Hapana. Kipindi Nyerere anaongoza hali ya siasa duniani kote ilikuwa ni tofauti kabisa na sasa. Ukifananisha Nyerere na marais wengine wa kipindi hicho, Nyerere alikuwa rais bora kabisa. Hakuwa anaua watu na alikuwa na vision. Alipokuwa anaondoka alitoa tahadhari kuhusu katiba na mfomo mzima wa utawala na pia alisema vyama vingi haviepukiki. Haya yanayotokea sasa ni matokeo ya uzembe wetu wenyewe kushindwa kubadili katiba. Na Magufuli ndiye shetani hasa kwa sababu bunge bovu, mauaji na uporaji wa kura kwa kiwango unaofanywa sasa hivi yeye ndiye alianzisha.
Mkuu nakushauri fikiri tena kwa kina hilo neno kuhusu
"uzembe wetu wenyewe kushindwa kubadili katiba". Na sisi ni kina nani? Tuko pamoja katika hili?
Kwa taarifa yako tangu enzi za Nyerere wamekuwepo Watanzania majasiri wanaojaribu kugusa eneo la Katiba kwa namna mbalimbali lakini mwisho wao haukuwa mwema.
Katiba kwa kundi la watawala ndani ya chama tawala, ni eneo tukufu lilisogusika kabisa (
sacred text).
It is untouchable.
Touch at your own peril. Hakuna ambaye angeweza wala anayeweza kufanikisha
marekebisho ya msingi ya katiba ya nchi hii bila kusababisha machafuko na maafa makubwa nchini. Awamu zote. Hadi leo Watanzania hawako tayari kwa mapambano hayo na vyombo vya dola.
Kila kukicha AMANI inasisitizwa, inahubiriwa, inaombewa kitaifa kwenye nyumba za ibada. Wapinzani wanasoteshwa kwa kutishia amani ya taifa kwa kushirikiana na mabeberu. Wanatekwa, wanatiwa ulemavu, wanauawa, wanapotezwa. Kina Lissu wako ndani. Wenzao wengine wananunuliwa kila kukicha. Sijui kama kweli, kwa kadhia hizi, bado ni "
uzembe wetu wenyewe" kushindwa kubadili katiba.
Nyerere ndiye aliyekuwa na
nguvu ya kipekee,
uelewa mkubwa na
ujasiri wa kipekee wa kuitisha na kusimamia hayo marekebisho yanayotakiwa mara tulipoanza mfumo wa vyama vingi. Kama vile alivyofunga mjadala wa ama kuingia vyama vingi au kubaki na chama kimoja pamoja na wengi (80%) kutaka chama kimoja. Alipoacha
status quo, waliopokea madaraka walikuwa kama mafisi walioachiwa bucha nzima milango yote ikiwa wazi. Si rahisi wakakubali ifungwe. Ni mwendo wa kurithishana tu.
Btw, katiba zote za taifa hadi ya 1977 na marekebisho ya 1984 (yaliyoingiza haki za binadamu) wakati anang'atuka ziliandikwa na Nyerere mwenyewe kwa msaada wa vijana wake kina Warioba na wengineo. Na alijua vizuri sana hatari ya hiyo katiba (tuliyo nayo hadi leo). Lakini naona hakuwa na ujasiri wa kushuhudia CCM ikiondolewa madarakani akiwa hai. Kuuawa kwa Azimio la Arusha na tishio la Muungano kuuawa na wale G55 vilimkosesha raha sana.
Muungwana Kikwete alijaribu kuachia mwanya kidogo tu akatishiwa kuondolewa madarakani akituhumiwa kutaka chama kimfie mikononi. Unaelewa msimamo wa Magufuli na wa utawala wa sasa
. Not an easy task at all.