessarly, ile kutoka tuu na kutembea, unapata kitu kinachoitwa exposure, kukutana na kubadilishana mawazo na wengine kuna ku broaden your perspective, you won't ne the same, think the same, you will think differently...
Exposure si tija. Yule aliyritwa mtalii alituacha wapi vile? Ukitoka na kuambulia vyandarua wakati madini na gesi vinayoyoma then exposure imemsaidiaje mndengeleko wa kipatimu?

Usipotoka na korona ikakosa nguvu ya kutesa jamii si heri hiyo kuliko utoke kwsvile wengine wanatoka? Kama mtu hatoki na anajenga bwawa la umeme bila tozo si tija hiyo?

Mwacheni JPM apumzike kwa amani nyie fanyeni yenu tu. Marehemu hawezi kywa kipimo cha ufanisi wetu tulio hai. Viatu vyake hamviwezi hata kuviweka mguuni, achilia mbali kupwaya au la.
 
mama ana wakati mgumu sana mwanamke yeyote katika jamii,kujaribu kumfurahisha wifi yake mwenye gubu.

wakati the late JPM anafanya haya,kuna kelele zilipigwa sana kwamba anaharibu mahusiano ya kimataifa,leo hii wale wale wanamsuta kwamba kaonekana kituko,hata kupokelewa imeshindikana maana ni mfano mbaya kwenye democrasia[emoji16][emoji16][emoji16].

ama kweli jpm alijua kuwanyoosha wazee wa kelele.
bimkubwa pambana,tulikuonya.
 
Miaka mitano yote akiwa madarakani tuliwakilishwa na mawaziri wa nje. Na hakuna mtanzania aliyeona labda tumepungukiwa kiuchumi. Zaidi ya kuona maendeleo kwenye sekta za afya, miundo mbinu na ukusanyaji mapato...
What do you mean? Una maana waliokwenda huko kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Jakaya walifanya makosa? Ina maana unaona Mama Samia kakosea kwenda UN kuhutubia pamoja na kukutana na viongozi mbali mbali? Wakati mwingine tuache kutumia vibaya uhuru wa kutoa maoni
 
Miaka mitano yote akiwa madarakani tuliwakilishwa na mawaziri wa nje. Na hakuna mtanzania aliyeona labda tumepungukiwa kiuchumi. Zaidi ya kuona maendeleo kwenye sekta za afya, miundo mbinu na ukusanyaji mapato.

Safari hii tumewakilishwa na mkuu wa nchi. Je, ndio kusema taasisi kubwa kama Imf, Wb na taasisi Tanzu za UN zitaisadia Tanzania na kupaaa kiuchumi? Je haya madhila ya kukosa ajira, kukosa madarasa, kukosa maji na uvunjifu wa haki za binadamu vitaisha?
Umbumbu tu! Nimemuuuliza Pascal huko kwanini aamini Tanzania itapaa zaidi kuliko mataifa yote yaliyofika pale? Kimsingi hakuna la maana zile ni siasa tu kukamllisha protocol lakini ata akienda waziri wako kukuwakilisha hakuna unachopoteza.
 
Not nécessarly, ile kutoka tuu na kutembea, unapata kitu kinachoitwa exposure, kukutana na kubadilishana mawazo na wengine kuna ku broaden your perspective, you won't ne the same, think the same, you will think differently.
Tena unaweza usiamini, akikutana na taasisi za human right wings, akirejea tuu, mara pap... DPP anapeleka Nolle na kumaliza hizi kelele !.
Wajameni, haya sasa ndio mambo haya...
Kuna vitu watu tulisema, japo tulibezwa sasa vinatokea na vinajidhihirisha.
Hapa nilisema kitu kuhusu Tanzania ya Samia compared na Tanzania ile, kiukweli kabisa, Tanzania tunakwenda kuwa na Tanzania bora, Tanzania njema na Tanzania nzuri kuliko Tanzania ile, kitu kinachohitajika sasa ni kumpa muda.

Hongera sana Mama Samia, una uwezo na unaweza kututoa hapa tulipo na kutufikisha kule tunapaswa kuwa.

P
Sidhani kama kwenda UN ni kupiga hatua. Au kuwa na hyo exposure unayoisema. Si mara ya kwanza Tanzania kuhudhuria hivyo vikao. Toka Nyerere, Mwinyi, Mkapa, na Kikwete. Tena Kikwete aliizunguka dunia nzima.

Magufuli kwenda UN hakuwahi hata siku moja. Lakini aliifanya Tanzania kuwa ya kisasa. Katika utawala wake Tanzania ilisikika kila mahala. Watu waliiongelea Tanzania kwa mafanikio ya kiuchumi. Nilishawahi kusema humu. Nchi fulani Ulaya walikuwa wakijadili Magufuli alivyo weza kuwa na miradi mikubwa ya kiuchumi.

