Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 42,525
- 74,605
Mimi sijasema ni jiwe, wewe wasemaUnadhani huyo Jiwe alijipa tu Urais 2015?😂
Mimi sijasema ni jiwe, wewe wasemaUnadhani huyo Jiwe alijipa tu Urais 2015?😂
Samia ni rais bora kuliko wote watano waliomtangulia, kafanya na anafanya mengi kuliko matarajio yetu, wengi wetu hatuwezi kuyafahamu kwa sababu ni watu wa miji mikubwa Arusha, Dar, Mwanza na Mbeya huko vijijini kabadilisha sana hali za kiuchumi na ustawi wa kijamii umeongezeka ubora wake.Tutaongea yote ila jiwe ndiye chanzo cha haya yote na ndiye aliyetufikisha hapa tulipo leo. Jini akishatoroka kwenye chupa ni vigumu sana kumrudisha, ni rahisi sana kuboma kuliko kujenga.
Kwa mema yote na kwa mabaya yote akumbukwe.
Uvivu wa kufikiri tatizo la wengi humu jukwaani na huko mtaani.Wala hujaambiwa usahau au usieleze hayo mabaya ya Jiwe ila kinachosemwa hapa ni kwamba kushindwa kurekebisha hayo makosa ya Jiwe na kufanyika yenye kuonekana ni sahihi kwa wakati uliyopo badala yake tunabaki kuendelea kumlaumu tu huyo Jiwe, huo ndio ujinga tunaosema hapa.
Kama hatuna nia ya kurekebisha makosa yaliyoanzishwa wakati wa Jiwe sasa huku kuendelea kumlaumu huyo Jiwe kunasaidia nini? Maana hakuna tunachojifunza zaidi ya kuonyesha tu kwamba Jiwe alikuwa mtu mbaya basi ambalo ni suala la kihisia zaidi tu. Ataondoka Samia watakuja wengine ila bado tutaendelea na kumlaumu Jiwe.
Sasa kuna upumbavu zaidi ya huo?
Mbona ULIMBOKA, MWANGOSI na yale Muaji ya Arusha 2011 tunayasahau jamani?Mkuu Nyerere hakuteka na kuua kama Jiwe na Samia
Mwinyi na Mkapa walikua wana “shughulikia” kwa kukufungia mirija
Jk aliteka kidogo
Jiwe na mama wanakupoteza mazimaaaa
Kipi kimejaribiwa kurekebishwa na nani huyo anayerekebisha? Kama kumbe kuna misingi ya ukatili basi sasa kwanini tuliaminishana kwamba kufa kwa Jiwe ndio mwisho wa ukatili na tukafurahia? Membe alikuwa wa kwanza kusema mauwaji hayato endelea tena kisa Jiwe kafa.Tunajaribu kurekebisha lakini still bado watu wanapotezwa wakijaribu kwasababu ya misingi thabiti ya kikatili aliyoweka Jiwe
Huwezi kuujua uchungu na hasira kwa ujinga aliouleta jiwe kama una faidika na ujinga huu au kama akili yako ni finyu kujua ubaya wa haya
Hata siku ujinga huu ukiisha Jiwe ataendelea kuwa reference forevere
Uchawa pia ulianza kuchipukia hukoShida ilianzia Msoga, kipindi chake nayeye amekunywa sana damu za watanzania, ila watu wanamuona kama alikuwa Saint. Ufisadi wa kutisha, watu kuanza kutekwa hadharani muasisi ni huyu. Jiwe aliendeleza alichokuwa anakiona, mengine ndiyo kama haya sasa.
Yote haya yamekuwepo tangu enzi za Marehemu Nyerere. Kusifia bila kuhoji ndio ile habari ya 'zidumu fikra sahihi za mwenyekiti' na wote wanaitikia zidumuuu.Yafuatayo Ndio mambo yalioanza kwa jiwe.
1.Kusifia bila kuhoji
2..Bunge Kuwa kabisa chini ya serikari
3.Wasiojulikana
4.kuuwawa kwa wapinzani.
Hakika hili siyo la kupinga...wakati tunakumbuka mazuri yake tukumbuke pia na mabaya yake ambayo ndiyo yametufikisha hapa tulipo.Tutaongea yote ila jiwe ndiye chanzo cha haya yote na ndiye aliyetufikisha hapa tulipo leo. Jini akishatoroka kwenye chupa ni vigumu sana kumrudisha, ni rahisi sana kuboma kuliko kujenga.
Kwa mema yote na kwa mabaya yote akumbukwe.
Yote haya yamekuwepo tangu enzi za Marehemu Nyerere. Kusifia bila kuhoji ndio ile habari ya 'zidumu fikra sahihi za mwenyekiti' na wote wanaitikia zidumuuu.
Wabunge wote ni wa CCM na wachache wa upinzani bunge linakuwa ni muhuri tu, ilianza tangu 1995 lilipoanza bunge la kwanza la vyama vingi.
Wasiojulikana wapo siku zote, marehemu Kombe aliyekuwa bosi wa usalama wa taifa alipofuatwa kuuwawa alinyoosha mikono juu ikiwa ishara ya kukubali kukamatwa na bado akapigwa risasi akafa, hiyo ni miaka ya Mkapa, wakati wa Nyerere pale wizara ya mambo ya ndani ukikatiza kwa nje ulikuwa unaona banda lenye rangi nyekundu likiwa karibu na ukuta, mle palikuwa na chumba cha mateso kwa waliojitokeza kumpinga Mwalimu.
Wapinzani kuuliwa ni ngumu kuisema ikiwa ushahidi hauwezi kuwekwa wazi, zipo tuhuma kwamba Mzee Ndesamburo aliuliwa kwa mbinu za kiusalama nyumbani kwake Moshi.
