Katika yote hatupaswi kusahau aliyetufikisha hapa tulipo sasa

Katika yote hatupaswi kusahau aliyetufikisha hapa tulipo sasa

Tutaongea yote ila jiwe ndiye chanzo cha haya yote na ndiye aliyetufikisha hapa tulipo leo. Jini akishatoroka kwenye chupa ni vigumu sana kumrudisha, ni rahisi sana kuboma kuliko kujenga.

Kwa mema yote na kwa mabaya yote akumbukwe.
Legasi Legasi Legasi.
 
Mkuu uongozi n ulevi mauaji(sokoine),chuki,katiba mbovu yalianza tangu nyerere,hata huyu alipoingia akaanza na propaganda (oh! mm sio kama mtangulizi wangu).
N.B:Tusipo badili mifumo ya utawala,sera na sheria,katiba n.k hata malaika akiwa rais anageuka kuwa shetani
 
Yafuatayo Ndio mambo yalioanza kwa jiwe.

1.Kusifia bila kuhoji
2..Bunge Kuwa kabisa chini ya serikari
3.Wasiojulikana
4.kuuwawa kwa wapinzani.
 
Anayekufanyia ubaya yupo hai unamuogopa unakalia kumsema marehemu hahaha mama endelea kuwapa kipondo Hawa mbwa
Ni upumbavu bila mabadiliko ya kimfumo tutaendelea kulaumu.
 
Kila siku nasema, kipindi cha mwendazake ndio UCHAWA ulishika chart, uongozi wa UMUNGU MTU ulishika hatamu.
 
Wewe unadhani kwamba huu uuwaji na utekaji ni issue aliyohusika nayo Magufuli na sasa Samia?
Alivyokufa Magufuli basi Membe alikuwa wa kwanza kusema kuwa hakutakuwa tena na mauwaji.
sio Membe tu kila mdhalimu alisema kwamba sasa nchi imetulia, sasa kiko wapi watu bado wanaendelea kutekwa na kuuliwa au marehemu anatoa maagizo akiwa huko, Magufuli alisingiziwa mengi sasa hivi wanaumbuka
 
Ukiwa na akili timamu unaelewa chanzo cha haya ni nyerere aliye asisi mfumo wa chama kimoja na ujamaa uchwara, huku akipinga na kuwashughulikia watu wote wenye mawazo mbadala kama kambona, bibi titi, jumbe nk.
Yeye ndio alitengeneza mfumo wa mwenyekiti wa CCM na raisi kuwa Mungu mtu.
Walio fuata ni wanufaika wa huo mfumo ovu ambao wanautumia wanavyo penda na kujisikia.
Na wakati anang'atuka alikiri wazi kuwa katiba ni mbovu. Kwa kipindi hicho angeweza kuweka katiba bora pasipo kizuizi ndani ya Chama. Tunayoyaona sasa ni matokeo ya uzalendo kwa Chama kuwa juu ya uzalendo kwa nchi - kitu alichoasisi yule mzee.
 
Na wakati anang'atuka alikiri wazi kuwa katiba ni mbovu. Kwa kipindi hicho angeweza kuweka katiba bora pasipo kizuizi ndani ya Chama. Tunayoyaona sasa ni matokeo ya uzalendo kwa Chama kuwa juu ya uzalendo kwa nchi - kitu alichoasisi yule mzee.
Afu akawa anasema et atatuombea
 
Nyerere na Kawawa hawakuendeleza mabaya ya mkoloni.
Aliyefuata baada ya huyo umsemae anaweza kuchagua njia tofauti na mtangulizi wake.
No excuses!
 
Back
Top Bottom