Reli ya SGR,kufufua reli ya Moshi Arusha hadi Dar. Kujenga Bwawa la Nyerere, kufungua masoko ya madini, na kiwanda cha uchenjuaji. Kuhamishia Makao Dodoma, kufufua shirika la ndege ATCL, kuyawezesha mashirika ya Posta na Simu. kujenga hospitali na vituo vya afya muhimbili sasa ni moja ya hospitali zinazoaminika. Kujenga madaraja na barabara za kisasa. Ni mengi kutaja huyu mnae msema hakuwa na exposure, lakini kafanya haya yote ndani ya miaka 5.

Watanzania baadhi ni wanafiki, wamezoea kujipendekeza ili wapate vyeo au njia za kujipatia pesa. Magufuli aliziba mianya yote, waliotegemea vyeo hawakupata. Wakaanza kujenga chuki zisizo na maana. Ndo maana hadi leo wanachukia hadi marehemu, wanafurahi mtu kufa utadhani wao wataishi milele.

Mama Samia apewe muda msimpe sifa zisizo stahili. Make hadi sasa ni ngumu kujua tunaelekea wapi. Nini hasa vision ya kiongozi wetu. Anaeogopa kutatua kero za wananchi hadharani. Kutwa nzima ni safari. Kikwete alisafiri lkn hatukuwahi kuona exposure hiyo ikiletwa Tanzania. Nilishawahi kwenda nchi fulani, katika mji wao mmoja ni mji wa kawaida tu. Nikafika hotel moja, nikaambiwa Rais Kikwete alipenda kufikia pale kalala mara kadhaa. Nikajiuliza Rais wa nchi anazurura hadi kuwa mteja wa hotel.

Msiyo mpenda Magufuli mtazidi umia na kuangaika. Yeye amepumzika. Alifanya yake kwa Tanzania. Swala kujiuliza wewe hapo umeifanyia nini Tanzania? Je japo unaishi haki gani unaitenda kwa wananchi wengine na kwa nchi yako?

Mauaji na utekaji umekuwepo Tanzania vipindi vyote. Wakati wa Kikwete tulijionea wasio julikana wakimteka Ulimboka, waandishi wa habari wakiteswa na kuuwawa. Mwanasiasa Mkongwe wa NCCR Dr. Mvungi alilalamika anafatiliwa baadae alivamiwa na kukatwa mapanga hatimaye alipoteza maisha.

Leo tunajifanya mabaya yote ni ya Magufuli. Tuache uzandiki. Magufuli aliirejesha heshima ya Tanzania.
Hakuna nchi duniani iliendelea kwa Demokrasia never. Marekani yenyewe wanawake wameanza kupiga kura miaka ya 60 japo walipata uhuru wao toka karne ya 18. Nchi nyingi za Ulaya zimeongozwa kimabavu ndo maana zilifanikiwa.

Leo mnadanganyika na Demokrasia na Human Right.
China inademokrasia gani? Na human rights zipi? Nchi za arabuni, Dubai, Saudia na nyinginezo wapi demokrasia na human right, mbona zimeendelea kuliko sisi tunao thamini wazungu.

Rwanda leo inasonga mbele wapi Demokrasia na human rights? Ethiopia inakuwa kwa kasi haijawahi kuwa na demokrasia wala human rights zenu. Libya ilikuwa bila demokrasia. Walipotaka Demokrasia wamejikuta kubaya.

Nasema hatuhitaji kuiga kila tuletewacho na mzungu. Tuwe na demokrasia yetu model tofauti na wazungu. Tunatofauti kubwa za kitabia na mazingira na wao hatuhitaji kuiga kila kitu. Kama ni human right Marekani imeua watu wangapi huko mashariki ya kati? Ni watu wangapi uuwawa marekani kila siku?

Imeua viongozi wangapi kwa uongo wa demokrasia.
Watanzania tubadilike hasa wachache tusiyoitakia mema nchi yetu kisa chuki binafsi. Umieni tu Magufuli atabaki kuwa kiongozi wa aina yake. Alie paisha jina la Tanzania. Nikizunguka ulimwenguni uwa naulizwa nchi ya Nyerere, kingine Magufuli alikuwa kiongozi mleta maendeleo, utasikia vizuri havidumu. Hao ndo wanao ongelewa sana.
Nawapenda Haiti, walikuwa hawampendi Rais wao, waliandamana kumpinga hakuleta maendeleo, ila alipouwawa Haiti waliumia, walihudhunika. Walisema japo walimpinga lakini hakustaili kuuwawa.

Hawa watu wanaubinadamu. Siyo baadhi ya watanzania, ambao kufa wanadhani ni kwa watu fulani tu, wanashangilia. Nami nasema mfanyao hivyo nanyi mtakufa na hamjajiuliza mtakufa vifo vya namna gani.
Narudia kusema Mch. Mtikila! Nyerere alipo kufa alisheherekea. Leo yupo wapi? Je, kifo chake kilikuwaje? Japo tunapingana lkn tujifunze kuwa na utu. Pia tusidhani Mzungu ni kila kitu. Tunawaabudu sana. Na mzungu ukimshobokea anakusanifu. Wanapenda msimamo wa mtu.
 