Mkuu hawa kulaumu imekuwa kama kiburudisho tu kwao hawana nia ya kuona chochote kubadilika, wao wanachopenda kufanya ni kulaumu tu. Ndio maana sio ajabu kwao kuanzisha mada ya kumlaumu mtu ambaye hayupo tena.Uvivu wa kufikiri tatizo la wengi humu jukwaani na huko mtaani.
Kila rais anabebeshwa mzigo wa lawama, maana yake anayelaumu anayo matatizo ya msingi kwenye maisha yake ya kila siku.
Inasaidia nini ukiyakumbuka hayo mabaya ikiwa hauna nia ya kuyarekebisha?Hakika hili siyo la kupinga...wakati tunakumbuka mazuri yake tukumbuke pia na mabaya yake ambayo ndiyo yametufikisha hapa tulipo.
Kesi yao ya uhaini ilikuwa ya kwanza kabisa, ile ya kina Hans Pope ya 1983 ilikuwa ya pili.Mnasahau sana, enzi za nyerere wakina Kambona walihoji na kupinga Gavoo,Bibi Titi akiwemo
Kumlaumu marehemu ambaye hawezi kufikishiwa ujumbe ni zaidi ya maisha ya kivivu, wapo vijana wengi humu wanapenda kulaumu bila ya kutumia akili za kawaida tu.Mkuu hawa kulaumu imekuwa kama kiburudisho tu kwao hawana nia ya kuona chochote kubadilika, wao wanachopenda kufanya ni kulaumu tu. Ndio maana sio ajabu kwao kuanzisha mada ya kumlaumu mtu ambaye hayupo tena.
Sasa unasema vipi watu walikua hawahoji enzi hizoKesi yao ya uhaini ilikuwa ya kwanza kabisa, ile ya kina Hans Pope ya 1983 ilikuwa ya pili.
Habari zao hazikujulikana tofauti kabisa na namna kina Mdude Nyagali wanavyopitia magumu na kila mtu akifahamu nini kinaendelea.Sasa unasema vipi watu walikua hawahoji enzi hizo
Uko sahihi kwamba wananchi (kwa ujumla wetu) tuna wajibu kwa hili. Lakini kihistoria hatuwezi kuacha kuchambua na kugawa lawama kwa wote wanaostahili kwa kiwango kikubwa sana.Wa kulaumiwa ni sisi wananchi. Na hii ni kwa sababu tuna mawazo kama yako i.e. kudhani kuwa watawala watatuonea huruma na kuja na katiba nzuri bila sisi kuidai. Kwa hili tutasubiri sana. CCM jana wamesema ilani yao ina kipengele cha katiba mpya. Watch out! Itakuja katiba mbovu kuliko hii. Hii ni kwa sababu sisi wananchi tumekaa na kudhani kuwa watawala wataleta wenyewe. Kipindi cha Nyerere, katiba za nchi nyingi hasa Afrika zilikuwa siyo nzuri. Wananchi tuungane tudai na siyo kusubiri.
Chanzo ni Kikwete. Alimkomoa mwenzie Lowasa ambaye ndiye alikuwa awe Rais. Sasa hadi sasa yeye ndiye anaongoza kwa mlango wa nyuma.Jiwe aliondoa hata aibu na haya kidogo iliyokuwa imebakia kwenye huo mfumo.
Umedadavua vizuri sana mkuu.Uko sahihi kwamba wananchi (kwa ujumla wetu) tuna wajibu kwa hili. Lakini kihistoria hatuwezi kuacha kuchambua na kugawa lawama kwa wote wanaostahili kwa kiwango kikubwa sana.
Kifupi elewa tu kuwa kufanya marekebisho ya katiba yatakayoimarisha demokrasia nchini maana yake halisi ni kutenganisha chama tawala (CCM) na dola ili kiwe sawa na vyama vingine vya siasa kama CHADEMA, ACT, CHAUMMA, NCCR, n.k. Kwa watawala, hilo ni suala la kufa na kupona (existential threat). Ni tangazo la vita.
Sasa hivi wananchi tumegawanyika sana. Wako wengi sana wanaoamini katika kusubiri bahati ya kugawiwa fursa na rasilimali toka kwa walio madarakani. Hawa wanaamini walioko madarakani ni halali yao kufanya wanavyotaka ikiwa ni pamoja na kutumia hazina ya taifa wanavyojisikia.
Wako wengi zaidi ambao ni wanyonge kabisa wasio na uwezo wowote zaidi ya "kuchakarika" kujitafutia riziki na kuhakikisha hawana mikwaruzano yoyote na taasisi za udhibiti za serikali na vyombo vya dola. Hawa wengi wao ama hawaelewi haki zao au hawaoni kama ni busara kuzipambania kwa kukwaruzana na serikali na vyombo vya dola.
Wako wapambanaji wenye ujasiri wa kupigania haki. Hawa si wengi sana na huwa wananchi wengi hawajitokezi kuwaongezea nguvu. Hivyo mapambano yao yanaishia kukwama tu bila kuwa na matokeo ya maana.
Kwa kifupi hadi siku wananchi wengi zaidi watakapokuwa tayari kwa ujasiri mkubwa kuunganisha nguvu kukabiliana na dola ndipo hayo mageuzi yatafanikiwa. Naamini mwaka huu utakuwa kielelezo (indicator) kikubwa cha mwelekeo huo.
Inasaidia nini ukiyakumbuka hayo mazuri ukiwa huna nia ya kuyaendeleza?Inasaidia nini ukiyakumbuka hayo mabaya ikiwa hauna nia ya kuyarekebisha?