Kama unammisi sana dikteta twende tukakufukie kwenye kaburi lake msituchoshe.

Zama za kishamba zimekwisha lazima mlikubali hili na hii nchi hatuwezi kurudia kosa kuwakabidhi washamba.
Sasa kati ya mshamba ba tapeli yupi ana afadhali! Mnachekelea nchi kurudi mikononi mwa matapeli
 
Kama mtu hatoki na anajenga bwawa la umeme bila tozo si tija hiyo?

Ni tija kama alikuwa hakwapui fedha za wafanyabiashara kwa nguvu kwenye task force zake na operation za bureau de change.

Na kuzuia kupanda kwa madaraja kwa wafanyakazi pamoja na nyongeza ya mshahara.
 
Exposure si tija. Yule aliyritwa mtalii alituacha wapi vile? Ukitoka na kuambulia vyandarua wakati madini na gesi vinayoyoma then exposure imemsaidiaje mndengeleko wa kipatimu? Usipotoka na korona ikakosa nguvu ya kutesa jamii si heri hiyo kuliko utoke kwsvile wengine wanatoka? Kama mtu hatoki na anajenga bwawa la umeme bila tozo si tija hiyo?
Mwacheni JPM apumzike kwa amani nyie fanyeni yenu tu. Marehemu hawezi kywa kipimo cha ufanisi wetu tulio hai. Viatu vyake hamviwezi hata kuviweka mguuni, achilia mbali kupwaya au la.
Umetoa good point.
 
Miaka mitano yote akiwa madarakani tuliwakilishwa na mawaziri wa nje. Na hakuna mtanzania aliyeona labda tumepungukiwa kiuchumi. Zaidi ya kuona maendeleo kwenye sekta za afya, miundo mbinu na ukusanyaji mapato.

Safari hii tumewakilishwa na mkuu wa nchi. Je, ndio kusema taasisi kubwa kama Imf, Wb na taasisi Tanzu za UN zitaisadia Tanzania na kupaaa kiuchumi? Je haya madhila ya kukosa ajira, kukosa madarasa, kukosa maji na uvunjifu wa haki za binadamu vitaisha?
Swali, je ajira na haki za binadamu zilikuwepo kipindi cha mwendakuzimu pamoja na kutoenda huko?
 
Not nécessarly, ile kutoka tuu na kutembea, unapata kitu kinachoitwa exposure, kukutana na kubadilishana mawazo na wengine kuna ku broaden your perspective, you won't ne the same, think the same, you will think differently.
Tena unaweza usiamini, akikutana na taasisi za human right wings, akirejea tuu, mara pap... DPP anapeleka Nolle na kumaliza hizi kelele !.
Wajameni, haya sasa ndio mambo haya...
Kuna vitu watu tulisema, japo tulibezwa sasa vinatokea na vinajidhihirisha.
Hapa nilisema kitu kuhusu Tanzania ya Samia compared na Tanzania ile, kiukweli kabisa, Tanzania tunakwenda kuwa na Tanzania bora, Tanzania njema na Tanzania nzuri kuliko Tanzania ile, kitu kinachohitajika sasa ni kumpa muda.

Hongera sana Mama Samia, una uwezo na unaweza kututoa hapa tulipo na kutufikisha kule tunapaswa kuwa.

P
Mayalla unataka kuniambia kuwa Magufuli hakuwa na exposure? Wasaidizi wake pia nao hawakuwa na Exposure? Nini maana ya kuwa na Balozi kama sio kutuexpose na mambo mbalimbali yanayoendelea huko ukizingatia uwepo wake wa muda mrefu katika mazingira hayo.

Safari ya siku tatu ndio ikuexpose kwenye mambo chungu nzima yanayoweza kulifaa taifa lako, like seriously! Raisi Kikwete alishinda ulaya na Amerika lakini bado hatukuwa hata robo ya hizo nchi kiuchumi, kielimu, kisiasa n.k.

Unataka kuniambia kweli kwamba Magufuli hakuwa na exposure ya dunia na yanayoendelea! Acha hizo mkuu, mama kaamua kudance na dunia, period.
 
Miaka mitano yote akiwa madarakani tuliwakilishwa na mawaziri wa nje. Na hakuna mtanzania aliyeona labda tumepungukiwa kiuchumi. Zaidi ya kuona maendeleo kwenye sekta za afya, miundo mbinu na ukusanyaji mapato.

Safari hii tumewakilishwa na mkuu wa nchi. Je, ndio kusema taasisi kubwa kama Imf, Wb na taasisi Tanzu za UN zitaisadia Tanzania na kupaaa kiuchumi? Je haya madhila ya kukosa ajira, kukosa madarasa, kukosa maji na uvunjifu wa haki za binadamu vitaisha?
Kule hawaruhusu kiswahili au kisukuma kuwasiliana, labda tatizo lilianziapo na kupelekea kutokwenda kule ,

Kuhusu faida au hasara ya kutokwenda tukuachie wewe mtoa mada udadavue
 
Back
Top Bottom